Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Dua anashauri kwamba serikali ingenunua dhahabu yote na tanzanite yote kwa kipindi cha miaka 3, ili tujue kiasi halisi. Kwa mwaka, Tanzania inauza nje dhahabu ya $700 milioni na tanzanite ya $400 milioni. Serikali yetu haina uwezo wa kununua madini ya $1,100 milioni kwa mwaka na ikabaki na fedha za matumizi muhimu. Kwa miaka 3, tungehitaji $3,300 milioni. Hii ni zaidi ya fedha zote za kigeni tulizo nazo.
Namshukuru Mwagenzi kwa upambanuzi wake wa kina kuhusu vigezo vinavyohatarisha amani ya nchi. Kwa maoni yangu, wizi wa kura na rushwa katika chaguzi zetu ni kigezo kinachoweza kuleta uchafuzi Tanzania mapema kuliko vigezo vingine vyote. A time will come when the opposition parties will choose to fight fire with fire. Kwa sasa, CCM inatumia nguvu za Jeshi, Usalama wa Taifa na Polisi kuhakikisha "wanashinda" karibu kila uchaguzi.
Jasusi,
Laiti tungekuwa na bunge lenye demokrasia ya kweli. Ungepita mswada wa kutaka kusiweko na kampuni ya nje yenye zaidi ya 40% ya hisa kwenye kuchimba madini. Naamini wabunge karibu wote wangeunga mkono mswada kama huo. Kinachokwamisha ni kukosekana demokrasia.
Tuko katika kipindi cha unyonyaji wa kutisha. Ni unyonyaji unaofanywa na makampuni ya madini, kwa makubaliano na serikali yetu. Kwa vile makubaliano yenyewe si ya haki, hairuhusiwi wananchi kuyajua. Hata wawakilishi wa wananchi, yaani wabunge, hawana haki kuyafahamu hayo makubaliano.
Historia inaonyesha kwamba makundi yanoyoweza kuokoa nchi iliyo katika lindi la ukandamizaji kama wa kwetu, ni wafanyakazi na wanafunzi. Laiti wanafunzi wetu wangetambua kwamba maisha ni zaidi ya mikopo yao! Inaelekea wafanyakazi wa Tanzania hawajui kwamba hali yao ya umasikini wa kutisha sio matakwa ya Mungu. Ni hali inayotokana na unyonyaji wa ajabu, na uongozi mbaya unaosimamiwa na CCM.