Microsoft kuleta intaneti kwa mamilioni ya Watu Afrika kupitia satelaiti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,504
9,283
Kampuni ya Microsoft imetangaza leo mipango ya kuleta huduma za intaneti kupitia satelaiti kwa watu milioni 10, nusu yao wakiwa barani Afrika, kama sehemu ya juhudi za kuziba pengo la kidijitali na ulimwengu unaoendelea.

Katika mkutano na viongozi wa Afrika mjini Washington ukiongozwa na Rais Joe Biden, kampuni hiyo kubwa ya teknolojia imesema itaanzisha mara moja mradi huo wa satelaiti kwa kipaumbele cha kuleta intaneti kwa mara ya kwanza katika maeneo ya Misri, Senegal na Angola.

Rais wa Microsoft Brad Smith amesema kampuni hiyo imevutiwa na wahandisi wake wa Nairobi na Lagos.

Smith amesema barani Afrika hakuna uhaba wa vipaji, lakini kuna uhaba mkubwa wa fursa. Viongozi 49 wa Afrika wanahudhuria mkutano huo wa kilele wa siku tatu ambao ulianza hapo jana.

Times of Malta
 
Itakufa kifo cha mende. microsoft sijaanza kumsikia leo kujifanya anajua na mwisho wa siku project zinafeli.

kwenye smartphone na mawasiliano hapa bora kuacha wengine tu
 
Itakufa kifo cha mende. microsoft sijaanza kumsikia leo kujifanya anajua na mwisho wa siku project zinafeli.

kwenye smartphone na mawasiliano hapa bora kuacha wengine tu

hakuna jambo lilifanikiwa kwa jaribio moja.
 
Itakufa kifo cha mende. microsoft sijaanza kumsikia leo kujifanya anajua na mwisho wa siku project zinafeli.

kwenye smartphone na mawasiliano hapa bora kuacha wengine tu
Yet, bado kwenye ulimwengu wa kijiditali na intaneti yuko vizuri. Soko la simu na software hawa jamaa wa android na ios walikuwa miles ahead, ilikuwa ngumu kuwapiku
 
Kampuni ya Microsoft imetangaza leo mipango ya kuleta huduma za intaneti kupitia satelaiti kwa watu milioni 10, nusu yao wakiwa barani Afrika, kama sehemu ya juhudi za kuziba pengo la kidijitali na ulimwengu unaoendelea...
Watu milioni kumi ni wachache sana. Wasituzuge na ahadi ambazo hawatazitekeleza.
 
Ngoja tuone labda ataweza kuja kumshusha bei Elon manake setting up yake ya internet kutoka Kwa masatelite inacost $ 500 madishi na bado kila mwezi Kama $100 huko inakopatikana sasa
 
Microsoft si kampuni ndogo kama unavyodhania haswa ikija katika maswala ya digital. Computer karibu zote Africa zinatumia microsoft windows.

labda ujaelewa !. dell iliacha kushugulisha na mawasiliano ya simu sababu kama hizo
 
kuna watu wanafikiria jambo jepesi sana. kuna kampuni na uwezo wao wote wakutengeneza ndege na meli ila wanatemgea rolls royce watengenezewe injini.

Hata hiyo starx ya elon bado inachangamoto zake kushindana na makampuni makubwa ya setelite.

kama unabisha hiyo microsoft mbona kashindwa kujikita kwenye mifumo kama ORACLE,CISCO na n.k sababu sio part yake abaki tu na kuendeleza OS na mifumo ya microsoft
 
Sawa mkuu, wamekusikia...Wataacha haraka iwezekanavyo
 
Itakufa kifo cha mende. microsoft sijaanza kumsikia leo kujifanya anajua na mwisho wa siku project zinafeli.

kwenye smartphone na mawasiliano hapa bora kuacha wengine tu
And yet anakua kuliko hao wanaojifanya wanajua? Sasa hivi Azure inatumika everywhere na ni Cloud communication.

Angalia Valuation ya Msft angalia na pato la Azure,
 
kuna watu wanafikiria jambo jepesi sana. kuna kampuni na uwezo wao wote wakutengeneza ndege na meli ila wanatemgea rolls royce watengenezewe injini.

Hata hiyo starx ya elon bado inachangamoto zake kushindana na makampuni makubwa ya setelite.

kama unabisha hiyo microsoft mbona kashindwa kujikita kwenye mifumo kama ORACLE,CISCO na n.k sababu sio part yake abaki tu na kuendeleza OS na mifumo ya microsoft
We jamaa hata huijui Microsoft bora unyamaze, windows inachangia asilimia 12 tu ya Microsoft, hii kampuni ina mambo Kibao hardware za Gaming kama Xbox, inatengeneza Games zake kibao kama Minecraft, Halo, Age of empire etc,

Pia Oracle ni kampuni ya 3 duniani kwa software, Nyuma ya IBM na Microsoft, sasa Microsoft kampuni ya kwanza Duniani kwa Software ila imeshindwa kujikita na inapitwa na kampuni ya 3?

Na Star X hana Changamoto na Satelite nyengine, sababu wapo wachache kwenye low orbit satelite, usimix low orbit na traditional satelite,

Star x competitors wake ni Fiber na Mobile internet kama 5G.
 
Kama Ulimaanisha Microsoft huyo Bill gate aliondoka Microsoft wengi hawajazaliwa humu, na alishauza na hisa, Bill gate anakumbukwa tu kama mwanzilishi ila sio mmiliki wala mfanyakazi alishajitoa.
Kaiza hisa zote unamaanisha
 
Kaiza hisa zote unamaanisha
Sio zote ila hisa zake zilizobakia ni kidogo tunaongelea kama 1% hivyo hayupo kwenye Bodi wala wamiliki wakubwa hana decision yoyote kuhusu Microsoft. Gate siku hizi hela nyingi anazo kama Cash hana time na Utajiri.
 
Back
Top Bottom