Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,177
Source: Inner City Press: Investigative Reporting from the United Nations, U.N. Officials Reluctant To Disclose Financial Relationships And Assets, Putting Spotlight On Ethics | Fox News, maoni binafsi na vyanzo visivyo rasmi.
Jitihada kubwa zilifanywa na Migiro binafsi na pia kuwatumia African Group of Nations kujaribu kuhakikisha Ban Ki Moon anabadilisha uamuzi wake wa kumtosa UN, lakini hilo halikusaidia kitu. Ban alishikilia uamuzi wake wa kuunda aliyoita 'timu ya kazi'. Sababu hazijawekwa wazi, lakini kama alivyobainisha Ban kuwa anataka ufanisi, ni wazi kuwa kulikuwa hakuna ufanisi.
Tayari ameshamteua mwanadiplomasia Jan Eliasson, raia wa Sweden, kuchukua nafasi hiyo ya Migiro. Migiro kwa mujibu wa mkataba wake, ataondoka rasmi UN mwezi Jun, 2012.
Hapa nyumbani, Tanzania kuna habari kutoka kwa insiders wa ikulu kuwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yanasubiri kurudi kwa Migiro.
Maisha ya Watanzania yameendelea kuwekwa rehani kwa sababu ya mtu mmoja. Kuna matatizo makubwa Wizara ya Afya, Wizara ya Nishati na Madini nk, Mawaziri wengi hawapo ofisini kwa sababu za kiafya na wengine wameonyesha kushindwa, na baadhi wana kashfa. Lakini kwa sababu ya mtu mmoja, hakuna mabadiliko ya cabinet hadi atakapokamilisha mkataba wake UN na kurudi TZ ili naye apangiwe Wizara katika mabadiliko hayo.
Matatizo mengi ambayo nchi inapitia leo yanasababishwa na malengo ya 2015.