ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Wana jamvi salam.
Waziri mpya wa nishati na madini, anaweza kujiuzulu kama kweli hatoendekeza siasa za CCM. Nasema siasa za CCM kwa kuwa yeye mpaka kuteuliwa kwake kuwa waziri wa wizara hiyo inayohesabu hasara kila mwaka, hakuwa kwenye siasa na wengi tulitarajia uwajibikaji uliotukuka.
Bodi ya wakurugenzi TANESCO, ilikutana mjini dodoma kwa lengo la kuangalia namna ya kuwasimamia watendaji wa Tanesco ili wizara hiyo isiingie tena katika kashfa. kati ya wana bodi, yumo ROBERT MBOMA aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi.
Ni kwa kutumia uzoefu wake, watendaji wa TANESCO waliamliwa kuwakatia wadaiwa sugu wa umeme na kwa kuanzia Jeshi la wananchi JWTZ na Jeshi la polisi, walikatiwa umeme tangu 16 may 2012 hadi 17 may 2012 umeme uliporudishwa majira ya saa nne usiku, na hili ni kwa jeshi la polisi, sijajua jeshi la wananchi ilikuwaje.
Majeshi yote walifika tanessco na kuambia wameagizwa kukata umeme na viongozi wao kwani JWTZ wana deni la bilio 6, huku jeshi la polisi wana deni la bilion 5.
kama umeme umerudishwa:-
1. Je madeni hayo yamelipwa?
2. Kama hayajalipwa, je waziri au watendaji wake wameamliwa kurudisha umeme kwenye taasisi hizo?
3. Kama wameagizwa na mamlaka za juu, je si kuingiliwa?
NB. Ikumbukwe kuwa majeshi yote huwa yanawasilisha bajeti, sasa kudaiwa hadi bilion tano, na sita fedha ya bajeti kwa matumizi ya umeme zilitumikaje?
my take.
Namshauri waziri, kama hawajalipa madeni hayo wakatiwe ili kuleta nidham ya matumizi ya fedha za walipa kodi na kama akilazimishwa kuwapa umeme, basi abwage manyanga kwani mda unakuja naye atatakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia wizara yake