mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 873
Katika sakata la Jairo, gazeti la mwanahalisi lilituonyesha orodha ya watu waliolipwa posho ya Tshs.280,000 kwa siku kwa Mheshimiwa Pinda, Spika wa Bunge, Mama Anna Makinda. Watu walianza kuhoji, uhalali wa waheshimiwa hawa kukubali posho kubwa kiasi hicho kwa msaa machache walizo kaa katika semina ya akina Jairo. Kosa la Pinda, lilikuwa dogo sana kwa sababu yeye aliletewa na hakuwa na bahati ya kuhoji sababu na uhalali wa kiasi hicho cha fedha. Pinda angeomba msamaha nadhani Watanzania wange msamehe tu.
Katika kujiondoa katika aibu, na kwa kukosa uzalendo na uungwana ameamua kuhalalisha kwa kushauriana na Mheshimiwa Spika, wapandishe posho ya kikao iwe Tshs.200,000 kwa siku na posho ya kujikimu Tshs. 80,000. Jumla yake ni shilingi 280,000, sawa na kiasi walichokipokea siku hiyo. Gharama kwa watanzania itakuwa kubwa kwa nia tu ya kuficha dhambi ndogo ya kupokea posho bila kuhoji.
Tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda, sio malaika, hata yeye anajua hilo, inakuaje atuingize hasara kubwa kiasi hiki na kwa miaka mingi ijayo. Mnaweza kumsamehe, ila mimi basi.