Mhe. Edward Lowassa Richmond kuibuliwa 2008 kama si mapenzi ya Mungu Israel na aseme

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Binafsi niungane na wale wasemao kila jambo linapotokea kuna sababu. Zaidi ya hili kuna wasemao apangalo Mungu mwanadamu hawezi kulipangua.

Nasema haya kwa moyo wa dhati kabisa baada ya kukaa na kufikiri dhoruba aliyoipata Mhe. Edward Lowassa mwaka 2008 jambo ambalo wahuni wachache waliamua kulitumia ili kumwaribia heshima yake pamoja na kutaka kumchonganisha yeye na Watanzania.

Ila kwa kuwa Mungu hali ugali wala hanywi uji na kwa kuwa vile vile Mungu si Mwakyembe wala si Sitta hata kabla ya muhusika kuwaeleza Watanzania hali halisi juu tuhuma zile Mungu ameanza kuyadhihirisha haya kwa Watanzania bila shaka yoyote.

Alisema yeye si Mungu wa dhuluma wala si Mungu wa visasi ila yeye ni Mungu wa HAKI kwa watu wake wote na haki yake hiyo ndiyo aliyoanza kuidhihirisha mbele ya jamii na hata kuanza kuonekana kwamba hili jembe na huyu Raisi tumtazamiaye alibebeshwa furushi la misuri lisilomuhusu

Japo amekuwa akilaumiwa sana ila imeendelea kudhihirika kuwa yaliyomfanya kufikia uamuzi ule si mengine bali ni maadili yake aliyofundishwa Chamani na hivyo kuamua kuangikwa msalabani ili kuendelea kukipa heshima Chama chake na viongozi wake.*

Niseme tu Edward si jembe tu bali ni rato, reki, beleshi ni kila kitu. Nimejaribu kutazama tu tena kupitia ktk ile Mikoa inayojifanya eti haimkubali Mikoa ambayo haizidi 9 (na naamini tu hawamkubali Mdomoni ila Moyoni jamaa wanamkubali sana).

Katika hii Mikoa sasa, toka Mwaka 2010 ukianzia ngazi ya Kitongoji kila siku iwayo kwa Mungu watu 5-10 humzungumzia na humkubali sana huyu jamaa, ukienda ngazi ya Kijiji ni watu 11-30, Kata ni watu 31-50, Tarafa ni watu 51-80, Wilaya ni watu 81-199, na Mkoa ni watu 200-399 ndio ambao humzungumzia na zaidi humkubali huyu mtu.

Sasa kama hivi ndivyo zidisha mara Mikoa tuliyo nayo mara siku 365 mara miaka iliyobaki ili tuingie kwenye uchaguzi halafu jumlisha utendaji wake halafu vile vile toa maadui zake walioanza kurudi kwake bila kushurutishwa then nipe jibu Uraisi ataukosea wapi Nchi hii.......

Baada*ya hesabu hizo sasa fikiri je huyo balaa aliyepewa jina la Richmond kama angetokea mwaka huu ama mwaka kesho Urais Edward angeupata je manake ingemchukua muda sana kutumia busara kama aliyoitumia toka Mwaka 2008 hadi leo. Mwacheni Mungu aitwe Mungu bana......

You know what Edward; Haters hate b'se they hate seeing you DO BETTER!

Karibu *Ikulu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa........
 
Shondola u made my day,ni kweli daima mioyoni mwetu tutamkumbuka lowasa kwa kasi yake,maamuzi yake, utendaji wake,na uthubutu wake ni mtu wa kusema na kutenda,tuachane na fikra eti membe jamani membe kwa hakika ni dhaifu mara mia mbili kuliko huyu mbayuwayu...lowasa for 2015.
 
Mbona hilo ulilosema sisi twalijua, huyu mheshimiwa Lowasa aliubeba msalaba kunusuru chama na serikali yake. nakumbuka wakati nikihudhuria ibada pale Azania Front mwaka wa 2007-2010 kuna mzee mmoja alidiriki kuniambia nihame bench alilokuwa anapendelea kukaa mheshimiwa Lowasa eti ni fisadi, mimi nilimwambia yule mzee usihukumu usije ukahukumiwa, kama hizo tuhuma dhidi yake zingekuwa za kweli huyu mheshimiwa angekuwa amepatwa na pressure na angekuwa mgonjwa kitandani lakini kwa vile hahusiki ndio maana unamuona anaendelea na maisha yake ya kawaida. Nina hakika yule mzee kama yupo hai atakumbuka maneno yangu. Watu wengi siku hizi wana roho za chuki kiasi kwamba busara haina nafasi kwao, nawaasa ndugu zangu tupendane tutakiane mema sio kama najipendekeza isipokuwa nasema kilcho moyoni mwangu.
 
Huyo hata huku Monduli tumemchoka na hutumtaki tena.

Watu wanaweza kukuzungumzia kwa uovu na mabaya uliwafanyia na siyo mema.

Aende zake huko, kama anaubavu amvue nguo Kikwete, mtu ambaye alitaka kumvua gamba akashindwa huyo ndio saizi yake.
 
Ndugu zngu habari za leo, ni muda kidogo nilikuwa nje ya ulingo, namshukuru Mungu nipo leo tena, wapendwa wapenda amani na maendeleo ya TZ naomba mkae mchunguze ukweli upo wazi, jamani Kagame ni rais ambaye alitokea jeshini na ameifanya nchi yake kuwa kama ilivyo japo ameiongoza kwa mkono wa chuma kwa muda, lkn leo, kila nyumba pale Rwanda wana ng'ombe wa maziwa waliopewa na Rais wao kwa kuwajali watu wake, rwanda leo ina ndege zinazokwenda mpaka dubai zikichukuwa wa TZ jamani nasema tena, wanaochukia huyu Ndugu yetu Lowasa kuwa rais wanampango wao, lkn kwa hapa tulipo nchi inatakiwa kuwa na kiongozi ambaye hata marafiki zake wamuogope, na waogope ikulu na waogope haki ya wa TZ, fikilini eti TANESCO tena kuna ufisadi sababu, wakubwa hawakupewa ten percent kwa ajili ya vikombe vya kwenye nguzo za umeme, jamani haya mpaka lini? Lowasa peke yake ndiyo mtu atakae tufikisha mahala pakuona mwanga na faida ya rasiimali za zetu. Najua watu wengi mtaendelea kutukana au kusema wanao sema ukweli kuhusu huyu jamaa wamehongwa lkn TZ inahitaji mtu ambaye akikohoa wakuu wa mikoa wanaamka wanauliza tuwasaidieje wa TZ, wakuu wa wilaya wawatetemekee wa TZ wanao hitaji misaada ya serikali.
Ukweli ni taa hatakama ikombali utaiona, japo ni njiti ya kiberiti katikati ya giza la nchi yetu itaonekana Lowassa analifaa taifa letu na siyo CCM, porojo siyo ufanisi, najua Dr, anafaa zaidi lkn wakuu wa mikoa wameteuliwa na CCM kwahiyo Lowassa akisema wote wataogopa kz wataifanaya,
samahani kusema san lkn ukweli umenifanya kusema yote.
 
Hata angekuwa mzuri kupita vyote,CCm hatuihitaji 2015,Dr Slaa daima milele,sasa na baadae!

Dr. Slaa kwa Chama gani sasa?? Akajipange sawa sawa kama ambavyo Zitto Zuberi Kabwe amejipanga la sivyo mtakuwa mnampaka mzee wa watu mafuta kwa mgongo wa chupa.....
 
Ndugu zngu habari za leo, ni muda kidogo nilikuwa nje ya ulingo, namshukuru Mungu nipo leo tena, wapendwa wapenda amani na maendeleo ya TZ naomba mkae mchunguze ukweli upo wazi, jamani Kagame ni rais ambaye alitokea jeshini na ameifanya nchi yake kuwa kama ilivyo japo ameiongoza kwa mkono wa chuma kwa muda, lkn leo, kila nyumba pale Rwanda wana ng'ombe wa maziwa waliopewa na Rais wao kwa kuwajali watu wake, rwanda leo ina ndege zinazokwenda mpaka dubai zikichukuwa wa TZ jamani nasema tena, wanaochukia huyu Ndugu yetu Lowasa kuwa rais wanampango wao, lkn kwa hapa tulipo nchi inatakiwa kuwa na kiongozi ambaye hata marafiki zake wamuogope, na waogope ikulu na waogope haki ya wa TZ, fikilini eti TANESCO tena kuna ufisadi sababu, wakubwa hawakupewa ten percent kwa ajili ya vikombe vya kwenye nguzo za umeme, jamani haya mpaka lini? Lowasa peke yake ndiyo mtu atakae tufikisha mahala pakuona mwanga na faida ya rasiimali za zetu. Najua watu wengi mtaendelea kutukana au kusema wanao sema ukweli kuhusu huyu jamaa wamehongwa lkn TZ inahitaji mtu ambaye akikohoa wakuu wa mikoa wanaamka wanauliza tuwasaidieje wa TZ, wakuu wa wilaya wawatetemekee wa TZ wanao hitaji misaada ya serikali.
Ukweli ni taa hatakama ikombali utaiona, japo ni njiti ya kiberiti katikati ya giza la nchi yetu itaonekana Lowassa analifaa taifa letu na siyo CCM, porojo siyo ufanisi, najua Dr, anafaa zaidi lkn wakuu wa mikoa wameteuliwa na CCM kwahiyo Lowassa akisema wote wataogopa kz wataifanaya,
samahani kusema san lkn ukweli umenifanya kusema yote.

Karibu sana Jalem;

Hukusema sana kaka ila umesimamia ukweli unaouamini brother......
 
Tusiwe maskini wa akili hakuna Aja ya kupoteza muda kujadili uyu fisadi mkuu nchini,kama

Amebeba mazambi ya wengine hata akiwa raisi ataendelea ivyoivyo kubeba mazambi ya wengine,,muogopeni kama ukoma.
 
Ndugu zngu habari za leo, ni muda kidogo nilikuwa nje ya ulingo, namshukuru Mungu nipo leo tena, wapendwa wapenda amani na maendeleo ya TZ naomba mkae mchunguze ukweli upo wazi, jamani Kagame ni rais ambaye alitokea jeshini na ameifanya nchi yake kuwa kama ilivyo japo ameiongoza kwa mkono wa chuma kwa muda, lkn leo, kila nyumba pale Rwanda wana ng'ombe wa maziwa waliopewa na Rais wao kwa kuwajali watu wake, rwanda leo ina ndege zinazokwenda mpaka dubai zikichukuwa wa TZ jamani nasema tena, wanaochukia huyu Ndugu yetu Lowasa kuwa rais wanampango wao, lkn kwa hapa tulipo nchi inatakiwa kuwa na kiongozi ambaye hata marafiki zake wamuogope, na waogope ikulu na waogope haki ya wa TZ, fikilini eti TANESCO tena kuna ufisadi sababu, wakubwa hawakupewa ten percent kwa ajili ya vikombe vya kwenye nguzo za umeme, jamani haya mpaka lini? Lowasa peke yake ndiyo mtu atakae tufikisha mahala pakuona mwanga na faida ya rasiimali za zetu. Najua watu wengi mtaendelea kutukana au kusema wanao sema ukweli kuhusu huyu jamaa wamehongwa lkn TZ inahitaji mtu ambaye akikohoa wakuu wa mikoa wanaamka wanauliza tuwasaidieje wa TZ, wakuu wa wilaya wawatetemekee wa TZ wanao hitaji misaada ya serikali.
Ukweli ni taa hatakama ikombali utaiona, japo ni njiti ya kiberiti katikati ya giza la nchi yetu itaonekana Lowassa analifaa taifa letu na siyo CCM, porojo siyo ufanisi, najua Dr, anafaa zaidi lkn wakuu wa mikoa wameteuliwa na CCM kwahiyo Lowassa akisema wote wataogopa kz wataifanaya,
samahani kusema san lkn ukweli umenifanya kusema yote.

.............kwa Lowasa hakuna jingine mpaka urais !? na akikosekana yeye tutakuwa tumeharibikiwa ?
Bila shaka kuna "ghaibu" na wacha Mungu husema maneno yao kwa "kadiri"!
Hivi "mungu Israel" ni yupi huyo ?
 
Mi sielewi ni kitu gani kinashabikiwa hapa. Mungu haangalii mvi wala misuli. Yupo Rais wa 2015 ambaye wacha Mungu wanamwombea ili Mungu amfunue kama Daudi alivyojitokeza kuwa Mfalme wa Israel. Kapakwa mafuta tangu tumboni mwa mamaye. Mnajisumbua kupigishana kelele kwa majina ya watu kwa kuwa mnawajua tu. Mtashangaa, subirini.
 
Kaaaazi kweli kweli...!!! Hiki ni kikosi kazi maalum kilichotumwa kumsafisha E. L kwenye mitandao! Kweli pesa ni sabuni ya roho, na njaa mbaya jamani... Hivi mmelipwa bei gani nyie???
 
Namkubali kwa kusimamia msimamo wake,kuongeza mahudhurio Kanisani baada ya 2008 kuchapa kazi Na kuwa kwake siriazi na mwenye kujiamini. Ila simkubali kwa kukubali kutumika kwa maslahi ya ccm badala ya maslahi ya taifa. Kama alikubali kuficha siri za wizi wa bosi wake Hata yeye ni mwizi. Kumfadhili mwizi ni kushiriki wizi.
 
sasa tuambieni ni nani fisadi wa richmond ebu mwageni ukweli tujue na sisi,ili tujiunge kumsafisa E.L,vinginevyo tutaendelea kuamini hivyo, mpaka pale yeye E.L atakaposema ukweli.
 
Back
Top Bottom