BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Wana JF, heshima mbele.
Nina rafiki yangu wa karibu mno kiasi cha kuitana ndugu. Alifunga ndoa mwaka jana october. Mwisho wa mwezi December mkewe akapata ujauzito. Kazini kwake ni Mikoani lakini yuko Dar kimasomo. Jamaa anasoma masters na mrs ni graduate and degree moja.
Mwezi november alienda kazini kwake akiwa anashughulikia ujenzi wa nyumba yake ambayo sasa anapaua, akakaa mpaka january.
Hakupanga chumba ila akawa amefikia kwa rafiki yake wa karibu sana ambaye ana nyumba kubwa ambako muda wote amekuwa akifikia hapo, tangia aende masomoni, ukizingatia kuwa wakati wa kwenda shule alirudisha nyumba aliyokuwa amepanga.
Tatizo lake, mkewe tangu apate mimba hataki kumwona wala kusikia sauti yake. She just hate him. Hivi majuzi mkewe alipangiwa kutuo cha kazi hapo hapo ambapo ni karibu na kazini kwa jamaa, baada ya jamaa kuhangaikia ili awe karibu na mkewe. Kwa kuwa alikuwa Dar, akamuomba huyo rafiki yake kuwa mkewe aendelee kukaa kwake kwa muda wakati anamalizia finishing ya nyumba yake. Jamaa akamkubalia na huyo mwanamke akaja. Ikawa jamaa akimpigia simu mwanamke hapokei, msg hajibu, akitumiwa hela hata hasemi kama amepata na hakuna kumshukuru kwa jinsi amavyomjali sana.
To make story short, wakakaa siku nne hakuna mawasiliano, jamaa akaamua kumtafuta huyo mwenye nyumba ili amfikishie ujumbe. Siku iliyofuata, binti akachukua taxi akachukua kilicho chake akakomba kila kitu akaondoka wakati mwenye nyumba hayupo, akaaga kwa majirani kuwa anaenda kuripoti kazini then anasafiri. Mumewe alipoanza kumtafuta mwenye nyumba akatoa ripoti kamili, jamaa akapigwa na butwaa. Kumbe huyo mwanamke hakusafiri wala nini, ni kwamba alipanga chumba sehemu nyingine. Jamaa alipoona hivyo, akapanda gari kuja kushuhudia kilichotokea, wakanza kumtafuta binti next day wakisaidiana na mwenye nyumba huyo, binti alivyogundua kuwa mumewe kaja, yeye akapanda gari kwenda Dar, wakati jamaa yuko mkoani.
Jamaa yangu huyu amechanganyikiwa wadau nimsaidieje?