Mifugo Hifadhi ya Ruaha ni balaa

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Ni kama wafugaji wa Tanzania hawaelewi umuhimu wa maeneo yanayohifadhiwa na kilindwa kwa maslahi ya Taifa linapokuka suala la wao kuwapatia malisho mifugo yao.

Ni kama pia idara za serikali zinazohusika na usimamizi wa Mifugo zimeshindwa kudhibiti ama kuratibu namna bora wananchi wananweza wakafuga mifugo yao bila kuathiri maeneo muhimu yanayohihifadhiwa nchini.

Eneo la Hifadhi ya Ruaha sio tu muhimu kwa utalii bali ni chanzo kikuu cha maji yanayokwenda bwawa la Mtera linalozalisha megawatts 80 za umeme ambapo kwa sababu za uharibifu wa vyanzo vya mito hiyo ikiwemo eneo Oevu la Ihefu bwawa la Mtera limekauka na kusababisha upungufu wa umeme.

Ni muhimu kujua pia Hifadhi ya Ruaha ndio maji yake yanakwenda bwawa la Kidatu linalozalisha megawatts 204 za umeme na kisha maji hayo hayo kuunganana na maji kutoka mito ya Kilombero kujaza bwawa la Nyerere linalotarajiwa kuzalisha megawatts 20115.

Kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa kudhibiti uhalifu na uvamizi wa maeneo oevu, maeneo yanayohifhadhiwa, vyanzo vya maji n. k haditihi ya kuisha kwa Mgao wa Umeme itaendelea kuwepo milele na milele.

Kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa kudhibiti uhalifu na uvamizi wa maeneo oevu, yanayohihifadhiwa, vyanzo vya maji n.k. Hadithu ya Mgao wa Maji na kukosekana kwa maji Safi na Salama haitakaa iishe nchini.

IMG-20231120-WA0541.jpg
IMG-20231120-WA0540.jpg
IMG-20231120-WA0544.jpg

Sent from my Infinix X6716B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mimi lawama zangu nazielekeza kwa government maana imeshindwa kuleta sera ambayo itambana mfugaji ili awe na kundi ambalo litahimiliwa na maeneo wanayomiliki,migogoro mingi ya wafugaji na wakulima chanzo ni wafugaji,watu wanauliwa na wafugaji kisa maeneo ya malisho.

Mimi nawachukia sana wafugaji kwani hawazingatii wakulima kabisa , wao wanachojali ni mifugo yao ishibe tu,hapa kwangu ninajirani kila mara tunagombana kisa mifugo kuingia ndani ya eneo langu kisa tu eneo langu ni kubwa na kuna nyasi,shida ninayo ipata ni miti kulishwa na ngombe.

Nashauri serikali iwabane hawa watu ni janga kWa taifa,kila mfugaji awe na eneo la malisho ambalo litatosha kuhifadhi mifugo wake na iwe marufuku kuchungungia kwa eneo la mwenzake bila kibari.

Serikali iache kuogopa kupoteza kura za wafugaji huku wakiharibu mazingira na kusababisha migogoro ambayo olinapelekea mauaji
 
Hili suala limeshaingiliwa na wanasiasa. Mamlaka husika zikifuata sheria tayari wanasiasa wanaingilia
Vyombo husika viachwe vifanye kazi yake
Kweli kabisa, taasis zikianza kutekeleza sheria kelele za wanasiasa zitaanza
 
Mkuu mimi lawama zangu nazielekeza kwa government maana imeshindwa kuleta sera ambayo itambana mfugaji ili awe na kundi ambalo litahimiliwa na maeneo wanayomiliki,migogoro mingi ya wafugaji na wakulima chanzo ni wafugaji,watu wanauliwa na wafugaji kisa maeneo ya malisho.

Mimi nawachukia sana wafugaji kwani hawazingatii wakulima kabisa , wao wanachojali ni mifugo yao ishibe tu,hapa kwangu ninajirani kila mara tunagombana kisa mifugo kuingia ndani ya eneo langu kisa tu eneo langu ni kubwa na kuna nyasi,shida ninayo ipata ni miti kulishwa na ngombe.

Nashauri serikali iwabane hawa watu ni janga kWa taifa,kila mfugaji awe na eneo la malisho ambalo litatosha kuhifadhi mifugo wake na iwe marufuku kuchungungia kwa eneo la mwenzake bila kibari.

Serikali iache kuogopa kupoteza kura za wafugaji huku wakiharibu mazingira na kusababisha migogoro ambayo olinapelekea mauaji
Nimekuelewa vizuri Sana
 
Oneni

Hatuelewani

Hakuna ulazima wa kupunguza idadi ya mifugo.

Ni kuweka tu utaratibu wa misimu ya kupitisha mifugo.

Kiukweli mifugo katika hifadhi ni moja ya njia borrrrra kabisa ya kuhifadhi hifadhi hizo🤔

Sijachanganya, nnarudia tena kwa lugha nyingine MIFUGO HUSAIDIA KUBORESHA MAZINGIRA YA MAENEO INAPOCHUNGIWA HUKO MISITUNI na hii ndiyo sayansi.

Hata mbunge wa Geita alipoomba hao wahifadhi waambatane na wachungaji ili wakawaoneshe uharibifu unatokeaje huoni walishindwa? Sayansi ipo upande wa wafugaji. Tena wafugaji wa makundi makuuuuuuuubwa ya ng'ombe.

Msikaririshwe mazingira, mazingira
 
Wanyama wenyewe ndo hao ninaosikia viongozi wachache ndio wanaowamiliki, wakitaka kuingiza ndege kwa makubaliano na matajiri wa huko ughaibuni wanawauza na pesa wanabeba wao?

Hapo lazima tukubaliane kwanza na kuheshimiana, mifugo ni ya watanzania, wanyama na mapori pia,

Viongozi wawe wazalendo kwenye rasilimali zetu,
 
Mkuu mimi lawama zangu nazielekeza kwa government maana imeshindwa kuleta sera ambayo itambana mfugaji ili awe na kundi ambalo litahimiliwa na maeneo wanayomiliki,migogoro mingi ya wafugaji na wakulima chanzo ni wafugaji,watu wanauliwa na wafugaji kisa maeneo ya malisho.

Mimi nawachukia sana wafugaji kwani hawazingatii wakulima kabisa , wao wanachojali ni mifugo yao ishibe tu,hapa kwangu ninajirani kila mara tunagombana kisa mifugo kuingia ndani ya eneo langu kisa tu eneo langu ni kubwa na kuna nyasi,shida ninayo ipata ni miti kulishwa na ngombe.

Nashauri serikali iwabane hawa watu ni janga kWa taifa,kila mfugaji awe na eneo la malisho ambalo litatosha kuhifadhi mifugo wake na iwe marufuku kuchungungia kwa eneo la mwenzake bila kibari.

Serikali iache kuogopa kupoteza kura za wafugaji huku wakiharibu mazingira na kusababisha migogoro ambayo olinapelekea mauaji
Wala! Serikali haiogopi kukosa kura za wafugaji, wanachoogopa serikali ni nyama kupanda bei.

Wakisema waanzishe operation ya kuwadhibiti wafugaji nchi nzima bei ya nyama itafika 25000 na ichi ndicho serikali wanachoogopa serikali . Ndyo maana linapokuja suala la wafugaji approach ya serikali huwa inakuwa inafanywa kwa umakini sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kuhamahama ndo akili yenyewe, tena kubwa. Nenda kasome
Ufugaji wa asili ndo unafanya wengi walau wanakula nyama, bila wasukuma kuhamia lindi na mtwara, kwa mfano, maeneo hayo nyama ilionekana kama anasa.

Hivyo mkitaka kuhamasisha ufugaji wa kisasa na wa kibiashara wengi wa watu nyama wataishia kuisikia harufu tu, maana hawatamudu kununua.
 
Oneni

Hatuelewani

Hakuna ulazima wa kupunguza idadi ya mifugo.

Ni kuweka tu utaratibu wa misimu ya kupitisha mifugo.

Kiukweli mifugo katika hifadhi ni moja ya njia borrrrra kabisa ya kuhifadhi hifadhi hizo🤔

Sijachanganya, nnarudia tena kwa lugha nyingine MIFUGO HUSAIDIA KUBORESHA MAZINGIRA YA MAENEO INAPOCHUNHIWA HUKO MISITUNI na hii ndiyo sayansi.

Hata mbunge wa Geita alipoomba hao wahifadhi waambatane na wachungaji ili wakawaoneshe uharibifu unatokeaje huoni waloshindwa? Sayansi ipo upande wa wafugaji. Tena wafugaji wa makundi makuuuuuuuubwa ya ng'ombe.

Msikaririshwe mazingira, mazingira
Hivi kweli mpaka hapo ulipofikia huoni vile Mifugo inavyoaribu hifadhi..?

Bila Shaka wewe ni miongoni mwa janga la wadugaji
 
Wala! Serikali haiogopi kukosa kura za wafugaji, wanachoogopa serikali ni nyama kupanda bei.

Wakisema waanzishe operation ya kuwadhibiti wafugaji nchi nzima bei ya nyama itafika 25000 na ichi ndicho serikali wanachoogopa serikali . Ndyo maana linapokuja suala la wafugaji approach ya serikali huwa inakuwa inafanywa kwa umakini sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Kwahiyo mkuu tuendelee kuharibu mazingira na watu waendelee kuuliwa na wafugaji kisa ni kuogopa bei ya nyama kupanda!? ,Sidhani kama ni busara juu ya hili,kwani kwa nchi za weNzetu wao wanafanyeje,je kuna huu ufugaji wa kiholela kama huku kwetu!?
 
Back
Top Bottom