Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Nionavyo mimi Muungwana angetupatia kwanza ile list ya wauza unga na wala rushwa kama alivyohaidi kabla ya kutuanzishia topic mpya ambayo inafahamika wazi haiwezi.Wananchi tunamachungu na masuala ya RADA, vikampuni vya mfukoni vya Umeme vilivyojaa pale ubungo Tanesco na masuala mengine ya msingi.
Please JK punguza Usaniinaization, Taifa unalipeleka pabaya!!
 
Labda sasa wanashtuka na kuchukua hatua...wakiendelea hivi watatutia moyo...

Pia hongera waziri kwa "kupunguza" mgogoro huko Kahama kwa kuruhusu kijiji kiendelee kuwepo sanjari na mgodi wa dhahabu.

Serikali yaachana na Alex Stewart

Na Midraji Ibrahim

WIZARA ya Nishati na Madini, imesema haitaongeza mkataba wa ukaguzi wa madini na Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) badala yake, itatumia wataalam wake wa ukaguzi.

Akiwasilisha taarifa ya serikali katika Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema wizara itahakikisha inajenga uwezo wa wataalam wake kufanya kazi hiyo.

"Baada ya mkataba wa Alex Stewart (Asseyers) kumalizika mwaka huu, hatutakuwa na ulazima wa kuendelea na makataba huo. Mchakato wa kuendeleza ukaguzi kama huo kwa wataalam wetu umeishaanza," alisema Ngeleja.

Kutokana na utekelezaji wa shughuli za ukaguzi kwenda kama ilivyopaangwa katika awamu ya pili ya mkataba, Ngeleja alisema, kuna matarajio sehemu kubwa ya kazi itakuwa imekamilika ifikapo mwishoni mwa kipindi cha mkataba huo.

Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wabunge na wananchi juu ya kuibiwa kwa dhahabu inayozalishwa na kampuni kubwa za kigeni kwa sababu ya kutokuwepo kwa usimamizi na udhibiti wa uchimbaji na biashara ya madini hayo.

Juni 14,2003, serikali kupitia Benki Kuu (BoT) iliingia mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya ASAGBC wa kufanya ukaguzi wa dhahabu katika migodi mikubwa ya dhahabu nchini; Bulyanhulu, Geita, North Mara, Goldenen Pride na Buhemba.

Ngeleja alisema, kulingana na mkataba huo, majukumu makuu ya ukaguzi yalikuwa ni kuchambua na kupitia utaratibu unaotumika katika uzalishaji, usafirishaji wa madini nje ya nchi na uendeshaji wa shughuli za madini nchini.

Majukumu mengine ni kuhakiki dhahabu inayozalishwa na kusafirishwa nje ya nchi na kampuni kubwa, ili kubaini usahihi wa ulipaji wa kodi na mrabaha kwa serikali unaofanywa na kampuni hizo;

Kuhakiki gharama za uwekezaji na uendeshaji wa migodi kama ilivyoainishwa katika mipango ya biashara ya migodi hiyo na kukagua na kuhakiki shughuli za utunzaji wa mazingira na gharama zake.

Hata hivyo, Ngeleja alisema kazi ya kuchambua na kupitia kanuni na taratibu zinazotumika katika uzalishaji, usafirishaji madini nje ya nchi na uendeshaji, haikukamilika kutokana na mkaguzi kuwasilisha taarifa yenye upungufu.

Ngeleja alisema, kutokana na kutokamilika kwa shughuli za mkaguzi kama ilivyoainishwa kwenye mkataba, Mei 28, 2005, BoT iliongeza mkataba wa kuongeza muda wa miaka mingine miwili.

Alisema kazi ya uhakiki imekuwa ikiendelea vizuri na taarifa za kila mwezi zinaonyesha kuwa takwimu zinazotolewa na kampuni hazitofautiana na za ukaguzi, hivyo kudhihirisha kuwa hakuna udanganyifu unaofanywa na kampuni za madini.

Kazi ya ukaguzi wa gharama za uwekezaji, uendeshaji na mazingira zimekamilika katika migodi ya Geita, North Mara, Golden Pride na Bulyanhulu na kwamba, kazi ya uchambuzi serikalini itaanza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo kwenye migodi mingine ya Tulawaka na Buhemba.

Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo kwamba hesabu za kampuni hiyo hazijakaguliwa tangu ipewe kazi na hivi karibuni alinukuliwa akimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kuwa anatetea kitu ambacho hakijui.

Hatua nyingine ambayo imekuwa ikilalamikiwa ni ile ya Waziri wa Fedha, Basil Mramba (wakati huo) kwa niaba ya serikali alisamehe kampuni huo kutotoa kodi ya mapato (withholding tax).

Katika mahojiano maalum na gazeti dada na Mwananchi, The Citizen, Desemba mwaka jana, Rais na Mtendaji Mkuu wa Alex Stewart (Asseyers), Dk Enrique Segura, alikanusha kampuni yake kulipwa kamisheni na Tanzania kwa kutumia mrabaha, bali mapato yatokanayo na dhahabu inayozalishwa na kuuzwa soko la dunia.

Mojawapo ya vifungo vya mkataba huo kinasema," Benki itamlipa mkaguzi ada ya mwezi ya asilimia 1.9 ya mauzo ya dhahabu na serikali kubaki na asilimia 1.1.

Ada inayokadiriwa kutolewa tangu Agosti 2003 kwa kipindi cha miezi 24 ni dola za Marekani 751,267.90. Kiwango ambacho kilikadiriwa mwaka 2003, lakini hakihusu kupanda kwa dhahabu kwenye soko la dunia tangu mwaka juzi.


SOURCE: Mwananchi 26 Machi, 2007
 
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema haitaongeza mkataba wa ukaguzi wa madini na Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) badala yake, itatumia wataalam wake wa ukaguzi.

Akiwasilisha taarifa ya serikali katika Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema wizara itahakikisha inajenga uwezo wa wataalam wake kufanya kazi hiyo.

Hatua nyingine ambayo imekuwa ikilalamikiwa ni ile ya Waziri wa Fedha, Basil Mramba (wakati huo) kwa niaba ya serikali alisamehe kampuni huo kutotoa kodi ya mapato (withholding tax). Mojawapo ya vifungo vya mkataba huo kinasema," Benki itamlipa mkaguzi ada ya mwezi ya asilimia 1.9 ya mauzo ya dhahabu na serikali kubaki na asilimia 1.1.


Umefika wakati wale walioweka saini huu mkataba kuchukuliwa hatua pamoja na BOT kuongeza mkataba ambao ulikuwa ni mbovu. Imekuwaje umekaa kwa muda mrefu namna hii. Hata mtu ambaye hakwenda shule ataona kwamba hapa kuna mchezo ambao umefanyika.


Je vipi Serikali imefikia wapi katika mikataba mingine? Je ni kwa nini makampuni ya kigeni yanaendeleza uchunguzi wa madini wakati hii mikataba yao ya mwanzo haijaangaliwa kwa kina?
 
Alisema kazi ya uhakiki imekuwa ikiendelea vizuri na taarifa za kila mwezi zinaonyesha kuwa takwimu zinazotolewa na kampuni hazitofautiana na za ukaguzi, hivyo kudhihirisha kuwa hakuna udanganyifu unaofanywa na kampuni za madini.
...

Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo kwamba hesabu za kampuni hiyo hazijakaguliwa tangu ipewe kazi na hivi karibuni alinukuliwa akimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kuwa anatetea kitu ambacho hakijui.

1. Je, naibu waziri ana uhakika gani kama wazalishaji na wakaguzi hawashirikiani kupika takwimu? Hiyo haikuwa kesi ya ngedere kumpelekea kima, au kumwachia fisi alinde bucha??

2. Je, haiwezekani Naibu Waziri naye anatetea kitu ambacho hakijui kama Mhe Cheyo alivyomtuhumu Waziri mwenyewe (Karamagi)??
 
Hapa Mzee RO kama unasoma ama kama vijana wako wanasoma , mpe ushauri Mkuu w Nchi n ondoa hisia za sisi kuona kwamba Serikali haijali kw aharufu ya 10% ama siku hizi 20% . Usalama wa Taifa jamani sasa ni wakati kusimamia usalama kweli japokuwa mambo mengi haya yanafanywa kisiasa lakini madhara yake baadaye tutawa laumu nyie .
 
Hapa Mzee RO kama unasoma ama kama vijana wako wanasoma , mpe ushauri Mkuu w Nchi n ondoa hisia za sisi kuona kwamba Serikali haijali kw aharufu ya 10% ama siku hizi 20% . Usalama wa Taifa jamani sasa ni wakati kusimamia usalama kweli japokuwa mambo mengi haya yanafanywa kisiasa lakini madhara yake baadaye tutawa laumu nyie .

Inaniuma sana kumbe hata huo mrahaba wa asilimi 3% hatupati, tunapata 1.1% yaani huyu mwizi mwengine amepewa naye zaidi ya Nchi yaani 1.9%.Wallahi nafwaa,Natamani nichukue Nchi......................Naamini hata kwa uzoefu wangu mdogo wa uongozi, I can do better!
 
Hapa Mzee RO kama unasoma ama kama vijana wako wanasoma , mpe ushauri Mkuu w Nchi n ondoa hisia za sisi kuona kwamba Serikali haijali kw aharufu ya 10% ama siku hizi 20% . Usalama wa Taifa jamani sasa ni wakati kusimamia usalama kweli japokuwa mambo mengi haya yanafanywa kisiasa lakini madhara yake baadaye tutawa laumu nyie .

Hivi sasa hatuna usalama wa Taifa Tulishauzika enzi ya nyerere ,Tuna usalama wa wawekezaji!
 
Naona Wabunge wametuona...

Wabunge wamrudisha Waziri
Shadrack Sagati
HabariLeo; March 28, 2007


KAMATI ya Uwekezaji na Biashara imeikataa taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya ukaguzi wa dhahabu unaofanywa na kampuni ya Alex Stewart hivyo wakaitaka wizara hiyo kuandaa ripoti nyingine.

Kamati hiyo iliyoko chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo, haikuridhika na taarifa hiyo ya Serikali ikielezwa kuwa ilikuwa haijitoshelezi kutokana na kutokuwa na takwimu zozote kuhusiana na ukaguzi huo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo zilieleza kuwa wajumbe hawakuafikiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ambaye taarifa yake ilijikita zaidi juu ya utendaji kazi wa kampuni ya Alex Stewart bila kuweka takwimu yoyote. “Tumeikataa taarifa ya wizara, tumewaomba wakaandae upya halafu watuletee tuweze kuijadili,” alidokeza mbunge mmoja aliyeko katika kamati hiyo.

Kamati hiyo inadai takwimu hizo kuoanishwa na ripoti ya kamati ya hesabu za serikali (PAC) iliyoitoa bungeni ikionyesha kuwa kutokana na kutokuwapo udhibiti migodini, kampuni za migodi ya madini zilitangaza kupata hasara ya Sh trilioni 1.1358 hadi kufikia mwaka 2005.

Mpasha habari alidokeza kuwa iwapo taarifa ya Serikali itakuwa na takwimu ni rahisi kwa kamati hiyo kuhoji mambo mbalimbali na kupata ufafanuzi kutoka kwa maofisa wa wizara ya nishati na madini. Alipoulizwa juu ya hali hiyo, Ngeleja alikiri kamati hiyo kumtaka aandae taarifa nyingine yenye maelezo ya kina tofauti na aliyoiwasilisha juzi.

“Ni kweli hawakuridhika na taarifa yetu; lakini hicho ni kitu cha kawaida, wanataka maelezo zaidi yawepo kwenye taarifa,” alisema Ngeleja wakati akizungumza na gazeti hili kwa simu.

Alikanusha taarifa yake kukataliwa, badala yake alisema kuwa ni mambo ya kawaida kwa wabunge kutaka maelezo zaidi juu ya mambo mbalimbali wanayotaka kuyajadili. “Wanataka taarifa zaidi ambazo naamini awali hawakuziomba katika barua yao,” alisema.

Naibu Waziri alisema kuna uwezekano kutokea mkanganyiko kutokana na barua iliyoandikwa na mwenyekiti wa kamati hiyo kwenda wizarani juu ya kile ambacho kamati ilitaka kutoka kwa wizara hiyo. “Kwa kweli wanataka kile ambacho hawakukiomba awali,” alisema Ngeleja na kufafanua kuwa kamati hiyo haikumpa siku ya mwisho ya kuandaa taarifa hiyo badala yake wamekubaliana iwe kabla ya kikao cha bajeti.

Katika taarifa ya Serikali iliyowasilishwa juzi mbele ya kamati hiyo, Ngeleja alisema hakuna wizi wala udanganyifu unaofanywa na kampuni za nje zinazochimba dhahabu nchini. Alisema taarifa za kampuni hizo hazina udanganyifu wowote kwani zinafanana na za kampuni ya Alex Stewart ambayo imepewa jukumu kufanya ukaguzi wa dhahabu inayozalishwa na kampuni kubwa nchini.

Ngeleja alisema kazi ya uhakiki wa uzalishaji na usafirishaji wa dhahabu imekuwa ikiendelea vizuri na taarifa za kila wakati zinaonyesha kuwa takwimu zinazotolewa na kampuni hazitofautiani na za mkaguzi.
 
Kamati hiyo inadai takwimu hizo kuoanishwa na ripoti ya kamati ya hesabu za serikali (PAC) iliyoitoa bungeni ikionyesha kuwa kutokana na kutokuwapo udhibiti migodini, kampuni za migodi ya madini zilitangaza kupata hasara ya Sh trilioni 1.1358 hadi kufikia mwaka 2005.

Hasara hiyo taifa linabebeshwa kwa kipindi cha miaka 2 (miwili iliyopita). Je kama kulikuwa na hasara hiyo ni kwanini waliendelea kupewa muda na kuendelea kupata hasara. Hata ambaye hayuko jikoni ataona hiyo ni pesa ambayo wajanja fulani wanaichukua. PCB na wengineo wako wapi? Wabunge tunawategemea kuweka mambo sawa.
 
El-Hillal to Invest $15 Million in Machines

The East African (Nairobi)
NEWS
March 27, 2007
Posted to the web March 27, 2007

By Mike Mande, the Eastafrican
Nairobi


EL-Hillal Minerals Ltd, one of Tanzania's leading diamond mining firms, is to invest $15 million in equipment to boost production and for it to perform better on the international market.

Speaking to The EastAfrican in Shinyanga last week, the firm's executive director, Hillal Hamad Hillal, said: "Within the next six months, the firm will acquire another gravel separation plant that can process 100 tonnes of alluvia ore, which will raise the production capacity from 230 to 330 tonnes per hour of diamond-containing two to 25 millimetres of gravel."

El-Hillal started diamond mining in January 2004 at Mwadui near the famed Williamson Mines in Shinyanga, with a projected capacity of 18,000 to 24,000 carats per year.

Last year, the company, Tanzania's second largest diamond miner, produced 23,434 carats worth $4,454,167.
It earned the government some $222,708.
It also exported 2,700 carats.


The new equipment is expected to bring production to 24,000 carats this year. The planned development is part of an upgrading exercise that began in 2005/2006, when the company imported its first modular processing plant.

The plant included a 30 t/h (tonnes per hour) run-of-mine front-end module, a 20-t/h dense medium separation (DMS) module and a containerised x-ray recovery plant.

The machine, into which aluminium ore is fed through the front, has a vibrating feeder, a scrubber and a surge bin.

Material from the machine is pumped to the recovery plant, which is fitted with a concentrates-classifying screen, which feeds the wet x-ray recovery machine via a tube feeder. The recovery plant is totally automated and sorting is done in the fully equipped, containerised unit.


Last year, the company, Tanzania's second largest diamond miner, produced 23,434 carats worth $4,454,167.
It earned the government some $222,708.
Serikali imepata asilimia karibu 5 (5%) na wakati huo huo tutaambiwa kwamba wanaingiza vifaa bila kodi, yaani huu ni wizi wa mchana kweupe ambao umehalalishwa na viongozi wetu. Je serikali ina mpango gani katika hii mikataba ambayo haina faida na wadanganyika?
 
Dua,
naona katika hili la kupata asilimia 5% ya mauzo ya almasi umeniwahi. hata mimi kwa kweli limeniacha hoi. hivi serikali haiwezi kuagiza hiyo mitambo na kufanya shughuli hiyo yenyewe?
 
jokaKuu

I am not in competition. Are you? Is this the reason for you not to accept the truth? Where did this come from?
 
posted by jokaKuu:
Dua,
naona katika hili la kupata asilimia 5% ya mauzo ya almasi umeniwahi. hata mimi kwa kweli limeniacha hoi. hivi serikali haiwezi kuagiza hiyo mitambo na kufanya shughuli hiyo yenyewe?

posted by Dua:
jokaKuu,
I am not in competition. Are you? Is this the reason for you not to accept the truth? Where did this come from?

Dua,
katika suala hili TUKO PAMOJA. niliposoma habari hii, nilitaka nii-post hapa jamboforum, lakini nikakuta wewe umeshaiona na umei-post. sasa ndiyo maana nikasema "umeniwahi."

ukweli hata mimi nimeuona, na nimeukubali. ndiyo maana nikauliza: kwanini serikali isinunue hiyo mitambo na kuchekecha hiyo almasi yenyewe. au hata kwanini isiweke arrangement ya kuwa na 50% shareholder ktk huo mradi?
 
Kama wanashindwa kukusanya ushuru kwenye vivuko wataweza kununua mitambo na kuzalisha? Labda iwe ndege au rada!
 
Kama Kamishna wa Madini anawatetea hadharani, ataweza ku-negotiate nao? Si kwamba asha-jeopardize bargaining power zake? Hayo ndiyo ya kina Mkapa na Yona kusema NBC isipouzwa itakufa...au kina Chenge eti TRC isipokodishwa itakufa...
Ndiyo maana JK kajisemea hatuna uwezo wa kujadiliana kwenye mikataba!
 
Mwanagenzi,
Hawa wote lao ni moja kabisa. Mimi sikuamini kuwa kungekuwa na mabadiliko katika mfumo uliopo hivi sasa wa uchimbaji madini Tanzania. Hofu zangu zikathibitishwa na Indaba 07, ile hotuba aliyoitoa Mheshimiwa mbele ya wachimbaji madini.
 
Rev Kishoka & Jasusi,

VDG, anahadaa wananchi kwa hili, kuna jamaa anaitwa Dr. Charles Tzeba, huyu alikuwa kwanza engineer pale halmashauri ya jiji la DSM, kutokana na ufuska wake wa kuuza viwanja kinyemela huyu jamaa at that time simkumbuki vizuri city engineer wa wakati ule alimtimua kazi baada ya malumbano makubwa serikali ikamsamee na kumhamishia halmashauri ya jiji la Mwanza. Akiwa pale akaanza tena vitimbwi vyake, akanza kuuza viwanja na baadae akauza kiwanja ambacho hakitakiwi kuuzwa na alimuuzia mtanzania mwenye asili ya Kihindi au Kiaarabu, na kwa haraka haraka huyo jamaa akajenga kituo cha mafuta, mahali ambapo haparuhusiwi na kibali alipewa na huyu Dr.Tzeba.

In fact akasimamishwa tena kazi, na wakamfuta hata kwenye bord of engineers, for proffesional misconduct. Waziri Mgufuli alisimama kidete sana kulaani huyu jamaa alivyotumia vibaya madaraka yake na more worse kijikampuni mshenzi cha huyu Dr.Tzeba ndo kikajenga hiyo petrol station, ambayo nafikiri serikali iliivunja baadae. Sasa umefika wakati wa uchaguzi jamaa akajipenyeza kwe mtandao kambi ya Mwanza na kuchangia pesa, baada ya uchaguzi JK kampa jamaa ukuu wa wilaya sasa hivi ni mkuu wa wilaya Sikonge, na akamwambia subiri kwanza watu wasahahu uliyofanya, tutaona wapi nikuweke, sasa kweli JK anapozungumzia ardhi, hebu aanze na huyu kwanza???
 
Nadhani tulishakubaliana kuwa hatuna uongozi ni usanii tu. Tuiombee Tanzania aliyotutakia Mwalimu angalau siku moja tuione.
 
Jasusi,
Kwa kuongezea tu, hii njemba ikiweka matingazi inajisahau na kuonyesha vi sms anavyotumiana na JK, ni aibu tupu huwezi kuamini lakini ndo JK tunaempenda mwenye sura ya walidi.
 
Muungwana aache Utapeli hapa!Ampokonye Ardhi EL ambae amechukua eneo kubwa Handeni kwa ajili ya Ranchi ya Mifugo yake.Kuna familia kama 10 zilihamishwa kwenye eneo hilo ili kumpisha Mkubwa afuge Ng'ombe hapo.Kuna Ng'ombe wengi wafanyakazi na Mabwana Mifugo (waajiriwa wa serikali) wanaosimamia Ranchi hiyo .Dr Abdallah Kigoda (Mbunge) analielewa hili lakini naona amelifumbia macho.
Sasa kama anataka Haki na Ukweli awapokonye hawa wenye nazo kwanza,ambao wanahodhi Ardhi kila mahali kutoka Hanang,Mto wa Mbu,Monduli na sasa Handeni.
 
Back
Top Bottom