Milioni 300 za mtandao zatumika kummaliza Makongoro Nyerere; kisa...

“Makongoro anadaiwa kuwa,
mwaka 2010 hakwenda Musoma
Mjini na alipotakiwa kumkana
mgombea wa Chadema kwamba
si ndugu yake alikataa.
“Makongoro alisema, Vicent ni
mdogo wake mtoto wa baba
yake mdogo mzee Kiboko, hivyo
hayuko tayari kumkana ndugu,
kwa sababu za kisiasa, kilisema
chanzo hicho...huu ujinga bilasha ulihasisiwa na kuratibiwa na Wasira,uliposhidwa kufanya kazi huko Musoma akaupeleka Arumeru pia nako ukafail,bila aibu akutumia tena kwa watoto wa kaka yake akawakana mara tatu kabla ya jua halijazama...mtu mnafki kama huyo ndo leo ni waziri!...
 
binafsi najipenda kuzaliwa mtanzania, nchi ambayo ni mabingwa wakutengeneza maneno ya kunogesha mabaraza yetu. uchaguzi wa kitaifa mgombea akishindwa huja na lugha ya kunogesha baraza nimeibiwa kura mimi ndiye niliyestahili kushinda, chaguzi ndani ya CCM mgombea akishindwa mtandao umenimaliza jamani, nilistahili kushinda msemo mwingine mafisadi wamenimaliza ,tukubaliane kwa pamoja jembe la ukweli litalima tu popote,propaganda za kizushi tuache baada ya kushindwa[kuzidiwa kura] hata wewe ni mshindi je? waliokupa kura uliwanunua? maneno ya mheshimiwa MKAPA yananifariji ;tuache kuishi kwa hisia . kuna mchungaji mmoja wa kanisa la sabato naye alinifurahisha saana anasema; siku hizi watu wanaogopa hata kutoa misaada kwa wenzao kwa kuogopa kuitwa freemason.
 
Waende zao huko, hivi ni lazima wafanye siasa? Aende kwenye mashamba ya mzee akalime huko!!!!
 
Kama ni za ukweli na uhakika mbona unasema mzee flani? kwanini usiwataje majina. Ni kitu gani unachokiogopa kuwataja majina?

Kama unashindwa kuwataja majina inamaanisha huna ushahidi ni majungu tu

mzee flani si yule naniliu yule mwenye MA-MVI kichwani banaa...........
 
mZEE FLANI AU lOWASSA??ACHENI KUZUNGUKA MBUYU WANDUGU
ukiona mtu anajiumauma ujue ni mzee wa kunzia miaka 55 kwenda juu. ni waoga kupitiliza. wengi wao wanaiogopa ccm kuliko hata MUNGU.wamejazana huko usidhani wana mapenzi ya dhati kumbe ni wanafiki tu.vijana nchi hii ni yenu, ukweli tu ndio utawaweka huru.tumefika hapa kwasababu ya undumila kuwili,kuweni huru, mwizi na aitwe mwizi, mla rushwa na atajwe na chama kinacho boronga na kipigwe chini.
 
Hii Ant-CCM nayo imeingiwa Kirusi wakuu! Eti kila kura ilikuwa inanunuliwa shilingi milioni..... ndo nini? Yaani sisi ndo tumalizie? Nyamb...f! Mara ooh ndugu yake aliyekuwa anagombea upinzani 2005, ni nani huyo kama siyo uongo huu? Eti mzee flani! Wewe ni Kirusi.
 
Shilingi milioni mia tatu {300mil} zatumika na wana mtandao ili kumwangusha mtoto wa rais wa kwanza wa Tanzania.

Inaelezwa kuwa kura moja ilinunuliwa kati ya shilingi, kisa cha kumchezea mchezo huo mchafu ni tukio kilichotokea mwaka 2005 katika uchaguzi mkuu,ambapo baadhi ya wana CCM walimtaka Makongoro amkane ndugu yake ambae wakati huo alikuwa akigombea ubunge kupitia upinzani. Jambo ambalo Makongoro alilipinga vikali na kuwajibu kuwa hawezi kumkana ndugu yake huyo kwa sababu za kisiasa wana CCM hao walimjengea hasira na kuamua kumsulubisha. Na kali ya mwaka ni hii. Hili limatokea Arusha,baada ya uchaguzi wa CCM uliofanyika katika hoteli ya Naura Spring ambao ulikuwa chini wa mzee flani.

Baada ya uchaguzi ule kufanyika kwa mafanikio makubwa mzee flani huyo aliwachukuwa wazee wa CCM ambao walionekana kuwa naye bega kwa bega katika kumsafishia mzee flani huyo njia ya kwenda ikulu na kuwapeleka mapumzikoni katika hifadhi ya Tarangire kwa siku tatu. Habari hizi nimezipata toka kwa mzee mmoja ambae na yeye alikwenda katika mapumziko hayo ya siku tatu. Chai ya asubuhi, ya saa nne, chakula cha mchana na usiku,malazi kuwalipa maguide pamoja na magari na kiingilio kwenye hifadhi, gharama zote hizi zilikuwa chini ya mzee flani huyo.

Mzee huyo anasema walikula na kunywa kadiri watakavyo na mwisho wa safari walipewa bahasha kila mmoja.

Habari hizi ni za kweli na uhakika.

.
Afadhali hata ungesema kuwa kaangushwa na mafisadi kwa sababu ya msimamo wake ndani ya vikao vya ccm dhidi ya mafisadi. Maana nakumbuka huyu Makongoro alikuwa mwiba mchungu kwa mapacha watatu.
.
 
.....hivi makongoro nyerere ni mtoto wa mwenye heri jk nyerere, hivi naye anavuta bangi(cdm)................
 
Makongoro alijiua mwenyewe kisiasa alipotoka NCCR Mageuzi wananchi hawamwelewi tena yeye ni mtoto wa Nyerere siyo Julias so anakula matapishi yake sasa
 
Hivi Lowassa na timu yao wana monitoring mechanism ipi ya kuwafanya waliohongwa hizi pesa kupiga kura (ambayo ni ya siri) kwa mtu wanayemtaka wao? maana yake unaweza vuta mshiko na ukapiga kura kinyume na matakwa yao.
 
Shilingi milioni mia tatu {300mil} zatumika na wana mtandao ili kumwangusha mtoto wa rais wa kwanza wa Tanzania.

Inaelezwa kuwa kura moja ilinunuliwa kati ya shilingi, kisa cha kumchezea mchezo huo mchafu ni tukio kilichotokea mwaka 2005 katika uchaguzi mkuu,ambapo baadhi ya wana CCM walimtaka Makongoro amkane ndugu yake ambae wakati huo alikuwa akigombea ubunge kupitia upinzani. Jambo ambalo Makongoro alilipinga vikali na kuwajibu kuwa hawezi kumkana ndugu yake huyo kwa sababu za kisiasa wana CCM hao walimjengea hasira na kuamua kumsulubisha. Na kali ya mwaka ni hii. Hili limatokea Arusha,baada ya uchaguzi wa CCM uliofanyika katika hoteli ya Naura Spring ambao ulikuwa chini wa mzee flani.

Baada ya uchaguzi ule kufanyika kwa mafanikio makubwa mzee flani huyo aliwachukuwa wazee wa CCM ambao walionekana kuwa naye bega kwa bega katika kumsafishia mzee flani huyo njia ya kwenda ikulu na kuwapeleka mapumzikoni katika hifadhi ya Tarangire kwa siku tatu. Habari hizi nimezipata toka kwa mzee mmoja ambae na yeye alikwenda katika mapumziko hayo ya siku tatu. Chai ya asubuhi, ya saa nne, chakula cha mchana na usiku,malazi kuwalipa maguide pamoja na magari na kiingilio kwenye hifadhi, gharama zote hizi zilikuwa chini ya mzee flani huyo.

Mzee huyo anasema walikula na kunywa kadiri watakavyo na mwisho wa safari walipewa bahasha kila mmoja.

Habari hizi ni za kweli na uhakika.

wajumbe wa NEC hiyo 2015 watatengeneza mitaji kweli kweli katika kinyang'anyiro cha kuwapitisha wagombea urais. EL na timu yake sijui watagawa ngapi ngapi. Membe nae itabidi ajitahidi kupanda dau zuri. mjumbe mmoja wa NEC anaweza kujikuta anarudi nyumbani na mil 500 namna hii.
 
Back
Top Bottom