Hii ndiyo tofauti ya JWTZ na Polisi wetu

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Muda mfupi uliopita nilikuwa kwenye daladala ya kutoka Gongolamboto kuelekea mjini.

Kwa sasa asilimia kubwa ya njia hiyo huwezi kukosa foleni Kwa sababu ya ujenzi unaoendelea.

Na Kwa sababu ya ujenzi huo, tulipofika katika kilima Cha Ukonga, magari yalisimama Kwa Muda mrefu kutoka na msingamano uliopo hapo, huku eneo kubwa la njia likiwa katika matengenezo.

Katika foleni hiyo mara walitokea askari wa Jeshi la wananchi,mmoja akiwa ameficha sura yake na na mwingine akiwa ameacha sura wazi.

Maaskari Hawa wakawa wanawaelekeza madereva juu ya umuhimu wa watu wote kutumia njia hapa ninanukuu kauli ya mmoja wao kwenda Kwa dereva wa daladala.

"Oya jombaa hii njia si inapaswa tutumie wote sasa kwanini ninyi mmebana kote kote hembu tafuteni nafasi nzuri kwenu na wengine wapite"

Dereva alimuelezea sababu ya kuwa upande ule na askari wa JWTZ akaridhika na kuondoka.

Dakika Tano baadae alikuja askari wa Jeshi la Polisi ambaye alishuka katika karandinga lao akiwa amevaa sare Jungle na kumfuata dereva wa daladala.

Neno la kwanza aliloanza nae ni vitisho dhidi ya dereva na hapa ninamnukuu.

"We jamaa unajua Mimi naweza nikakunyanyua nikakutupia Kule na usinifanye chochote mpumbavu wewe ondoa gari hapa"

Hata dereva alipomuelekeza kuwa ameambiwa na askari mwenzie anayeongoza magari huko alipotoka kuwa apite Kule yule Mzee wa Jungle hakuelewa na aliendeleza vitisho na matusi

Nanukuu "Askari ndiyo Nini wewe K.m.nitakuwasha Mimi"Kisha akaondoka.

Baada ya matukio hayo binafsi nimeingia katika tafakari kuu juu ya majeshi haya mawili na wajibu wao Kwa wananchi.
 
Umewasikia watu wawili tofauti mmoja ni mtumishi wa watu na mwingine ni mtumishi wa yeye mwenyewe.
 
Hii tofauti iko kwenye fikra zako na siyo uhalisia. Polisi Wana madhaifu mengi lakini kuwalihganisha na JW linapokuja suala la kuhudumia Jamii ni kujitoa fahamu kama ulivyofanya wewe. Huwajui JW kaa hivyo hivyo na sifa zako jumuishi.
 
Mkuu, kwani wewe haujiulizi kwanini hata wakuu wa nchi hua hawavai uniforms za majeshi mengine kama pilisi au magereza na uhamiaji...??? Badala yake wanavaaga mabaka tu..😊
 
Mkuu hiyo tofauti yako watu wa Kawe hawawezi kuielewa kwa namna walivyotembezewa kichapo na hao unaowaona wastaarabu kwa mujibu wa nyuzi nyingi za takribani wiki tatu zilizopita
 
Back
Top Bottom