Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,104
- 26,070
Sababu alizotoa Rais za kuahirisha shamra shamra za uhuru za mwaka jana na kuamuru usafi ni mbili:
1. Alikuwa na mwezi mmoja tu tokea ashike wadhifa wa urais
2. Gharama kuwa kubwa kufikia bil 4,ikwemo maandalizi,chakula na posho!Akasema alihoji kama watanzania wote wangenufaika na chakula hicho na posho,akaambiwa hapa na kuwa wanufaika ni waalikwa!Kwa mantiki hiyo akasema hapana,hakuna shamra shamra!
Naomba nijikite kwenye hoja namba 2!
- Ingawaje Rais alisema gharama za mwaka huu zimepungua hasa baada ya kufuta chakula,hakuweka wazi kuwa ni kiasi gani na kama posho pia zilifutwa!Sitaki kuamini kama posho zilitolewa maana alihoji mwaka jana kama posho zile watapata watanzani wote,alipoambiwa hapana akasema basi!
Wakati huo huo alisema shamra shamra zijazo na kuendelea zitafanyika Dodoma,hivyo kuonesha wazi kuwa sherehe zijazo zitakuwa na shamra shamra na maandalizi!Kwa mtazamo huu,ni wazi kuwa kama Rais atasimamia msingi wa kuahirisha shamra shamra za mwaka jana basi hakutakuwa na posho wala chakula kwa maana ya dhifa ya kitaifa unless kama watanzania wote watanufaika na hizo posho na chakula!
Hii inatoa tafsiri kuwa hata sherehe nyingine za kitaifa,si haki wachache kupata posho na chakula wakati watanzania wengine wanaangalia tu kupitia luninga!
Je,mheshimiwa Rais atayaishi maneno yake?
Note-: Ni vema kwa viongozi kuongea pale tu ambapo kuna cha kuongea na si kuongea kwasababu tu imekubidi kuongea!