Ushauri: Rafiki yangu katelekezewa watoto mlangoni

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,210
Kuna jamaa yangu Ni mkandarasi serikalini, mkewe Ni mtendaji. walijenga hapa Dar baadae jamaa kaja kuhamishiwa mkoani kikazi, ikabidi mkewe nae kikazi ahamie huko huko mkoani wilaya alipo Mumewe. Hivyo nyumba Yao ya Hapa Dar wakaipangisha.

Mwaka juzi jamaa alikuja kupata kesi fulani uko kazini kwake mkoani, hivyo nafasi yake akateuliwa mtu mwingine, nae akatakiwa kuripoti makao makuu Mara Moja, ila matumaini ya jamaa Ni kwamba atapangiwa majukumu mengine.

Hivyo Jamaa hakuona umuhimu wa Kurud Dar na familia nzima akisubiri kujua atapangiwa wapi Tena. Hivyo nae akatafuta nyumba nyingine akapanga hapa hapa Dar, mkewe akimuacha kule kule mkoani.
 
Muda ulivozidi Kwenda yupo yupo tu makao makuu na hapangiwi Kazi nyingine, na bado kesi yake kule mkoani inamvuruga kichwa ikambidi yule mpangaji wake Kodi ikiisha asipokee Tena Kodi yake. Hivyo kumpa notisi kwa Nia ya kuhamia kwake mwenyewe, lengo Ni apunguze gharama za maisha.

Akiendelea kuishi apa Dar mwenyewe, akaja kuingia kwenye mahusiano na binti mmoja Ni mwalimu wa shule ya msingi. Mahusiano yao yalianza kuingia mgogoro binti alivopata tu mimba ya jamaa. Na mgogoro wao mkubwa ulikua Ni suala zima la pesa.

Kwa maelezo ya jamaa Ni kwamba madam haridhiki na anachohudumiwa, anaomba pesa za matunzo kuliko uwezo wake, asipopewa Ni migogoro juu ya migogoro.
 
Kama mtu wake wa karibu nikamshauri amvumilie tu, asijibizane nae, ahudumie kilicho ndani ya uwezo wake. Itakua Hali ya mimba ndo inampelekesha, akishajifungua atakua kawaida, Jamaa kasema sawa.

Ilipofika mwaka Jana mwanzoni, madam kajifungua mapacha na hapo ndio migogoro Yao ikafika pabaya pale ambapo binti akawa anataka kulazimisha akaishi kwenye nyumba kubwa Ya jamaa anayoishi peke ake na sio kule kwake alikokua anaishi kwenye Chumba kimoja na sebule, uswahilini kidogo.

Jamaa akamweleza haiwezekani kuishi pale kwake maana ile Nyumba ni ya yeye na mkewe alieko mkoani, huyu madam hawezi kuja kuishi apa, italeta mgogoro sana Kwenye ndoa yake. Madam akawa ana ng'ang'ana Sana, ikabidi Watu wake wa karibu tukae na madam tumwelekeze vizuri Hali halisi na awe mwelewa. Madam kaelewa.

Ila madam akaomba kupangishiwa nyumba nzima sehem nyingine ili alee wale mapacha wake vizuri, kule alikopanga uswahilini mazingira hayaridhishi. jamaa akalalama Sana Hana Ela ya kumpangia nyumba nzima, uchumi wake umeyumba Sana kwa Sasa.
 
Watu wake wa karibu tukamweleza tayar ushayakanyaga brother, heri nusu Shari kuliko Shari kamili, pambana ulipie tu Kodi binti akae kwa kutulia. Jamaa akawa analipa Kodi kwa binti na Matumizi mengine akaendelea kutoa Kama kawaida.

Baada ya mwezi tu tangu madam ahamie makazi yake mapya, tukasikia jamaa anaitwa ustawi wa jamii, anashtakiwa na binti, kesi Ni katelekeza Watoto wake mapacha, hatoi matumizi yoyote ya watoto. Duh! Tukashangaa.

Binafsi Nikamuulza jamaa vipi, akasema matunzo anatoa ila sio Kama zamani maana sasa hivi kayumba Sana kiuchumi ukizingatia kazini kwake kule ana kesi, inamtafuna sana pesa kuizima, na yupo yupo tu, anafika kazini anasaini na kuondoka, kwasasa Hana mishe za zozote za kumuingiza pesa mjini.
 
Nikamwambia kuyumba haiwez kua excuse ya kutokutoa matumizi ya watoto wako, Kama mwanaume pambana uwezavyo utunze hizo damu zako. Haijakaa vizur umezaa afu utoi matunzo, Tena watoto wenyewe hao ni mapacha. Nawajua vzur changamoto zao,maana mi mwnyw pia ninao mapacha.

Jamaa akasema hapa Juzi kati ndo katoka kulipa Kodi ya pango milioni 1.2 kwa miez 6 pale alikohamia binti. Sasa madam akiachiwa ela ya kula kwa siku chini ya elfu 20 anazisusa, hazitaki, anazirudisha, anadai haziwez kutosha chochote kile ndani kwake.

Na Kuna mda anamtupia kabisa usoni, aondoke nazo,kwaiyo nae ndo akaamua kama mbwai iwe mbwai ,kususa kutoa kabisa. Ikabd kumpigia madam mwnyw kuthibisha maneno ya jamaa, seriously madam akasema pesa anayopewa na jamaa Ni ndogo Sana, kwaiyo haoni sababu ya kuipokea, Bora ijulikane hajapewa kabisa matumizi kuliko kukadiriwa pesa ya matumizi Kama Mabinti wa kuokota mitaani.
 
Nikamuulza madam Kama anaijua Hali halisi ya jamaa kwa Sasa kiuchumi, madam akanijibu kwamba Hilo halimhusu, anachojali Ni afya ya watoto wake Kwanza, Kama hawamhusu jamaa Basi aweke wazi maana vyombo vya Sheria vipo, haki yake itapatikana.

Duh! Kimoyomoyo nikajua huyu madam Ni mshari Sana, ila sioni tatizo kwa jamaa. Basi ikabd kumkatisha madam, niongee kwanza na jamaa afu ntampa mrejesho. Madam akasisitiza Kama hawezi kutoa matumizi kwa hiari, Basi anakoelekea atatoa matumizi kwa shuruti. Nikamsihi madam asifike uko. Madama akaikata simu.

Nikarudi kwa Jamaa,
Jamaa akanisisitizia kwamba huwa anatoa, Sema ndo hivyo kwasasa sio Kama zamani, madam haelewi na Mambo yameyumba Sana. Nikamsihi akifika uko ustawi wa jamii awaeleze Hali halisi alivyo asifiche. Akanijibu sawa, nikaagana nae, kaelekea zake ustawi wa jamii, nikaelekea kwny shughuli zangu.

Baadae Kwa maelezo ya Jamaa,
Ni kwamba alivofikishwa ustawi wa jamii akawaeleza Hali halisi, kule akapangiwa kutoa elfu 70 kwa mwezi. Na walipotoka kule, jamaa akayasimamia vile yalivyo Yale maelekezo ya ustawi wa jamii na kweli akawa anampatia madam elfu 70 tu kwa mwezi mzima, yaani mwezi Hadi mwezi, anatoa elfu 70 cash.
 
Madam akaona 70 haitoshi,imekua ndogo sn kuliko ata ile ya mwanzo elfu 10-20 kwa siku aliyokua akipewa na jamaa, akaenda kumshtaki jamaa ofsini kwake kwa wakubwa zake. Kule jamaa kaitwa na kakiri kweli kazaa nae ila Hali yake kiuchumi haiko sawa. Wakubwa zake wakakomaa madam lazma apate haki Yake ili alee watoto wake vizuri.

Ilipofika mwisho wa mwezi jamaa kashtuka vp anapata posho yake pungufu ya 150,000, kuuliza kwa wakubwa zake vipi, akaambiwa wazi kwamba imekatwa Moja kwa Moja na Kwenda kwenye account ya mzazi mwenzie, yule madam maana kaonyesha ukaidi hataki kuzihudumia damu zake. Jamaa ikambidi kua mpole.

Sasa jamaa Kurudi kwa binti, kashangaa mwanamke anachekelea sana na kufurahi kana kwamba kilichofanyika dhidi Yake kule kazini kwake Ni kizuri. Akamweleza kabisa alichokisababisha kule kazini kwake hajakipenda kabisa, haya sio maisha ya kuishi na mzazi mwenza.

Madam akachekelea Sana na kumwambia wazi kwamba nae kalipiza alichokifanya kule ustawi wa jamii alikoandikiwa elfu 70, kwaiyo sahivi ngoma Ni droo droo, yeye ana konection Kali Sana na asithubutu Tena kumjaribu. Sahv Moyo wake umesuuzika Sana, pesa yake ya matunzo ataipata kwa wakati

Jamaa akamwambia madam kwamba kilichotokea na jins anavofurahi, maamuz aliyochukua mahusiano Yao Ni bora yaishie Apo apo,hamna maelewano Tena baina yao. Madam akamjibu jamaa kwamba hata haimstui, yeye akwende zake uko maana tayar anao uhakika wa 150,000 KILA mwisho wa mwezi. Jamaa kasema POA, akakata mawasiliano kabisa na madam
 
Leo asbh nashangaa jamaa ananipigia simu Yuko getini kwangu anashida, ananiomba Mara Moja. Nmeamka natoka nje kumskiliza namkuta jamaa kabeba Watoto wake wawili mapacha anasema yule mwalimu kamtelekezea hawa Watoto mlangoni kwake alfajiri anadai maisha ni magumu Sana, hawezi Tena kuendelea kulea hawa Watoto peke Yake.

Nikamuulza jamaa kwani ile pesa waliyokua wakukakata kazini na kumuingiza binti kwny account yake ilisitishwa? Akamjibu "hapana bado nakatwa, anaingiziwa binti". Wote tukabaki na mshangao inakuaje binti anafanya kitendo kama hiki.

Hatua nilizochukua,
Nikamshaur jamaa Kwanza Hawa Watoto wake wabaki apa kwangu, MKE wangu atawaangalia. Kisha mimi nikalitolee ripoti uongozi wa mtaa au polisi na yeye akalitolee taarifa kwa maboss wake uko kazini kwake.

Upande wangu nmeshatekeleza suala la taarifa, mwanamke kapigiwa sana na simu yake haipatkani mpk Sasa, na kazini kwake tumetafuta hayupo, simu tumepiga mpk tumechoka.

Maswali nilobaki nayo kichwani zaidi Ni utimamu wa akili za huyu mwanamke.

Kwa maana alililia matunzo ya Watoto anayopewa hayatoshi mpaka akapigania mwanaume amekatwa posho yake kule kazini kwake 150,000 KILA mwezi kwa lazima ili kugharamia matunzo ya watoto na yeye akalifurahia sana Hilo, Tena kwa ngebe kabisa.

Imekuaje sahivi analeta pigo za kutupiana Watoto wachanga vibarazani, Tena alfajiri kabisa na mvua hizi zinazonyesha za masika.

WAKUU KAMA KUNA LA KUSHAURI, nawakaribisheni NI RUKSA,

ILA MPAKA JIONI HII NMERUD NYUMBANI KWANGU NMEKUTA WATOTO WA JAMAA WAKO SALAMA SALMINI MIKONONI MWA MKE WANGU MAMA G

Nawasilisha
 
Leo asbh nashangaa jamaa ananipigia simu Yuko getini kwangu anashida, ananiomba Mara Moja. Nmeamka natoka nje kumskiliza namkuta jamaa kabeba Watoto wake wawili mapacha anasema yule mwalimu kamtelekezea hawa Watoto mlangoni kwake alfajiri anadai maisha ni magumu Sana, hawezi Tena kuendelea kulea hawa Watoto peke Yake.

Nikamuulza jamaa kwani ile pesa waliyokua wakukakata kazini na kumuingiza binti kwny account yake ilisitishwa? Akamjibu "hapana bado nakatwa, anaingiziwa binti". Wote tukabaki na mshangao inakuaje binti anafanya kitendo kama hiki.

Hatua nilizochukua,
Nikamshaur jamaa Kwanza Hawa Watoto wake wabaki apa kwangu, MKE wangu atawaangalia. Kisha mimi nikalitolee ripoti uongozi wa mtaa au polisi na yeye akalitolee taarifa kwa maboss wake uko kazini kwake.

Upande wangu nmeshatekeleza suala la taarifa, mwanamke kapigiwa sana na simu yake haipatkani mpk Sasa, na kazini kwake tumetafuta hayupo, simu tumepiga mpk tumechoka.

Maswali nilobaki nayo kichwani zaidi Ni utimamu wa akili za huyu mwanamke.

Kwa maana alililia matunzo ya Watoto anayopewa hayatoshi mpaka akapigania mwanaume amekatwa posho yake kule kazini kwake 150,000 KILA mwezi kwa lazima ili kugharamia matunzo ya watoto na yeye akalifurahia sana Hilo, Tena kwa ngebe kabisa.

Imekuaje sahivi analeta pigo za kutupiana Watoto wachanga vibarazani, Tena alfajiri kabisa na mvua hizi zinazonyesha za masika.

WAKUU KAMA KUNA LA KUSHAURI, nawakaribisheni NI RUKSA,

ILA MPAKA JIONI HII NMERUD NYUMBANI KWANGU NMEKUTA WATOTO WA JAMAA WAKO SALAMA SALMINI MIKONONI MWA MKE WANGU MAMA G

Nawasilisha

kwani ungeiweka story yote kwene page moja ungepungukiwa na nn
 
Pole kwa jamaa..
Wife ake anaichukuliaje huu ishu?? Coz namuona jamaa anapoteza kote
Huu ni ukweli sababu ya tamaa zake za kipimbavu anavunja ndoa yake. Na hata kama ikiendelea haitakiwa kama mwanzo.

Moja, amshauri Mke wake wauze hiyo nyumba ya pamoja wahame sehemu nyingine.
Lakini tatizo litakuja kwa hao watoto bado wadogo kama mama yake yupo atafute mtu atakayeweza kulea hao watoto.

Huyo binti atamuharibia kazi, ndoa na atakuwa

😂😂Kwa kweli kila nikijaribu kufix naona bado kuna pwaya
 
Back
Top Bottom