Katika mambo yaliyousikitisha umma wa wastaarabu wa Tanzania katika kampeni za Arumeru Mashariki ni kauli chafu iliyotolewa na mbunge wa mtera (sijui ni mheshimiwa au ni kichaa) Livingistone Lusinde. Pamoja na mambo maneno mengine aliyoongea kwa kujiamini ni suala la kudai kuwa Mheshimiwa mbunge wa Arusha mjini alipata alipata bwana wakati akiwa mahabusu. Ni maneno ya aibu kutoka kwa mwanachama wa chama ambacho serikali yake inajitapa kuwa inafuata utawala wa sheria. Ni kauli ya kusikitisha ila kwa maana nyingine inataka kutupa ujumbe ufuatao:-
Kwa kuwa jeshi la magereza halijakanusha kutokea kwa kitendo hicho, na kwakuwa maneno hayo yalitoka kwa mtu wa CCM, hii inatuthibitishia kuwa hata kama Lema hakupata bwana, Serikali ya CCM ikishirikiana na jeshi la magereza huwa inaweka mafirauni inaowafahamu ndani ya mahabusu ili kuwafanyia vitendo vibaya watu ambao serikali ya CCM inawabambikizia kesi.
Kwa kuwa CCM haijamkemea wala kumwadhibu huyo mwanachama wake, hii inatufanya tuamini kuwa serikali ya CCM inafadhili na kusimamia vitendo vya udhalilishaji wa raia wake inayotamba kuwa waliiweka madarakani kwa ushindi wa Tsunami.