Miili ya wanajeshi wetu wa JWTZ jinsi ilivyopokelewa na ndugu, viongozi na wananchi

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264

Wanajeshi wa JWTZ wakibeba jeneza lenye mmoja wa askari wenzao saba waliouawa kwa shambulio la ghafla wakiwa katika Jeshi la Ulinzi wa Amani la Umoja wa Mataifa mjini Darfur, jumamosi iliyopita. Miili hiyo iliwasili leo saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga cha JWTZ.

Baadhi ya viongozi wakiongozwa na Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal wakishuhudia miili ya wanajeshi saba wa JWTZ waliouawa na waasi mjini Darfur, miili hiyo ilipofikishwa leo Uwanja wa Ndeje wa Kikosi cha anga cha JWTZ jijini Dar es Salaam.








Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Job Masima wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga cha JWTZ, kabla ya miili kuwasili. Wengine kulia ni Ridhiwani Jakaya Kikwete, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba. ambao walihudhuria mapokezi ya miili hiyo.

Makamu wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Mstaafu, Abdurhaman Kinana, baada ya kuwasili kwenye mapokezi ya miili ya wanajeshi hao. Katikati ni Waziri wa Ulinzi Shamshi Vuai Nahodha
Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauyebaada ya kuwasili kwenye Mapokezi ya miili ya askari wa JWTZ waliouawa mjini Darfur



Makamu wa Rais, Dk. Muhamed Gharib Bilal akiagana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, baada ya mapokezi ya wanajeshi wa JWTZ waliouawa Darfur kukamilika
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo na Adam Sudi Wakuduwaa wakati miili ya askari hao ilipokuwa ikishushwa kwenye ndege baada ya kuwasili leo jioni Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha anga.
Ndugu wa mmoja wa askari wa JWTZ waliopoteza maisha kwa kushambuliwa na waasi mjini Darfur akiwa mwenye majozi wakati wa mapokezi ya askari hao.
Msafara wa malori saba yaliyobeba miili ya askari saba wa JWTZ waliouwa Darfur uliongozwa na polisi wakati wa kutoka Uwanja wa Ndege, Kikosi cha Anga baada ya kupokewa leo jioni. Picha zote na the Nkoromo Blog
 
Binadamu wote tunapita hapa duniani.

Katika kitabu cha Mwanzo 3:19 kinasema, kwa maana wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi.
( For you are dust, and to dust you will return )
 
Wasiwasi wangu ni kama hizo familia watalipwa fedha zao zilizotolewa na UN, kwa ufisadi wa Serikali kandamizi ya CCM, Sijui aisee, labda UN wawape hizo familia pesa zao moja kwa moja, lakini zikipitia mikononi mwa hayo Majambazi itakula kwao. Badala ya milioni 112 kila familia wanaweza kupewa hata milioni moja moja au wakazungushwa hadi wakate tamaa. Hakika CCM ni laana kwa nchi hii.
 


macho ya uzee haya, huyu mwenye shati nyeupe ni kiongozi gani vile?
Nimemuuliza jirani yangu hapa ananiambia eti huyo ni yule mfanya biashara maarufu wa bidhaa ambayo kule China ukikamatwa nayo unanyongwa. Hata sijamuelewa. Nisaidieni na mie.
 


macho ya uzee haya, huyu mwenye shati nyeupe ni kiongozi gani vile?


Kichefu chefu sana nchi hii,sasa sijui hapo kasimama yeye kama nani...
Jeshi hili wanalidhalilisha sana kwa sasa,limekuwa linwatumikia wanasiasa hivi,inachukiza sana
 
Nimemuuliza jirani yangu hapa ananiambia eti huyo ni yule mfanya biashara maarufu wa bidhaa ambayo kule China ukikamatwa nayo unanyongwa. Hata sijamuelewa. Nisaidieni na mie.

biashara yake inamwingizia mamilioni......

au anamuwakilisha baba yake hapo.....
 


macho ya uzee haya, huyu mwenye shati nyeupe ni kiongozi gani vile?

FUSO umenichekesha sana, you just made my day! Ah hii nchi hii tamu sana! Nimejaribu kuangalia itifaki hapo haisomeki au ametumwa kumwakilisha mtu!
 
Kinana na nape wapo hapo kama kina nani?
Je na mwenezi wa updp angekuwepo hapo protocol ingemtambua?
 
Back
Top Bottom