Mhe. Pinda apigilia msumari kauli yake: Serikali haitavumilia fujo zozote!

Kama kweli ana nia ya kupambana na wanaopandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa Watanzania basi wa kwanza anayestahili kukamatwa na kushughulikiwa ipasavyo ni mzushi, gaidi muuaji mwigulu nchemba. Haoni wala kusikia yanayofanywa na huyu muuaji!? Aache usanii banaaa!!! na kauli zake fyongo.

Katika gazeti la Nipashe leo 29 Juni 2013, Mhe Pinda amenukuliwa:
"Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.

"Serikali itachukua hatua bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya Taifa letu...na vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii".
 
nasikia mkutano ule haukuwa na fujo zozote ila hilo la bomu inaelekea lilisukwa.

Kuondoa mzizi wa fitna ni kuweka wazi ile clip ili aliyerusha hilo bomu ajulikane wazi-awe polisi au vinginevyo.
Sasa ninelekea wiki ya pili hata kwenye youtube haijawekwa, wasi wasi unantanda kuwa si ajabu aliyepanga swala zima halijaenda kama lilivyotarajiwa-ama sivyo ukimya huu una maana gani?

ile clip ni noma wale jamaa waliosema wanaushahidi itawaumbua maana ni wapo waliopanga dili hivyo jeshi la polisism linatakiwa kuja na ushahidi wa kina haswaa na wale ma big boss/sponsor waliomtuma mrushaji wakamatwe ili tujue motive behind. Mzee mzima mbow..itamuumbua haito hiyo, polisi usalama wafanye kazi yao..
 
Kaa na wajukuu umezeeka,na mkeo yule watano anakutaka nyumbani.

Umeulizwa ama anakumbukumbu kama za kuku?? We unaanza kuzungumza maisha yake binafsi... Kutokukaa na wajukuu wake ama kutokumuona mkewe kuna waathiri nini watanzania in comparison na hizo kauli tatanishi za mtoto wa mkulima aliejisahau alikotoka!!

Acheni hizo bwana, kama mtu kakosea si anasemwa kakosea, kama alikuwa na uwezo wa kutetea kauli yake mbona spika aliingilia kati kuokoa jahazi!!!

Watu wengine sijui mnafikiri kwa kutumia VINENA vyenu!!
 
Mbona angesema hivyo watu wala wasingempigia kelele? au ana kumbukumbu kama za kuku?

hapa suala ni kwamba akiri kauli ya awali ni ya kuipinga yeye mwenyewe na sio kutoa kauli ya kuyeyusha kauli ya mwanzo.

ni kupiga tu ....... na ukikaidi amri ni kipigo tu.
 
Hapa alichosema Pinda ni kauli ambayo inategemewa kutoka kwa kiongozi wa nchi. Kuwashughulikia wafanya fujo ni kuwapeleka mahakamani na kuwashitaki si kuwapiga mitaani. Hapa sioni tatizo lolote na kauli yake. Ila mleta mada anashindwa kuona tofauti kati ya kauli hii na kauli ya kuruhusu polisi kupiga raia.
Kweli mleta mada akili zako ni za KIPINDA PINDA
 
At last Mhe Pinda amewajibu wale waliokuwa wakihoji hoji tamko lake la kuwashughulikia kwa kuwapiga watakao leta fujo nchini.
Ni tamko linalotia moyo na kurudisha heshima ya nchi na kudumisha amani kwa nguvu yoyote ile.
Wale waliosikika wakisema nchi haitotawalika wako kimya .
Hata Yule mama Helen Bisimba hajawahi kutolea tamko huu usemi wa nchi kutokawalika, kimsimamo wa haki za binadamu maana yake nini hasa, na nchi itakuwaje isipotawalika.

Katika gazeti la Nipashe leo 29 Juni 2013, Mhe Pinda amenukuliwa:
"Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.

"Serikali itachukua hatua bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya Taifa letu...na vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii".

Wakati huo huo wengi tunajua kuwa kuna mbunge asiyejiheshimu amemtukana Waziri Mkuu mtandaoni.
Na mwingine yuko on record akisema polisi wamerushia mabomu wananchi ili wawaue huko Arusha

Sasa hapa ni patamu, maana waziri Mkuu asingesema aliyoyasema bila kuwa na background information.

Ni vizuri upande unaojisikia unakusudiwa ujisafishe haraka katika jamii, maana wamesha jipakaa tope la kusika na fujo zilzopelekea mauaji nchini.

Kwa kifupi waswahili wana sema CDM should come clean!!

Thus very nice statement! Watu wanatamka hadharani kuwa nchi isitawalike bado human right walinyamazia kimya angali waliyaona.Nafikira nivema ukalizimishiwa amani pale unapoivunja.
 
Thus very nice statement! Watu wanatamka hadharani kuwa nchi isitawalike bado human right walinyamazia kimya angali waliyaona.Nafikira nivema ukalizimishiwa amani pale unapoivunja.
Unafiki huwa unaumbua!
Huyo mama Bi Simba sijawahi kusikia tafsiri yake ya nchi kutotawalika na jinsi haki za binadamu wengine zinavyofinyangwa na hao waleta fujo.
 
PM kaongelea ishu ya mbunge kuandika matusi kwenye mtandao na mambo ya bomu Arusha au kaongelea kuhusu kauli yake ya kupambana na wachochezi
na wavunjifu wa amani?

au hapo umeamua kuunganisha habari mbili kutengeneza conclusion?

carter nimesoma gazet leo kuwa huyo MBUNGE hana kesi ya Kujibu,
 
Last edited by a moderator:
Thus very nice statement! Watu wanatamka hadharani kuwa nchi isitawalike bado human right walinyamazia kimya angali waliyaona.Nafikira nivema ukalizimishiwa amani pale unapoivunja.
Amani huwa hailazimishwi ndugu huwa inajengeka pale pande zote zinapokuwa na Busara na kuheshimiana, Kama akina Lusinde, Mwigulu, Selukamba, Juma Nkamia na wengine ndani ya CCM wamatoa kauli zisizo stahili na wanaonekana hawana makosa laki Sugu, Lisu na wengie wa upinzani wanapotoa kauli ambazo pia si stahili wanaonekana wamefanya makosa makubwa sana unatarajia amani itapatika?
 
Mbona angesema hivyo watu wala wasingempigia kelele? au ana kumbukumbu kama za kuku?
Taratibu mkuu, Sugu must be sorry now for his verbal diarhea.
Halafu mtu mzima unapokuwa kama Sugu, nawe ni thinker wa CHADEMA, its despicable.
I demand better than this.
 
Mheshimiwa waziri mkuu pinda uko sahihi kabisa, nchi zote duniani zina taratibu na sheria na si lazima watu wote wazipende hapana ila lazima watu wote wazifuate na kuziheshimu maana hakuna hata siku moja sheria na taratibu zote zikapendwa na raia wote....... Na ndio maana tunaona kuna watu wameandamana afrika ya kusini kupinga ziara ya rais wa dunia 'obama' lakini haina maana kwamba wao wanawakilisha wananchi wooote wa south africa .....hapana..... Wana maslahi yao wanayoyajua wao ......... Muheshimiwa uko sahihi kabisa kazi ya dola ni kuhakikisha sheria na taratibu za nchi zinaheshimiwa na kufuatwa na ni wajibu wa serikali kukumbusha kuwa utii bila shuruti ni jambo muhimu kwa jumuia yoyote duniani..... Haiwezekani kila mtu au kikundi cha watu fulani wakajifanyia mambo wanayotaka katika nchi ...hapana hiyo itakuwa vurugu tupu.... Taratibu lazima zifuatwe na ziheshimiwe popote. Mungu ibariki tanzania. Siasa za tanzania kwa sasa ni aibu kuna wahuni, kuna watu wako tayari watu masikini wafe ama wadhurike ili wao wafaidike kisiasa............ Ama wapumbavu ndio waliwao.
 
carter nimesoma gazet leo kuwa huyo MBUNGE hana kesi ya Kujibu,

Thanks mkuu kwa kunielewesha! Maana mtoa mada anataka kumuwekea PM maneno mdomoni kwa kuandika mambo ambayo hayapo!

me najua PM katetea kauli yake kuhusu polisi kupiga raia! Ila mleta mada kaunganisha na mambo yake ya mbunge na matusi na bomu la Arusha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom