dalili ya ukilaza kama werema
Sasa kipi unacho bisha hapo ? Mh Werema amesema wazi watu wenye utaalamu na elimu ya sheria ya katiba ni kama Dr. Mwakyembe, Prof. Palamagamba Kabudi na sio Prof. Shivji, yeye hakusomea sheria ya katiba. Sikiliza Bunge acha uchovu
Kama Werema angesema kuwa alizaa na mama yako na hivyo yeye ni baba yako mzazi ungekuja kukomaa hapaJF kuwa kasema kweli?
Mh. Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema, amempa somo Tundu Lissu kuwa bado ni mchanga kwenye sheria, kwani yeye anajua sheria za mazingira tu na hajui sheria za katiba. Kwa maana hiyo basi, ameseme yeye amejitolea kumfundisha Lissu sheria za katiba ili aweze kutafsiri vizuri katiba na kujua maana yake. Hii yaonyesha kumbe Lissu ni mchovu wa elimu ya sheria ya katiba. Kitu kama hukijui Mh. Lissu , sema hukijui kuliko kupotosha wananchi kwa maana siyo.
Sasa tunajuwa ni kwanini Prof Shivji hakuteuliwa kwenye Tume ya Warioba, wakubwa wanataka 'makada' na huyo Pof Kabudi ticks the box! Mkuchika naye baada ya kupenea chupuchupu ya re-shuffle anaonekana kupata nguvu ya kutetea serikali dhaifu. 48 years wanaulizwa faida za muungano wao wanakuja na ngonjera. Not any more.
Ni kweli Dume la Mbegu, ila AG naye mbona amewataja makada wa CCM tu na kumwacha Dk. S. Mvungi maana naye ni mtaalamu sana wa eneo hilo. Naona kama wakati mwingine AG Werema anakuwa kikada zaidi badala ya kuwa kitaaluma na kitaalamuMkuu kwenye fani ya sheria na wao wan a specialize kwenye specific areas tu na si kuwa kila mtu anajua kila kitu. Mh lissu yeye ni mtaalam wa sheria za mazingira na si mtaalam wa sheria za katiba. Magwiji wa utaalam wa sheria za katiba ni Dr mwakyembe na Pro palamagamba kabudi
Werema angekuwa anajua sheria za katiba angeleta ule uvundo bungeni yeye na Celina Kombani wake na kuuita muswada wa katiba mpya? Pamoja na kejeli zake wakati huo lakini siku 40 baadaye wabunge walikaa tena na kuufanyia marakebisho! Hatuna mwanasheria mkuu, tuna msanii mkuu!
Nimekupata Father Magobe, la umenikumbusha darasa la Logic. Thank U very muchHapa wewe ndiye unayeonesha uchovu wa elimu kwa maana ukisikia tu maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali basi unadhani ni kauli ya Mungu na ya wengine siyo sahihi. Hii ni 'reasoning' ya ajabu sana! Tafsiri ya sheria inazingatia mambo mengi sana na ndiyo maana wanasheria wanatofautiana na ni vizuri watofautiane. Kwani hujawahi kusikia wanasheria wanatofautiana - baadhi wanasema "adhabu ya kifo ni ya kikatiri ifutwe" na wengine wanasema ni "bado inafaa iendelee"? Hata majaji wenyewe wanatofautiana kutoa hukumu - wengine wanasema hivi na wengine vile. Hivyo, Mwanasheria Mkuu wa serikali kusema "Tindu Lissu ni mchanga wa sheria kwani yeye anajua sheria za mazingira tu na hajui katiba..." Ni errenous reasoning/falacy. Kwani ambao wanasaini mikataba mibovu kwa niaba ya serikali wanapata ushauri kutoka kwa nani? Serikali inapata ushauri wa kisheria kutoka kwa nani? Kama serikali imeweza kufanya madudu yote ambayo imeweza kuyafanya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayejua Katiba alikuwa wapi? Hii ni lugha tu inayotumiwa kuwakandamiza wabunge wenye maoni na mitazamo tofauti. Kama serikali na chama tawala hawataki maoni ya wengine kwa nini wanaleta bungeni hoja zijadiliwe na watalazimishaje wabunge wajadili au watoe maoni yanayofanana na ya kwao tu?
Mh. Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema, amempa somo Tundu Lissu kuwa bado ni mchanga kwenye sheria, kwani yeye anajua sheria za mazingira tu na hajui sheria za katiba. Kwa maana hiyo basi, ameseme yeye amejitolea kumfundisha Lissu sheria za katiba ili aweze kutafsiri vizuri katiba na kujua maana yake. Hii yaonyesha kumbe Lissu ni mchovu wa elimu ya sheria ya katiba. Kitu kama hukijui Mh. Lissu , sema hukijui kuliko kupotosha wananchi kwa maana siyo.