GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,955
- 109,766
Kwanza nianze kwa kuwapeni wale ' Wanamapinduzi ' wenzangu wote kwa ' Msiba ' mkubwa sana uliotokea muda si mrefu wa ' kuondokewa ' na Rafiki yetu mkubwa sana Tanzania aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro.
Hakuna asiyejua kuwa urafiki wetu Tanzania na Cuba ni wa ' Kihistoria ' kabisa hasa ukizingatia kuwa ' uliratibiwa ' vizuri mno na Kiongozi huyo wa Kihistoria wa Cuba na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hizi nchi mbili zimefaidika mno kwa ushirikiano wa Kisiasa, Kilimo, Biashara bila kusahau Kiulinzi na Kiusalama.
Ndipo kwa Heshima na taadhima kabisa huku nikijua kuwa Mheshimiwa Rais wetu ana ratiba ngumu kabisa na majukumu mengi ya kututumikia sisi Watanzania na mara nyingi amekuwa akituma wawakilishi wako katika mambo kadhaa huko nje ya nchi hasa Makamu wake Mama yetu Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim ila kwa huu ' msiba ' mzito na mkubwa wa Kidunia tunamwomba sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ' akatuwakilishe ' moja kwa moja Watanzania na ' tutafarijika ' sana.
Naomba ' uzi ' huu usieleweke vibaya labda kama nataka kumpangia Rais nini cha kufanya kwani kiukweli hata uwezo huo sina ila ' nimeguswa ' na huu ' msiba ' mzito kabisa kutokana na Historia zetu hizi nchi mbili na Urafiki wetu wa shida na raha na Watu wa Cuba.
Poleni sana Watanzania mlioguswa kama Mimi na huu ' msiba ' na pia pole zao kubwa Wananchi wa Cuba kwa kuondokewa na Revolutionary Icon na True Hero Mzee Fidel Castro na ama hakika ametuachia kumbukumbu na legacies nyingi mno sisi Wanamapinduzi ambayo bila shaka inabidi sasa tupite mule mule ambapo ' Marehemu ' alipita.
Nitoe pia pole zangu kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) kwani najua kuwa tulikuwa na ' ushirikiano ' mkubwa na mzuri mno na Watu wa Cuba hasa ukizingatia kuwa ' Marehemu ' alilipenda na kuliheshimu mno Jeshi letu la Tanzania na hakuna ubishi kuwa asilimia fulani za ' uzuri ' na ' ufanisi ' wa ' kiutendaji ' wa Jeshi letu pendwa na zuri la JWTZ pia zilichangiwa na Millitary Philosophies za Mzee Fidel Castro.
Nimtakie tu maziko mema Mzee Castro na may his soul rest in peace. Jembe la ukweli na la Kimapinduzi limeondoka na ' ubora ' na ' utamu ' wake.