Mishahara serikalini kulipwa dirishani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SERIKALI imetangaza kuwalipa watumishi wa umma mishahara yao kupitia madirishani kwa muda wa miezi miwili.

Katika kipindi hicho, itachukua hadhari zote ikiwamo ya kuhakikisha hakutokei uporaji mishahara hiyo ili kuwagundua watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, alisema hayo juzi mjini hapa kwenye mafunzo ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili.

“Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa,” alisema Ghasia.

Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20.

Kuhusu uboreshaji wa maslahi ya watumishi ikiwamo mishahara, alisema Serikali itaendelea kuiboresha kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.

Akiwa kwenye mafunzo hayo, Ghasia aliwataka watendaji wa halmashauri kusimamia vema fedha ili kuondoa mawazo kuwa halmashauri zimejaa wezi.

Kuhusu ajira, alisema kuanzia sasa mtu atakayefaulu usaili wa kazi katika utumishi wa umma na kupangiwa kituo cha kazi, hataitwa tena katika usaili wa kazi yoyote serikalini.

Alisema hiyo ina nia ya kukabiliana na watu ambao wanapewa kazi, lakini wanakwenda kuripoti vituoni na kuchukua fedha za kujikimu, kisha kutoweka.

Waziri Ghasia yuko katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya utumishi wa umma awamu ya pili na jana alitarajiwa kuwa Misenyi.
 
walishaliongelea siku nyingi sana na ilikuwa imebaki utekelezaji tu. You create more problems than you solve. Yetu macho
 
nimeiweka hii habari ili nijue je ni njia sahaha ya kubaini wafanyakazi hewa?kwasababu miaka kama 4 iliyopita wafanyakazi walikua wanachukulia dirishani na bado kulikua na wafanyakazi hewa kibao
 
Bongo bana, yaani hii ndiyo solution inayotolewa na waziri? Mshahara dirishani du? Sasa kama watendaji kwenye maeneo tofautitofauti hawaaminiki (This should be the case) kuassess idadi ya watumishi halali wataaminikaje kwenye kutoa hela dirishani? After all this is more tempting!!!!!!
 
na kuna wafanyakazi wapo mashuleni ina maana waache shule warudi kuchukua mshahara then waende tena vyuoni?mie sielewi hii serikali yaani miaka mingi sana wamelipa watu kupitia madirishani na bado kulikua na wizi sana kuliko hata sasa sijui wanachotafuta nini naona kama wanachezea pesa tu maana mishahara inaweza kutekwa au wafanyakazi wanaweza kutekwa wakiwa na mishahara na kisha kunyanganywa
 
SERIKALI imetangaza kuwalipa watumishi wa umma mishahara yao kupitia madirishani kwa muda wa miezi miwili.

Katika kipindi hicho, itachukua hadhari zote ikiwamo ya kuhakikisha hakutokei uporaji mishahara hiyo ili kuwagundua watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, alisema hayo juzi mjini hapa kwenye mafunzo ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili.

"Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa," alisema Ghasia.

Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20.

Kuhusu uboreshaji wa maslahi ya watumishi ikiwamo mishahara, alisema Serikali itaendelea kuiboresha kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.

Akiwa kwenye mafunzo hayo, Ghasia aliwataka watendaji wa halmashauri kusimamia vema fedha ili kuondoa mawazo kuwa halmashauri zimejaa wezi.

Kuhusu ajira, alisema kuanzia sasa mtu atakayefaulu usaili wa kazi katika utumishi wa umma na kupangiwa kituo cha kazi, hataitwa tena katika usaili wa kazi yoyote serikalini.

Alisema hiyo ina nia ya kukabiliana na watu ambao wanapewa kazi, lakini wanakwenda kuripoti vituoni na kuchukua fedha za kujikimu, kisha kutoweka.

Waziri Ghasia yuko katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya utumishi wa umma awamu ya pili na jana alitarajiwa kuwa Misenyi.
Siku zote solution ya mpuuzi huwa niya kipuuzii, kwani lazima ulipia mishahara dirishani ndio ujue watumishi hewa?????
 
Huyu mama kweli hamnazo!, anashindwa kufanya sensa makini ya watumishi laki 3 na nusu (kwa mujibu wa JK)?, MI ANIPE asilimia 1 ya hizo wanazotaka kuwagawia DOWANS nizunguke ofisi zote aone kama sitaleta data za uhakika akalinganishe na payroll yake!
 
Siku zote solution ya mpuuzi huwa niya kipuuzii, kwani lazima ulipia mishahara dirishani ndio ujue watumishi hewa?????
Hawa kweli amnazo mbona kuna very cheap and easy IT system ya kubaini watumishi hewa,hivi Serikali aina watu wa IT wakawashauri haya majua?
Masikini Tanzania
 
Siku zote solution ya mpuuzi huwa niya kipuuzii, kwani lazima ulipia mishahara dirishani ndio ujue watumishi hewa?????

You are damn right. Kuzuia wizi wa fedha sio kupambana na vidagaa wenye mishahara midogo, wangeanza na mapapa wanaoiba mabilioni. It is not a good idea to target the weak by less intellingent methods.
EPA, DOWANS ndio issues tunazotakiwa kupambana nazo.
 
hawana pesa ndio maana leo hii wanakumbuka hata kuna watumishi hewa
 
hivi jamani mtu km hawa ghasia ndo waziri mnategemea nini. kwa kweli tutaendelea kuwa maskini milele na milele amina!!!!
 
Yaani unataka hadi kulia. Hivi jamani hizo shule mlisoma haziwasaidii kitu? Can this be a solution really?
 
Hawana pesa hao ndiyo tapatapa yote hiyo na delaying tactic, baadae yatafuatia mauzauza kibao ya watumishi kukosa mishahara yao kwa kisingizio 'kuna makosa yalifanyika, tunarekbisha, tunaomba watuvumilie' wakilegeza inapita miezi. hii ndoo bongo.

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Hi,Madam,

Be careful with your strategy,mind you bandits are so clever,and now we are in the era of science and technology and you are taking back employee to the era of old age,technology is there to help you,consult ICT personnel,

Elisante
 
Yaani kugundua wafanyakazi hewa ndio mshahara ulipwe dirishani? Na waliopo shule na katika mafunzo mbalimbali watafanywaje?
 
Huyu mama huyu.....kweli karne ya 21 bado tunafanya haya madudu...hapo dirishani ndio atapigwa kwelikweli
 
Back
Top Bottom