Mheshimiwa Msechu unastahili pongezi

I have a dream,

Tendo la kumsifia ndani ya JF ya 2012 Mtanzania mwenzio kwa mema au mafanikio aliyosotea na kuyapata ni kusaka matusi na kejeli.

Pamoja na hayo, ukweli unabaki kuwa ukweli; Nehemia anafanya kazi na kutoa matokeo yenye mafanikio ya hali ya juu. Ni rahisi kwa kipofu kushuhudia hili kuliko baadhi ya wana-JF

Msikimbilie kujificha kwenye shuka la positivism. Nimeuliza swali naomba nijibiwe? watanzania ambao makundi mbali mbali ya wanasiasa yanawaahidi kuwakomboa wanaweza kununua nyumba za mchechu? au na wewe ni mmoja wa watu ambao wakiona magorofa wanasema tunaendelea?
 
jamaa yupo smart sana ata roma haikujengwa kwa sku moja bt mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Mchechu anajtaidi
 
You may be right but missing some points. Shirika la Nyumba la Taifa si sawa na benki binafsi eg. CBA. For one thing, NHC ni shirika la umma. Lengo lake si kuingizia serikali mapato. Bali ni kutoa huduma kwa watanzania. Yes. Linapaswa kujiendesha kwa faida lakini lengo kuu si profit maximization. Unapoendesha shirika hili, ambalo waasisi wake walilenga watu wenye kipato cha kawaida, kama benki ya biashara unakuwa unaongozwa na malengo ya kutengeneza faida kubwa ili usifiwe (Kama unavyomsifia Bosi wa Posta) na kuwasahau walengwa ambao ni Watanzania wa kipato cha kawaida. Huyu Bwana amelichukua Shirika likiwa halina uwezo wa kifedha (so they say). Hivyo, akaamua kuja na style ya kujenga nyumba kwenye "prime plots" za shirika hili na kuziuza ili kujenga uwezo wa kifedha (ninaambiwa hata mtumishi wa NHC ni shughuli kupata nafasi ya kuuziwa nyumba hizo, if you know what I mean). Fine. Uwezo wa kifedha utaongezeka (if it works) lakini asset za shirika zitapungua. Kupungua kwa assets za shirika kunapelekea kufa kwa shirika, regardless of how much money you have at hand. Na kumbuka kutengeneza faida kubwa si lengo la shirika.

Lengo la shirika ni kuwapatia Watanzania makazi bora kwa gharama nafuu. Kabla ya huyu bosi kuongoza Shirika na inavyofanyika nchi nyingine, Shirika hili linapaswa kujenga makazi bora ya gharama nafuu na kuendesha renting business. Watanzania walio wengi watamudu kulipa gharama ya pango kila mwezi lakini hawawezi kumudu kulipa Shilingi 100 million kwa mkupuo. Hawakopesheki. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza rushwa. Itaongeza ufanisi wa kazi. Badala ya mfanyakazi kufikiria namna ya kuiba ili aweze kujenga nyumba au kununua nyumba ya NHC, atatulia na kufanya kazi. Kwa sababu uhakika wa makazi anao. Na usipolipa pango kwa mwezi, unatolewa anapewa mtu mwingine. This is how it should work. NHC isishindane na mabenki kutengeneza faida kubwa. Hili ni shirika la umma. Lilenge kutoa huduma zaidi. And yes. Linastahili ruzuku ya serikali at some point (economists hate subsidy arguing it's an inefficient way to allocate resources. But who doesn't do it?).

Na NHC ikifanya kazi yake vizuri, gharama ya pango inayotozwa sokoni kwa sasa itaji-regulate vizuri sana. Kwa sasa wenye nyumba wanatoza bei yeyote wanayotaka. Hakuna wa kumuuliza. Na kwa kuwa kuna shida ya makazi, watu wanaishia kuiba ili kumudu gharama za pango. Mishahara haiendani na gharama za pango sokoni. Watu wanamudu vipi kulipa kama si kwa kuiba?

Bw. Mchechu, NHC ni mkombozi wa Watanzania linapokuja swala la makazi.Jitahidi kuhudumia Watanzania wenye mahitaji na si matajiri wanaotafuta kujilimbikizia mali. Kwa kuuza maeneo mazuri ya NHC, huna tofauti na wale waliojiuzia nyumba za Serikali. We are counting on you!

Kidude cha LIKE hakipo kwenye post yako tu, nadhani mods wanania ya kuhujumu mawazo yako,umeeleza kwa ufasaha sana kile mimi nilichoshindwa kuelezea kiasi cha kupelekea mtu mmoja hapo juu kuandika katika namna inayomaanisha kwamba watu hapa JF hawana shukrani na hawapendi mafanikio ya watu wengine. NAKUPA LIKE MKUU. spiritual-thinker na Ericus Kimasha karibuni mchangie kwenye hii post.
 
Watanzania huwa wananishangaza sana, wapo wanao onekana kupenda maendeleo kwa maneno lakini anapotokea mtu anayetekeleza mipango ya maendeleo kwa vitendo wanapiga mayowe. Mchechu ni katika majembe machache sana yaliyo kwenye mashirika ya umma chini ya serikali ya magamba. Hili shirika lilikuwa linakufa kama asingetokea Dr. Magufuli kuliokoa ile mwaka 2006. Hata hivyo halikuwa na kiongozi visionary na chapa kazi kama Mchechu.

Huna aibu kusema anatafuta sifa kwa kutoomba fedha serikalini???!!! Hivi akianza kutegemea fedha kutoka kwenye serikali hii dhaifu ya magamba kuna mradi hata mmoja utakaofanikiwa!! hawawezi kununua CT scan, watajenga nyumba??? Ndugu yangu use the white matter in your skull.

Eti, amezoea profitability!!! Unataka aliongoze shirika kwa hasara ili muuziane kama mlivyozoea kufanya kwa kisingizio cha hasara??!!

All in All Mchechu is a rare gem. Jembe lingine la kwenye shirika la umma ni new CEO wa Posta Bank Mr. Moshingi, ndani ya mwaka wake mmoja ofisini, profit growth 300 perc. Bravo!! this is what we want.

wote wanaomsifu na wanaomkandia lao moja ni kumuaanika ili akikosea as normally human beings do, watu wapate pa kuanzia kumsimanga. sitashangaaa miongoni mwa wanaolia sana ndio waliomuua marehemu. yangu macho mttakuja kuniambia sio siku nyingi. Kyando-Mchechu , angalia akumulikaye mchana usiku atakuchoma. Zingatia wajibu wako LUKOLO
 
Ukitaka kujua uozo wa NHC kaulize wafanyakazi wake! Wengi wamekata tamaa na Mchechu amebadilisha Malengo ya awali ya Shirika! Leo shirika la nyumba la taifa halina tena hadhi ya Utaifa, ni kama Taasisi binafsi ya kibiashara! Mchechu aliahidi Kujenga Nyumba 15000, Muulize leo hii ameshajenga Nyumba ngapi?? Leo hii shirika lina Engineer mmoja tu, ambaye kwa stress ambazo alizipata alitaka kuacha kazi mwaka jana, akabembelezwa kwa kuwa tu yeye ndiye pekee ana muhuri unaokubaliwa kuidhinisha miradi mikubwa!! Kuna wazee wana matatizo ya kiafya ila Mchechu awehamishia kwenye remote areas kama Bukoba, shinyanga, singida Lindi na kwennengineko, ambapo kwa mahitaji yao matibabu wanatumia pesa nyingi na muda mwingi kwenda Dar esalaam kwa matibabu yao! Kaulize viwanja vya NHC walioziwa Wakubwa kwa bei chee! Utalia! NHC sio kwa watanzania wa kawaida tena!!
 
Huyu Bwana namfahamu tangu akiwa chuo kikuu, na kamradi kake ka Bar baadae akahamia kwenye daladala. He has a business oriented mind. Leo hii ukimwambia aendeshe shirika kama NHC na asifikirie kutengeneza faida, ila awe kisiasa zaidi ili awaguse moyo Watanzani wa hali ya chini. Atarudisha huo CEO kesho asubuhi kwa wizara husika.
 
Hili nalo ni siasa?Mods ebu tusaidie hapo kama siyo plz do the needful
 
Sifa anazopewa hazina mashiko kivile kwani bei za nyumba zinazojengwa na NHC hazishikiki. Au NHC imebadilishiwa SABABU ya kuanzishwa kwake? Yaelekea haipo tena kwa ajili ya wananchi wa 'kawaida'.
Bei za chini ni Tsh 150 milioni, nani atamudu kama sio wachache wa kipato cha juu sana?
Uliza bei ya za Arusha, utachoka.
Pia NHC ina WAKURUGENZI wengi sana, na nafasi nyingi zimeundwa wakati huu wa Mchechu, na kipato chao si mchezo, hivyo gharama zote hizo zinaenda kwa 'mnunuzi' wa nyumba ya NHC.
Pia hii Thread si ya kuwekwa kwenye 'Siasa'.
 
Nimekuwa nikitafakari kazi anazofanya mweshimiwa mchechu ni nzuri sana na anastahili pongezi.

Tangu amekuwa mkurugenzi wa NHC ni mengi amefanya kuanzia na utawala na hatimaye upatikanaji wa makazi bora kwa watanzania. Upatikanaji wa makazi bora unapitia mchakato mrefu sana lakini at the end ameweza kufanikisha to some extent. Ana maamuzi ya busara na ya kutokuogopa( RISK TAKER) na ni smart. Hasiti kumpa mtu nafasi ya kuonyesha ujuzi wake professionally. Hii ndiyo siri ya mafanikio. Mimi mwenyewe nilipata nafasi ya kufanya naye kazi eventhough siko kikazi NHC.

Pia natoa pongezi kwa viongozi kumwamini na kumchagua

Wito wangu ni kwa sister organisations kumuunga mkono mia kwa mia mfano tanesco, maji, tanroad, TBA na nyinginezo ili kurahisisha utekelezaji wa project alizoazisha na anazoplan kufanya. Hatimaye na mimi nitaweza kupata nyumba inayomilikiwa na NHC.

Marafiki zangu mnaofanya kazi NHC Juhudi zisipungue

Wito wangu kwa JF panapostahili kusifiwa ni vizuri tukasifia: HONGERA SANA MH.MCHECHU KWA KAZI NZURI

Halafu tukiisha mpongeza SO WHAT?. Yaani tumpongeze mtu kwa kufanya kazi inayomletea kipato chake cha kila siku? kweli jamani kweli?, huu utamaduni gani sasa tumeanza nao?. Fanya kazi yako kwa kujituma waache watu wakukumbuke baadae kwa legacy yako. Hatuhitaji kumsifia ila tunahitaji kuangalia utendaji wake akikosea tutamshitua na akiwa sahihi tutakaa kimya. As long as nobody is shouting at him basi anafanya yale ambayo kila mtu aliyepewa dhamana anastahili kuyafanya.

Waswahili walisema MGEMA AKISIFIWA...
 
Halafu tukiisha mpongeza SO WHAT?. Yaani tumpongeze mtu kwa kufanya kazi inayomletea kipato chake cha kila siku? kweli jamani kweli?, huu utamaduni gani sasa tumeanza nao?. Fanya kazi yako kwa kujituma waache watu wakukumbuke baadae kwa legacy yako. Hatuhitaji kumsifia ila tunahitaji kuangalia utendaji wake akikosea tutamshitua na akiwa sahihi tutakaa kimya. As long as nobody is shouting at him basi anafanya yale ambayo kila mtu aliyepewa dhamana anastahili kuyafanya.

Waswahili walisema MGEMA AKISIFIWA...

Baelezee. mara January Makamba, mara Mchechu. Cjui ni 'kamtandao?'
 
jambo usilo lijua ni kama usiku wa kiza,mimi naamini baada ya post hii utalipwa hela na Mchechu kwa kumpa sifa za kijinga ambazo huyo tajiri yako hasitahiri,Nyumba za NHC zinauzwa kwa milion 100 kwenda juu,hapo analenga kuujia akina nani kama sio wenye pesa na sio watu wa kawaida tu, Mchechu analipwa milioni 24 kwa mwezi na pia posho za NHC kwa kikao chochote ni laki 3. MCHECHU ana ajiri watu kwa maelekezo na yeye anaowataka! Yeye mwenyewe ali ajiliwa kwa maelekezo ya Katibu Kiongozi wakati ule Mzee Luhanjo ambae ni mjomba wake! Mchechu ametengeneza directorate 12 badala ya 5 alizo zikuta,na directors wote wanapata take home ya 8 milioni kwa mwezi na wote ni rafiki zake! Kuna madudu mengi ambayo yana fanyika NHC baada ya miaka miwili Mchechu atanuka kwa kashifa!
 
Kwanza kabisa, nakubaliana 100% na pongezi alizopewa Mr. Mchechu. NHC ni shirika ambalo lazima lijiendeshe kibiashara for at least the next 10 yrs, ili kujenga faida na capital base ya kuanza kufikiria hizo nyumba za bei nafuu.

Huo uozo kwamba mashirika ya serikali ni ya kutoa huduma, ndiko kulikopeleka TANESCO, TTCL, ATC kuwa mzigo kwa serikali na at the same time kutoa huduma mbovu, yaani LOSE LOSE situation.

Demand ya nyumba za Middle class ni kubwa mno, so Mchechu ana cover area ambayo inawafikia vijana wengi walioanza kazi, na hizo nyumba zinauzwa kwa mikopo ambayo NHC wameline up kupitia mabenki mbalimbali nchini.

NHC kwa kufuata upuuzi wa kisiasa iliingia JV na majambazi wanaotengeneza hela za kufa mtu, wakati shirika lina pata 20% while ni owners wa hizo prime plots zilizojengwa. Mlikuwa wapi kulaani huo uozo??

Sasa Mchechu anaanza mambo ya maana na yanayotakiwa kuigwa, ooh ajenge nyumba za bei rahisi, kwa pesa zipi??? Kuna hela zenye 0% interest mlizompatia?? NO Sasa shirika la NHC likipata faida, where do u think hizo Retained Earnings zitapelekwa?? Ndio uko kwenye nyumba za bei nafuu, lakini sio sasa wakati shirika limekuwa Mismanaged for the past 20 yrs +.

Mchechu mkuu mwnedo mdundo, faida zitaonekana uko mbeleni.

May God Bless Tanzania.
 
Disgusting. Orodhesha hayo mafanikio unayosema kwa Watanzania. NHC inapaswa kujenga low cost housing nyiiingi ziwanufaishe Watz wengi. Sasa mill 150 si za matajiri na process ya kuziuza ni rushwa tupu? Hamna issue. Atimize malengo ya NHC kwa walengwa sio kubabaisha kwenye TV na yule jamaa wa Clouds as if kuna chochote tunachofaidi kwenye hivyo vipindi.

Afadhari nawe useme, kuna siku nilichangia nikadakwa juujuu.
Kenya wana mifano mizuri sana ya low cost housing. Wana Estates nyingi za bei nafuu na wala hakuna mizengwe kama huku.
Za NHC za kununua kwa tenda au kwa uwezo, mafisadi wananunua zote na kulipa cash halafu watapangisha kwa bei ya juu. Unafuu gani huo.
 
Huyu Bwana namfahamu tangu akiwa chuo kikuu, na kamradi kake ka Bar baadae akahamia kwenye daladala. He has a business oriented mind. Leo hii ukimwambia aendeshe shirika kama NHC na asifikirie kutengeneza faida, ila awe kisiasa zaidi ili awaguse moyo Watanzani wa hali ya chini. Atarudisha huo CEO kesho asubuhi kwa wizara husika.
Na atakapotakiwa kuwasilisha mchango kwa Chama kwa ajili ya Uchaguzi 2015? atafanyaje?
 
NHC inahitaji kufanya vitu vitatu ambavyo naona ndiyo majukumu ya msingi :

1.kuwa na nyumba nyingi za kupanga mijini kwa kodi ya bei nafuu kusaidia wanachi wenye kipato cha chini.hii ikibidi hata kwa kutengewa fungu kutoka serekalini kila mwaka kupitia wizara ya ardhi na maendeleao ya makazi.hili ndilo jukumu kuu la kuanzishwa kwake.

2.Kujenga nyumba za bei nafuu kwa kutumia teknolojia rahsi kama hizo hydrofoam blocks n.k za kuuza kwa wananchi kwa bei nafuu.

3.Kujenga na nyumba za ghali hizo kwa kimombo wanasema "high end houses" kwani hizo pia soko lake lipo.

sasa ni kipi wanachofanya sasa hivi kati ya hivi ?
 
Nehemiah, we appreciate your job. Endelea hivyo hivyo. Jenga nyumba za middle class, sisi wengine tutazinunua. Wanaotaka nyumba za bure bure waende makanisani au misikitini. Na kama dar wakizidi kukuzengua njoo uzijenge hizo nyumba kule LUDEWA.
 
Natamuunga mkono, akiwafukuza wahindi katikati ya miji, wao kina nani? mbona watanzania weusi sijawahi kuwaona mjini?
 
jambo usilo lijua ni kama usiku wa kiza,mimi naamini baada ya post hii utalipwa hela na Mchechu kwa kumpa sifa za kijinga ambazo huyo tajiri yako hasitahiri,Nyumba za NHC zinauzwa kwa milion 100 kwenda juu,hapo analenga kuujia akina nani kama sio wenye pesa na sio watu wa kawaida tu, Mchechu analipwa milioni 24 kwa mwezi na pia posho za NHC kwa kikao chochote ni laki 3. MCHECHU ana ajiri watu kwa maelekezo na yeye anaowataka! Yeye mwenyewe ali ajiliwa kwa maelekezo ya Katibu Kiongozi wakati ule Mzee Luhanjo ambae ni mjomba wake! Mchechu ametengeneza directorate 12 badala ya 5 alizo zikuta,na directors wote wanapata take home ya 8 milioni kwa mwezi na wote ni rafiki zake! Kuna madudu mengi ambayo yana fanyika NHC baada ya miaka miwili Mchechu atanuka kwa kashifa!

Duh duh... Huo ulaji ni hatari & haufai kabsaaaaa...
 
Back
Top Bottom