Mhe. Pinda apigilia msumari kauli yake: Serikali haitavumilia fujo zozote!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,906
13,211
At last Mhe Pinda amewajibu wale waliokuwa wakihoji hoji tamko lake la kuwashughulikia kwa kuwapiga watakao leta fujo nchini.
Ni tamko linalotia moyo na kurudisha heshima ya nchi na kudumisha amani kwa nguvu yoyote ile.
Wale waliosikika wakisema nchi haitotawalika wako kimya .
Hata Yule mama Helen Bisimba hajawahi kutolea tamko huu usemi wa nchi kutokawalika, kimsimamo wa haki za binadamu maana yake nini hasa, na nchi itakuwaje isipotawalika.

Katika gazeti la Nipashe leo 29 Juni 2013, Mhe Pinda amenukuliwa:
"Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.

"Serikali itachukua hatua bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya Taifa letu...na vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii".

Wakati huo huo wengi tunajua kuwa kuna mbunge asiyejiheshimu amemtukana Waziri Mkuu mtandaoni.
Na mwingine yuko on record akisema polisi wamerushia mabomu wananchi ili wawaue huko Arusha

Sasa hapa ni patamu, maana waziri Mkuu asingesema aliyoyasema bila kuwa na background information.

Ni vizuri upande unaojisikia unakusudiwa ujisafishe haraka katika jamii, maana wamesha jipakaa tope la kusika na fujo zilzopelekea mauaji nchini.

Kwa kifupi waswahili wana sema CDM should come clean!!
 
Mkutano wa Chadema Arusha kulikuwa na fujo hata wapige bomu na kuua raia na wengine majeruhi?
 
Nasikia mkutano ule haukuwa na fujo zozote ila hilo la bomu inaelekea lilisukwa.

Kuondoa mzizi wa fitna ni kuweka wazi ile clip ili aliyerusha hilo bomu ajulikane wazi-awe polisi au vinginevyo.
Sasa ninelekea wiki ya pili hata kwenye Youtube haijawekwa, wasi wasi unantanda kuwa si ajabu aliyepanga swala zima halijaenda kama lilivyotarajiwa-ama sivyo ukimya huu una maana gani?
 
PM kaongelea ishu ya mbunge kuandika matusi kwenye mtandao na mambo ya bomu Arusha au kaongelea kuhusu kauli yake ya kupambana na wachochezi
na wavunjifu wa amani?

au hapo umeamua kuunganisha habari mbili kutengeneza conclusion?
 
At last Mhe Pinda amewajibu wale waliokuwa wakihoji hoji tamko lake la kuwashughulikia kwa kuwapiga watakao leta fujo nchini.
Ni tamko linalotia moyo na kurudisha heshima ya nchi na kudumisha amani kwa nguvu yoyote ile.
Wale waliosikika wakisema nchi haitotawalika wako kimya .
Hata Yule mama Helen Bisimba hajawahi kutolea tamko huu usemi wa nchi kutokawalika, kimsimamo wa haki za binadamu maana yake nini hasa, na nchi itakuwaje isipotawalika.

Katika gazeti la Nipashe leo 29 Juni 2013, Mhe Pinda amenukuliwa:
"Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.

"Serikali itachukua hatua bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya Taifa letu...na vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii".

Wakati huo huo wengi tunajua kuwa kuna mbunge asiyejiheshimu amemtukana Waziri Mkuu mtandaoni.
Na mwingine yuko on record akisema polisi wamerushia mabomu wananchi ili wawaue huko Arusha

Sasa hapa ni patamu, maana waziri Mkuu asingesema aliyoyasema bila kuwa na background information.

Ni vizuri upande unaojisikia unakusudiwa ujisafishe haraka katika jamii, maana wamesha jipakaa tope la kusika na fujo zilzopelekea mauaji nchini.

Kwa kifupi waswahili wana sema CDM should come clean!!

importent country/state declines itself for their dirty plan.The sharper the toung is easy to cut his own throat on it.
 
PM kaongelea ishu ya mbunge kuandika matusi kwenye mtandao na mambo ya bomu Arusha au kaongelea kuhusu kauli yake ya kupambana na wachochezi
na wavunjifu wa amani?

au hapo umeamua kuunganisha habari mbili kutengeneza conclusion?

hiyo nafikiri ni kazi ya mwigulu!
 
Viva Pinda.

Kama unaona unaonewa hamia Somalia ama Sudani. Ila serikali haitovumilia wahuni wachache kuhatarisha amani ya Taifa.
 
At last Mhe Pinda amewajibu wale waliokuwa wakihoji hoji tamko lake la kuwashughulikia kwa kuwapiga watakao leta fujo nchini.
Katika gazeti la Nipashe leo 29 Juni 2013, Mhe Pinda amenukuliwa:
"Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.

"Serikali itachukua hatua bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya Taifa letu...na vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii".

Kwa kifupi waswahili wana sema CDM should come clean!!
Tunataka kama PM yupo serious na kauli yake basi pia achukue hatua dhidi ya Lipumba ambaye ameshiriki kueneza chuki za kidini kupitia misikitini. Na pia achukua hatua za haraka dhidi ya Mwigulu Nchemba ambaye anamtembeza na kumdhalilisha yule kijana Tesha na kupandikiza chuki za kisiasa katika jamii kwamba CHADEMA wanamwagia watu tindikali ilihali hakuna ushihidi wa dhahiri isipokuwa wa polisi kupiga watu na kuwalazimisha wakubali kwamba walimwagia tindikali.

Mbona CHADEMA hawajafukua maiti ya Mbwambo kule Arumeru mashariki na kuitembeza mitaani kwamba CCM wanaua watu? Mbona polisi hawatumii nguvu kama hiyo wanayoitumia dhidi ya wamwagia tindikali, kuwatafuta na kuwakamata wauaji wa Mbwana Masudi kule Igunga aliyeuawa na wanaCCM au Mbwambo kule Arumeru aliyeuawa na viongozi wa CCM? Tunataka PM afanye kazi kwa haki na usawa na si kuwapendelea wachache na kuwaumiza wachache kama anavyofanya Ndugai bungeni. Hatutakuwa tayari kuvumilia uonezi wa aina yoyote ile. Tunataka maamuzi yawe ni ya haki kwa wote.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
mtoto wa mkulima yuko vizuru sana..PM lazima uwe mkali,lazima uwe jasiri na mtu asiyependa masihara...naam lazima wanachi waokolewe dhidi ya matukio ya kigaidi yanayofadhiliwa na CDM.....MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom