Mheshimiwa Msechu unastahili pongezi

Nimekuwa nikitafakari kazi anazofanya mweshimiwa mchechu ni nzuri sana na anastahili pongezi. Tangu amekuwa mkurugenzi wa NHC ni mengi amefanya kuanzia na utawala na hatimaye upatikanaji wa makazi bora kwa watanzania. Upatikanaji wa makazi bora unapitia mchakato mrefu sana lakini at the end ameweza kufanikisha to some extent. Ana maamuzi ya busara na ya kutokuogopa( RISK TAKER) na ni smart. Hasiti kumpa mtu nafasi ya kuonyesha ujuzi wake professionally. Hii ndiyo siri ya mafanikio. Mimi mwenyewe nilipata nafasi ya kufanya naye kazi eventhough siko kikazi NHC. Pia natoa pongezi kwa viongozi kumwamini na kumchagua Wito wangu ni kwa sister organisations kumuunga mkono mia kwa mia mfano tanesco, maji, tanroad, TBA na nyinginezo ili kurahisisha utekelezaji wa project alizoazisha na anazoplan kufanya. Hatimaye na mimi nitaweza kupata nyumba inayomilikiwa na NHC. Marafiki zangu mnaofanya kazi NHC Juhudi zisipungue Wito wangu kwa JF panapostahili kusifiwa ni vizuri tukasifia: HONGERA SANA MH.MCHECHU KWA KAZI NZURI
Hakuna lolote hapo, jiulize hizo nyumba za NHC ni watu wangapi wenye kima cha chini wanaoweza kununua nyumba ya TShs 100m... Hii misomi ya Tz sijui imelogwa? Niliwakuta one time eti watu wa masoko NHC wameenda kuzitangaza hizo nyumba zao kwa walimu wa shule za msingi...what nonsense? Ni upuuzi mtupu...wanagapi wanaweza kuzinunua? T Tuache kudanganyana hapa, propaganda hazitaisadia hii nchi, inazidi kuangamia.. Nitamsifu Mchechu kama atakuja na project ambazo ni feasible kwa watu wa kawaida na sio hizi project za sasa hivi...
 
Niliwahi kumkubali kidogo Mchechu kipindi fulani wakati anaanza pale alipowakurupua wahindi na serikali kwa kulimbikiza bill.

Ila baada ya kuusikia mpango mkakati wake wa miaka mi5 kujenga nyumba elfu 5 nchi nzima....

Toka hapo nguvu zimeniisha nabaki namuangalia tu....
NHC ni takataka nyingine tu kama mashirika mengine ya kipuuzi ya taifa hili....

Kama we una matumaini na Mchechu na NHC yake, haya kila la kheri....

Tutayaona na tutayasikia......!
 
NHC inahitaji kufanya vitu vitatu ambavyo naona ndiyo majukumu ya msingi :

1.kuwa na nyumba nyingi za kupanga mijini kwa kodi ya bei nafuu kusaidia wanachi wenye kipato cha chini.hii ikibidi hata kwa kutengewa fungu kutoka serekalini kila mwaka kupitia wizara ya ardhi na maendeleao ya makazi.hili ndilo jukumu kuu la kuanzishwa kwake.

2.Kujenga nyumba za bei nafuu kwa kutumia teknolojia rahsi kama hizo hydrofoam blocks n.k za kuuza kwa wananchi kwa bei nafuu.

3.Kujenga na nyumba za ghali hizo kwa kimombo wanasema "high end houses" kwani hizo pia soko lake lipo.

sasa ni kipi wanachofanya sasa hivi kati ya hivi ?
wanaimplement number three
 
Ukitaka kujua uozo wa NHC kaulize wafanyakazi wake! Wengi wamekata tamaa na Mchechu amebadilisha Malengo ya awali ya Shirika! Leo shirika la nyumba la taifa halina tena hadhi ya Utaifa, ni kama Taasisi binafsi ya kibiashara! Mchechu aliahidi Kujenga Nyumba 15000, Muulize leo hii ameshajenga Nyumba ngapi?? Leo hii shirika lina Engineer mmoja tu, ambaye kwa stress ambazo alizipata alitaka kuacha kazi mwaka jana, akabembelezwa kwa kuwa tu yeye ndiye pekee ana muhuri unaokubaliwa kuidhinisha miradi mikubwa!! Kuna wazee wana matatizo ya kiafya ila Mchechu awehamishia kwenye remote areas kama Bukoba, shinyanga, singida Lindi na kwennengineko, ambapo kwa mahitaji yao matibabu wanatumia pesa nyingi na muda mwingi kwenda Dar esalaam kwa matibabu yao! Kaulize viwanja vya NHC walioziwa Wakubwa kwa bei chee! Utalia! NHC sio kwa watanzania wa kawaida tena!!

Nadhani hata kabla ilikua hivyo na kwakweli ilikua kwa watu flani na wahindi tu! Mtu ananyumba sehemu nyingine ile ya NHC anapangisha kodi kubwa so ilkua ni miradi ya watu,sasa pengine wamethibitiwa na sasa wameanza Majungu! Wazee walitakiwa wastaafu waache vijana wafanye kazi bwana!
 
Kujenga nyumba nyingi ni sawa kabisa, lakini angeanza na zile za kupangisha mijini na kuuza baadaye
 
Back
Top Bottom