Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,104
- 26,070
- Thread starter
- #21
Tumeshajua mapungufu yake kwenye kujenga hoja!msingi wa mada hii,je hoja hizo na mapungufu yake yuko radhi kuzisimamie?Au leo nguruwe haramu kesho halalipia,kwa mila za kiafrika,kumnyima mtu chakula,hasa mgeni,huwa ni jambo la mwisho sana,hizi sababu za kusema kumpa mgeni chakula ni gharama,ni aibu kubwa sana kwetu kama taifa,bora tutunge sababu nyingine tu,
Hivi hao wageni wakila chakula saaana,watamaliza gunia tatu za mchele(kama laki nne hivi)
Hivi wakila sana watamaliza kuku mia tatu (kama laki sita hivi Tsh)
wakinywa sana,watamaliza vinywaji vya milioni 5?
yaani milioni kama ishirini kukirimu watu,kubadilishana mawazo na viongozi wa ndani na nje ni gharama? hata ikiwa milioni 50?
eti unawaambia mabalozi na wageni kama mzee mwinyi,leo hakuna kula! hivi kula kwao ni nini hasa kwa mtu kama balozi wa uingereza,marekani,canada,rwanda!
kweli kula nayo ni ishu!!!
unasema unabana matumizi watu wasile wakati viongozi wakuu na wakuu wa wilaya na mikoa wana vxx8 za milioni 300!!