Mimi sio fisadi - sitta

muheza2007

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
483
771
Mbona haongelei mambo ya CDA na TIC? Mambo ya kabla ya 80, karibu kila Mtanzania alikuwa mzalendo. Dawa ya milioni mbili, nyumba ya mabilioni, ni fisadi tu na yeye.

Sitta awaponda wanaosema yeye fisadi

Imeandikwa na Anastazia Anyimike;
Tarehe: 12th April 2010




SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema, maadui wake kisiasa wameshindwa kudhibitisha madai ya kuwa yeye ni fisadi.

Akizungumza kabla ya kuzindua programu ya Urejeshaji wa maadili kwa Umma (PIRI) unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sitta amesema, kama angekuwa na hata dola moja kwenye akaunti ya nje basi mpaka sasa adui zake wangeweza kuliweka peupe.


“ Maadui zangu wanapenda kunisema kuwa mimi ni mnafiki, na kama ningekuwa na dola moja nje ya nchi wangekuwa wameweka wazi, lakini sasa wameishia kusema natembelea benzi la gharama wakati si mimi ninayenunua, na hata waziri mkuu na Jaji Mkuu wanayo.


“ Pia wanasema kuwa ninaishi kwenye nyumba ya gharama, wameuza nyumba zote na nikipangishiwa wanasema inagharama kubwa.”


Sitta amesema, kama angekuwa fisadi basi angefanya hivyo tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya Kwanza kuwa Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano mwaka 1974.


“ Nikiwa na miaka 34, niliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano na nikahusika katika kununua ndege za abiria tatu huko Canada baada ya Jumuia ya Afrika Mashariki kuvunjika, tulipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo ( kwa wakati huo-Pierre Trudeau) aliniambia kunakamisheni ya dola za Marekani laki 3 na kupewa maelekezo hizo hela ziende wapi.


“ Kwa vile mimi nilikuwa na maadili, nilipiga simu nyumbani na Nyerere alinaimbia fedha hizo zichukuliwe na ndizo zilizosomeshea marubani wa kwanza wa ATC, lakini asilimia kubwa ya viongozi wa sasa wangepata nafasi hiyo fedha hizo zingekwenda mifukoni mwao.


Sitta aliongeza kuwa: “ Nilihusika kusaini mkataba ya ujenzi wa daraja la Salender mwaka 1981, barabara ya Moro-Dodoma mwaka 1983, ningeweza kupata fedha ambazo kwa sasa ningekuwa nawatemea mate, sio kama najivuna, mikataba yote hiyo sikuweza hata kujenga kibada. Mfano wa mikataba mibovu ni ule wa TRL.”


Amesema,kuna haja ya kuanza kufuata misingi iliyoweka na Nyerere inayozingatia usawa, kuwajali na kuwatumikia wanyonge, uadilifu na kuheshimu utu wa mtu bila kujali kabila, rangi, utajiri, jinsia au eneo wanaotoka ambayo imeifanya kuwa kisiwa cha amani na utulivu .


“ Hatuna budi kuidumisha misingi hiyo kwa nguvu zote kwa maslahi ya taifa na vizazi vijavyo. Nayasema haya kwa sababu zimeanza kujitokeza dalili na vitendo vya waziwazi vyenye mweleko wa kuibomoa misingi hii ambavyo ni rushwa, ufisadi, ubadhirifu, ubabe katika utawala na kuhubiri siasa za chuki. Vitendo hivi na vingine vimeanza kuzoeleka na kuwa sehemu ya utamaduni,”


Amesema,kwa muda mrefu taifa halikuwa na utaratibu rasmi wa kuandaa viongozi,wakati umefika kwa suala kupewa kupaumbele na uzito unaostahili kwa kuweka utaratibu wa kuandaa viongozi kwa kuwapatia nyezo na mafunzo katika nyanja za maadili, uzalendo na uadilifu.


“ Kizazi chenu kitafaidika na elimu ile, lakini wapo ambao kwa sasa ndio wanaoendesha mambo ya nchi ambao wataweza kutumia nafasi zao kutunga sheria za kukandamiza, na wale ambao wana miaka 40, ili watakapoaachia ninyi basi mambo yawe rahisi kwani kinyume cha hapo mtakapotaka kufanya mabadiliko basi mtaambiwa mnafanya mapinduzi.”


Pia Sitta ametaka programu hiyo ifike kwenye vyuo vya kati kama vyuo vya uwalimu, ufundi kutokana na kuwa navyo vinahusika kuzalisha wanafunzi wengi.


Sitta alisema ni vyema program hii ikafika katika ngazi za chini kama vijijini, kata na halmashauri ambao ndio waathirika wakuu wa mmomonyoko wa maadili.
 
=muheza2007;877598]Mbona haongelei mambo ya CDA na TIC? Mambo ya kabla ya 80, karibu kila Mtanzania alikuwa mzalendo. Dawa ya milioni mbili, nyumba ya mabilioni, ni fisadi tu na yeye.
Hebu tuhabarishe ni yepi hayo ya CDA na TIC? Kwa kuwa Serikali yetu siku zote inahitaji uwepo ushahidi wa kutosha wa kutukubalisha juu ya ufisadi wa kiongozi yoyote, tunakuchallenge umwage data hapa na ushahidi ili tuweze kumhukumu vizuri Mzee Six. Vinginevyo kaa kimya muacha afurahie uzalendo wake!

Gharama za tiba na nyumba ya mabilioni ni utaratibu tu ambao Serikali yetu tukufu imejiwekea ili wateule wake waishi kwa amani na starehe wakiwa pia na afya njema. Kosa si la Sita ni la utaratibu uliowekwa na Serikali. Umesahau kwamba Gavana wa Benki Kuu ambaye naye ni mteule wa Serikali yetu anavyotesa kwenye jumba la mabilioni lenye swimming pool? Je, la Mzee Six nalo lina vikorombwezo kama hivyo?

Tulilie mfumo na taratibu mbovu, kama wa viongozi waandamizi kupewa upendeleo uliokithiri unaotumia fedha nyingi za umma wakati wananchi walio wengi wanaumia.
 
Sikujua kuwa fisadi ni yule mwenye mapesa nje tu, na kama ni usafi wakati wa mwalimu hata baba wa mafisadi Mkapa kipindi hicho anaweza kusema hakuwa fisadi!
 
Hiki kinachoitwa ufisadi wa Mzee Sitta kingekuwa ni kweli leo hii Sitta angekuwa ameshafikishwa mahakamani maana hicho ndicho kingekuwa ni silaha ya mafisadi. Lakini kwa vile wenyewe wanajua kwamba tuhuma hizo ni kinga dhidi ya yale ambayo Mzee Sitta angesema hadharani. Kama mafisadi wana uwezo wa kuzua pale kunapokuwa hakuna kitu, definately haya yangekuwa ya kweli ungekuwa ndiyo mtaji wao mkubwa na sasa Sitta angekuwa keshazikwa kisiasa.

Alichokizungumza kuhusu zao la viongozi wa leo ndiyo ukweli na ndiyo motivation ya wengi kuingia kwenye uongozi wa nchi. Mzee Sitta endelea hivyo hivyo.
 
Kama kuna ushaidi wa hayo ya cda na mengineyo, tuwekeeni hapa.
 
Sikujua kuwa fisadi ni yule mwenye mapesa nje tu, na kama ni usafi wakati wa mwalimu hata baba wa mafisadi Mkapa kipindi hicho anaweza kusema hakuwa fisadi!

Sawa lakini hiyo haimaanishi kwamba kila aliyekuwepo wakati huo na sasa ni kiongozi basi yeye ni fisadi. Kwa ujumla hakuna hoja katika tuhuma dhidi ya Sitta zaidi ya chuki dhidi ya Sitta mwenyewe.
 
Back
Top Bottom