Mheshimiwa diwani afariki dunia

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722


CCM yapoteza diwani


na Elizabeth Kilindi, Tanga


DIWANI wa Kiomoni, Masota Mayala (CCM), amefariki dunia juzi kutokana na maradhi ya mapafu na ubongo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mtoto wa marehemu, Kelvin Mayala, alisema kifo cha baba yake kimetokea ghafla na ni pigo kubwa kwao.
" Kifo cha baba yetu ni pigo kubwa kwetu na familia kwa ujumla kwani alikuwa ni nguzo katika maisha yetu," alisema Mayala.

Alisema baba yao alianza kusumbuliwa na maradhi hayo tangu mwezi uliopita na alikwenda katika Hospitali ya Masana, iliyopo Mbezi, Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Tanga, Lusia Mwiru, alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwao na serikali kwa ujumla, kwani diwani huyo alikuwa ni mwadilifu na mchapa kazi.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego alisema wilaya yake na CCM waimepata pigo kwa kumpoteza diwani huyo ambaye alikuwa mshauri mkubwa wakati wa kutekeleza ilani ya chama hicho.

Alisema mazishi ya Diwani Mayala yamefanyika jana katika kata hiyo.
 
Back
Top Bottom