Miaka 50 ya Uhuru: Wimbo wakataliwa kupigwa redioni

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, kuna mtunzi ametunga wimbo mmoja lakini umekataliwa kupigwa redioni. Sijui hatima ya aliyetunga huu wimbo lakini umebeba maudhui makubwa tuu hasa katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru na ni bora watu wengi wakausikiliza huu wimbo. Sikiliza au jipakulie wimbo wenyewe hapo chini. Nawatakia wote miaka 50 ya uhuru.

[JFMP3]View attachment Miaka 50 ya Uhuru -King Pao.mp3[/JFMP3]
 
Wengine masikio yeshatangulia mbele ya haki hasa linapokuja hili la 'wanaofoka foka'

Hebu tuandikieni mistari ilivyo
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Aisee!hivi hakuna dj hata moja tu akaupiga huu wimbo jamani?ukwel mtupu huyu jamaa kaimba!laiti wangepata ujasiri wa kuupiga leo!!ungepeleka ujumbe mzito!ngoja niupige na spika zangu kubwa hapa nje ya duka langu walau ujumbe uwafikie wananchi!radion wasipoupiga mitaan tutaupiga.
 
anastahili pongezi jamaa, angalau kajitoa na kupinga hizi sherehe, tatizo ni kwamba kachelewa kuitoa hii kitu. angeitoa mapema. halafu kwako EMT, ukimwona tena huyu jamaa mwambie aurekebishe wimbo wake sababu kaimba kwa kasi sana hivyo hata kama alikuwa naujumbe mzuri mwishoni unashindwa kueleweka. apunguze spidi.
 
Tumtafute Ridhiwani akaongee na mshua hampe na huu ujumbe...
 
Tumtafute Ridhiwani akaongee na mshua hampe na huu ujumbe...

Muacheni Jakaya mambo yamemzidi kimo , huku kuna sakata la Jairo na Luhanjo; huku mambo ya katiba hayaelewi ingawa ametia saini muswada; huku anasusia kusaini posho za wabunge na huku Lowassa anamchongea kuwa yeye ndiyo mhusika mkuu wa Richamond!! Hizi kelele za milango lazima zitamkosesha mwenye nyumba usingizi pengine awe maiti!!
 
Wimbo ni mzuri! Nilishasema maendeleo yanakuja kwa kuelezana ukweli na kama hatutaki ukweli kwa lengo la kuendelee kuwa maskini lazima tuajiri watangazaji walamba nyayo ambao wanashadidia uongo. Tuko pamoja, tutafika tu kwani harufu ya mavi hazuiliwi kwa kufunikwa na tenga.
 
Wimbo ni mzuri! Nilishasema maendeleo yanakuja kwa kuelezana ukweli na kama hatutaki ukweli kwa lengo la kuendelee kuwa maskini lazima tuajiri watangazaji walamba nyayo ambao wanashadidia uongo. Tuko pamoja, tutafika tu kwani harufu ya mavi hazuiliwi kwa kufunikwa na tenga.




jamani naupendaga huu wimbo
mwenye nao nauomba pls
 
Back
Top Bottom