Werema hana lolote anachosema ni upotoshaji mtupu, anatetea maovu ambayo yamefanywa na serikali ya ccm, tangulini mtu kaambiwa ni mwizi na akakiri mimi mwizi, Tatizo la CCM hawataki kuelezwa ukweli, binaadamu asiye-accept ya wenzake huyo ni hatari sana, na mwisho wa siku ataishia pabaya. Lisu usivunjike moyo sisi watanzania tuko pamoja, ukweli wa mambo haya utajulikana siku si nyingi. Lisu Mungu akulinde Mungu akubariki, Werema Mungu aendelee kukupiga upofu. AMEN.
Mh. Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema, amempa somo Tundu Lissu kuwa bado ni mchanga kwenye sheria, kwani yeye anajua sheria za mazingira tu na hajui sheria za katiba. Kwa maana hiyo basi, ameseme yeye amejitolea kumfundisha Lissu sheria za katiba ili aweze kutafsiri vizuri katiba na kujua maana yake. Hii yaonyesha kumbe Lissu ni mchovu wa elimu ya sheria ya katiba. Kitu kama hukijui Mh. Lissu , sema hukijui kuliko kupotosha wananchi kwa maana siyo.