Mheshimiwa Pinda amewasaliti Watanzania na kwa kosa hili hasameheki

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
1,571
873
Katika sakata la Jairo, gazeti la mwanahalisi lilituonyesha orodha ya watu waliolipwa posho ya Tshs.280,000 kwa siku kwa Mheshimiwa Pinda, Spika wa Bunge, Mama Anna Makinda. Watu walianza kuhoji, uhalali wa waheshimiwa hawa kukubali posho kubwa kiasi hicho kwa msaa machache walizo kaa katika semina ya akina Jairo. Kosa la Pinda, lilikuwa dogo sana kwa sababu yeye aliletewa na hakuwa na bahati ya kuhoji sababu na uhalali wa kiasi hicho cha fedha. Pinda angeomba msamaha nadhani Watanzania wange msamehe tu.

Katika kujiondoa katika aibu, na kwa kukosa uzalendo na uungwana ameamua kuhalalisha kwa kushauriana na Mheshimiwa Spika, wapandishe posho ya kikao iwe Tshs.200,000 kwa siku na posho ya kujikimu Tshs. 80,000. Jumla yake ni shilingi 280,000, sawa na kiasi walichokipokea siku hiyo. Gharama kwa watanzania itakuwa kubwa kwa nia tu ya kuficha dhambi ndogo ya kupokea posho bila kuhoji.

Tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda, sio malaika, hata yeye anajua hilo, inakuaje atuingize hasara kubwa kiasi hiki na kwa miaka mingi ijayo. Mnaweza kumsamehe, ila mimi basi.
 
Duuuu, kwahiyo unataka kutuambia hiki ndiyo kigezo walichotumia kujiongezea posho. "Hivi Pinda bado ni mtendaji serikali hii?"
 
aaagh huyo simpendi tangu ameuza ardhi huko kwao kwa wazungu ,,,hebu fikiria wafugaji na wakulima wanauwana kwa sababu ya arthi ingekuwa mimi kipao mbele ningewapa watz kwanza ,,,chakula tunacho kingi tu tumeona tbc wakulima wanalalamika wanaomba kama serikali imeshindwa kununua wakayauze nje ya nchi
 
Hawa ndo marais tunaowategemea,,,anajifanya kuwaonea watu huruma mpaka analia ....kumbe ilikuwa danganya toto......arudishe fedha zetu mara moja
 
hii nchi haina rais wala waziri mkuu......ina watu wanao watusi tu watanzania......
 
kama ndo hivyo basi joni shibuda (mubunge wa maswa) ni very intelegency aka bonge la kichwa.
 
msimlaumu Mh Pinda, mzilaumu sheria zenu na jinsi zinavyotengenezwa na kupitishwa pitiswa kisiri siri, hata hili la posho za wabunge kupandishwa kinyemela msiwalaumu wabunge, shambulieni mfumo uliopo.

Kumlaumu Pinda ni sawa na kumwonea - tatizo si waziri mkuu au spika kulamba posho, tatizo ni mfumo mzima. ndiyo maana tunatengeneza katiba itakayoelekeza mamlaka ya kila kitu.
 
Kijana wa ccm huyo, si mtoto wa mkulima tena, na ndo maana Luanjo aliona nazingua wakati mpango anaujua
 
Katika sakata la Jairo, gazeti la mwanahalisi lilituonyesha orodha ya watu waliolipwa posho ya Tshs.280,000 kwa siku kwa Mheshimiwa Pinda, Spika wa Bunge, Mama Anna Makinda. Watu walianza kuhoji, uhalali wa waheshimiwa hawa kukubali posho kubwa kiasi hicho kwa msaa machache walizo kaa katika semina ya akina Jairo. Kosa la Pinda, lilikuwa dogo sana kwa sababu yeye aliletewa na hakuwa na bahati ya kuhoji sababu na uhalali wa kiasi hicho cha fedha. Pinda angeomba msamaha nadhani Watanzania wange msamehe tu.

Katika kujiondoa katika aibu, na kwa kukosa uzalendo na uungwana ameamua kuhalalisha kwa kushauriana na Mheshimiwa Spika, wapandishe posho ya kikao iwe Tshs.200,000 kwa siku na posho ya kujikimu Tshs. 80,000. Jumla yake ni shilingi 280,000, sawa na kiasi walichokipokea siku hiyo. Gharama kwa watanzania itakuwa kubwa kwa nia tu ya kuficha dhambi ndogo ya kupokea posho bila kuhoji.

Tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda, sio malaika, hata yeye anajua hilo, inakuaje atuingize hasara kubwa kiasi hiki na kwa miaka mingi ijayo. Mnaweza kumsamehe, ila mimi basi.

Unafiki mbaya sana, shangingi kakataa kwa vile linaonekana barabarani, posho anapokea kwa vile inakaa kwenye wallet. Jamani mwisho wa dunia ni lini tupumzike na maajabu ya duniani
 
inawezekena wameziba shimo la panya kwa mkate.

Hivi watu huwa mnatoa wapi maneno yenye kuchekesha kiasi hiki lakini yenye ukweli? Kweli JF kiboko, mimi Pinda nilimkosea imani siku nyingi tu alivyoanza kulia bungeni kujionyesha anathamini albino kumbe moyoni ni ili asifukuzwe kazi! Nakaribia kutoa tusi nimeogopa ban, lkn moyoni najua nilichokifanya.
 
Hawa ndo marais tunaowategemea,,,anajifanya kuwaonea watu huruma mpaka analia ....kumbe ilikuwa danganya toto......arudishe fedha zetu mara moja

Hana lolote! huwa anatoa machozi ya mamba!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom