Mikoa Mipya 3 ya Tanzania

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Mikoa mitatu iliyoanzishwa mwaka jana kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ni:

Mkoa wa Njombe
ambao unaundwa na wilaya za Njombe, Ludewa na Makete ambazo awali zilikuwa ndani ya Mkoa wa Iringa na wilaya mpya ya Wanging’ombe sehemu ya iliyokuwa wilaya ya Njombe.

Mkoa wa Geita unaoundwa na Wilaya za Geita (iliyokuwa mkoa wa Mwanza), Bukombe (kutoka Mkoa wa Shinyanga) na Chato (iliyokuwa ya Mkoa wa Kagera). Mkoa huu pia una Wilaya mpya ya Nyang’hwale (imetokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Geita).

Mkoa wa Simiyu ambao unaundwa na Wilaya za Bariadi, Meatu na Maswa (zilikuwa za Mkoa wa Shinyanga), Wilaya mpya ya Busega (awali ilikuwa mkoani Mwanza na Wilaya ya Itilima (inatokana na kugawanywa kwa iliyokuwa Wilaya ya Bariadi).

Kwa mamlaka aliyopewa, Rais anaweza kuigawa nchi katika mikoa au Wilaya ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya mikoa mama ili wananchi wapate huduma za kiutawala ngazi ya mikoa kwa karibu.
 
Shukrani kaka kwa taarifa nilikuwa sijui kama kuna mikoa zaidi ya 26 ya Jamhuri ya Muungano Tanzania,sijui sasa makao makuu ya hiyo mikoa ni wilaya zipi kati ya zinazounda hiyo mikoa,na sijui wakulu wa hiyo mikoa na wakulu wa wilaya hizo ni akina nani,au bado mkulu anangpjea kutoa sandakalawe kwa wateule wa njii hii wachache
 
X-PASTER MIKOA ILIYOUNDWA NI ZAIDI YA 3:
1. Njoruma
Ludewa
Makete
Njombe
Wanging'ombe

2.
Katavi
Mpanda
Kaliua
Mlele

3.
Simiyu
Bariadi
Itilima
Meatu
Maswa
Busega
4.
Geita
Geita
Nyang'hwale
Mbogwe
 
Sidhani kama nia ni kutaka kufikisha maendeleo kwa urahisi kwa wananchi kama inavyodaiwa mi nao ni kuongeza ghalama zisizo za msingi na kuitwika serikali mzingo zaidi.
 
Napenda mnijuze je ni mikoa 3 au 4 naona mkoa wa Katavi hautajwi au mpango wa kuwa mkoa umefutwa? Mikoa inayotajwa ni Njombe,Geita Na Simiyu lakini Katavi hatajwi why?
 
Naomba niwaambie ukweli ndugu zangu, hakuna kitu kama hicho cha mikoa mipya wala wilaya mpya kwa sasa, zile zilikuwa ni danganya toto ili Kikwete aweze kupata kura wakati tukielekea uchaguzi mkuu kwani hali yake ilikuwa mbaya sana. Ushahidi ni katika bajeti itakayosomwa bungeni muda si mrefu ambayo inahusu mikoa 21 tu na soma hapa Bajeti ijayo haiitambui mikoa mipya Kikwete mkweere ni msanii mno na hana uwezo wowote wa kiuongozi. Mwalimu Nyerere aliona mbali sana 1995 kumkataa yeye na swahiba wake Lowassa. ndiyo maana akasema "Kama unaupenda uzuri wa sura yake mkaribishe nyumbani kwako umpe chai" lakini si kwa uongozi.

Nasema hakuna mikoa mipya!....
 
Back
Top Bottom