Mh Rais Tuokoe Wakazi wa Kisarawe II Kigamboni.

hamisihamisi9

New Member
Jan 23, 2015
1
0
Mh Rais sina njia nyingine bora ya kuwasiliana na wewe zaidi ya hii niliyoipata, naandika barua hii nikiwa nyumbani sijaenda kazini kwani sioni tena hata faida ya kuendelea kufanya kazi. Naomba kukutaarifu tu kuwa eneo la kisarawe II kibada kigamboni, linatarajiwa kuchukuliwa na mwekezaji mchina kwa ajili ya kujenga makazi ya kisasa chini ya usimamizi wa Manispaa ya Temeke. Mimi kama mwanachi na mkazi wa Kisarawe II ninayependa maendeleo sina tatizo na huo mradi isipokuwa mbinu zinazotumika na Mkuu wa wilaya za ubabe, dhuluma, kinyonyaji na kidalali anazozifanya kuwasaidia wachina hawa kupora makazi yetu. Mh Rais rejea hotuba yako moja mwaka juzi ya tabia ya baadhi Halmashauri na Manispaa kupora ardhi kwa bei ya chini kwa wananchi na kuiuza kwa wawekezaji kwa bei ya juu.

Hicho ndicho kinachoenda kutokea kutokea kisarawe II mh Rais. Tumetangaziwa na Diwani kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya kuongea na uongozi wa serikali ya kijiji mtaa wa kichangani kuwa kuanzia April mwaka huu mradi huo unaanza na mwananchi atalipwa fidia ya ardhi tsh elfu kumi kwa square mita moja.

Fidia hii sit u ndogo bali ni ya dhuluma ukilinganisha na thamani ya maeneo tuliyopo na bei ya soko huria, na inatoa picha kuwa hata fidia ya nyumba na mali zetu kama mazao itakuwa ni ya ya dhuluma. Hayo yote ya mradi kuanza Mwezi April na kiwango cha malipo hatujashirikishwa mh Rais kama ambavyo Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya utwaaji ardhi kwa manufaa ya nchi na Sheria ya mipango miji. Mh Rais hii ni dhuluma inayofanyika chini ya utawala wako na tunaomba msaada wako. Kwa juhudi zako umefanikiwa kuboresha maisha ya wafanyakazi hasa idara ya Mahakama, mishahara toka umeingia madarakani imepanda kwa zaidi ya asilimia 200, na hii ndo imetuwezesha kununua ardhi na kufanikiwa kujenga nyumba, leo hii Mkuu wa wilaya anakuja anataka kuwapa wachina eneo tunaloishi kwa bei ambayo inatia dosari juhudi zako za kuhakikisha sisi wafanyakazi tuna maisha na makazi bora.

Mh Rais awali eneo tuliloambiwa kuwa limetengwa kwa ajili ya mwekezaji lilikuwa ni eneo linaloitwa Lingato, eneo hili ni pori kubwa linalopakana na mtaa wetu na lina ukubwa wa ekari zaidi ya 400, na wamiliki wake hawazidi hata 10. Ilikuwa ni rahisi sana kwa mradi huo kufanyika huko kwani sehemu kubwa ya eneo ni pori na wamiliki ni wachache, lakini ghafla Mkuu wa wilaya anasema hata eneo la makazi nalo litatwaliwa. Ok haina shida lakini kwa nini hatushirikishwi? kwa nini watwae ardhi kwa bei ya dhuluma?

Kwa nini tuambiwe kuwa mwezi wa nne tunatakiwa kuondoka wakati tuna watoto shule ambao wengine tumelipa ada mpaka za mwaka mzima na sisi sio sio wakimbizi wala wavamizi katika ardhi hii?Kwa nini kama mwekezaji anajenga makazi sisi tuondolewe?Kwa nn waache pori waje kwenye makazi? Mh Rais, mimi nimehamia makazi yangu mapya Jan 11 Mwaka huu, nimenunua kiwanja hiki mwaka 2012 baada kuhama maeneo ya uvumba tulipoambiwa kuwa eneo hilo linachukuliwa na mwekezaji, wakati hata fidia ya eneo la uvumba hatujalipwa karibu mwaka sasa, huku nako naambiwa nihame tena kwa fidia ya dhuluma!!!Kabla ya kununua eneo hili la Kisarawe II nilienda manispaa kuulizia kama eneo hilo liko kwenye mipango yoyote ya kutwaliwa, nilijibiwa kuwa eneo hilo ni la makazi ya kawaida na nikaoneshwa mchoro wa makazi uliokuwa umeandaliwa na Ifakara Health Institute, ndo ikafanya maamuzi ya kununua na kujenga eneo hili kulingana na mchoro wa manispaa, na hivi baadhi ya wenzangu wameshapimiwa na wana hati miliki. leo tena naambiwa nihame? Niende wapi Mh Rais?

Ardhi ndio rasilimali pekee niliyonayo,,niende wapi mimi leo? Tena kwa fidia kidogo ya kidalali kama hiyo?Hii nchi mbona mheshimwa watendaji wako wanatunyanyasa sana? Kwa nini tunaishi kwa hofu hivi kwenye nchi yetu wenyewe Mh Rais?Tuko jirani na Waziri Mkuu Pinda, ana eneo kubwa sana lkn eneo lake halijaguswa, wanakuja kwa walalahoi mwenye kiwanja cha hatua 20 kwa 20, kwa nn Mh Rais?Kuna maeneo ya wazi ya akina OilCom, Hamidu, Akiberali na Baghdad tajiri wa Dar es Salaam Zoo, maeneo yao hayajaguswa na ni mapori hayajajengwa na ni maelf ya ekari, lakini wanakuja kwetu
 
Mh Rais sina njia nyingine bora ya kuwasiliana na wewe zaidi ya hii niliyoipata, naandika barua hii nikiwa nyumbani sijaenda kazini kwani sioni tena hata faida ya kuendelea kufanya kazi. Naomba kukutaarifu tu kuwa eneo la kisarawe II kibada kigamboni, linatarajiwa kuchukuliwa na mwekezaji mchina kwa ajili ya kujenga makazi ya kisasa chini ya usimamizi wa Manispaa ya Temeke. Mimi kama mwanachi na mkazi wa Kisarawe II ninayependa maendeleo sina tatizo na huo mradi isipokuwa mbinu zinazotumika na Mkuu wa wilaya za ubabe, dhuluma, kinyonyaji na kidalali anazozifanya kuwasaidia wachina hawa kupora makazi yetu. Mh Rais rejea hotuba yako moja mwaka juzi ya tabia ya baadhi Halmashauri na Manispaa kupora ardhi kwa bei ya chini kwa wananchi na kuiuza kwa wawekezaji kwa bei ya juu. Hicho ndicho kinachoenda kutokea kutokea kisarawe II mh Rais. Tumetangaziwa na Diwani kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya kuongea na uongozi wa serikali ya kijiji mtaa wa kichangani kuwa kuanzia April mwaka huu mradi huo unaanza na mwananchi atalipwa fidia ya ardhi tsh elfu kumi kwa square mita moja. Fidia hii sit u ndogo bali ni ya dhuluma ukilinganisha na thamani ya maeneo tuliyopo na bei ya soko huria, na inatoa picha kuwa hata fidia ya nyumba na mali zetu kama mazao itakuwa ni ya ya dhuluma. Hayo yote ya mradi kuanza Mwezi April na kiwango cha malipo hatujashirikishwa mh Rais kama ambavyo Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya utwaaji ardhi kwa manufaa ya nchi na Sheria ya mipango miji. Mh Rais hii ni dhuluma inayofanyika chini ya utawala wako na tunaomba msaada wako. Kwa juhudi zako umefanikiwa kuboresha maisha ya wafanyakazi hasa idara ya Mahakama, mishahara toka umeingia madarakani imepanda kwa zaidi ya asilimia 200, na hii ndo imetuwezesha kununua ardhi na kufanikiwa kujenga nyumba, leo hii Mkuu wa wilaya anakuja anataka kuwapa wachina eneo tunaloishi kwa bei ambayo inatia dosari juhudi zako za kuhakikisha sisi wafanyakazi tuna maisha na makazi bora.
Mh Rais awali eneo tuliloambiwa kuwa limetengwa kwa ajili ya mwekezaji lilikuwa ni eneo linaloitwa Lingato, eneo hili ni pori kubwa linalopakana na mtaa wetu na lina ukubwa wa ekari zaidi ya 400, na wamiliki wake hawazidi hata 10. Ilikuwa ni rahisi sana kwa mradi huo kufanyika huko kwani sehemu kubwa ya eneo ni pori na wamiliki ni wachache, lakini ghafla Mkuu wa wilaya anasema hata eneo la makazi nalo litatwaliwa. Ok haina shida lakini kwa nini hatushirikishwi? kwa nini watwae ardhi kwa bei ya dhuluma? Kwa nini tuambiwe kuwa mwezi wa nne tunatakiwa kuondoka wakati tuna watoto shule ambao wengine tumelipa ada mpaka za mwaka mzima na sisi sio sio wakimbizi wala wavamizi katika ardhi hii?Kwa nini kama mwekezaji anajenga makazi sisi tuondolewe?Kwa nn waache pori waje kwenye makazi? Mh Rais, mimi nimehamia makazi yangu mapya Jan 11 Mwaka huu, nimenunua kiwanja hiki mwaka 2012 baada kuhama maeneo ya uvumba tulipoambiwa kuwa eneo hilo linachukuliwa na mwekezaji, wakati hata fidia ya eneo la uvumba hatujalipwa karibu mwaka sasa, huku nako naambiwa nihame tena kwa fidia ya dhuluma!!!Kabla ya kununua eneo hili la Kisarawe II nilienda manispaa kuulizia kama eneo hilo liko kwenye mipango yoyote ya kutwaliwa, nilijibiwa kuwa eneo hilo ni la makazi ya kawaida na nikaoneshwa mchoro wa makazi uliokuwa umeandaliwa na Ifakara Health Institute, ndo ikafanya maamuzi ya kununua na kujenga eneo hili kulingana na mchoro wa manispaa, na hivi baadhi ya wenzangu wameshapimiwa na wana hati miliki. leo tena naambiwa nihame? Niende wapi Mh Rais? Ardhi ndio rasilimali pekee niliyonayo,,niende wapi mimi leo? Tena kwa fidia kidogo ya kidalali kama hiyo?Hii nchi mbona mheshimwa watendaji wako wanatunyanyasa sana? Kwa nini tunaishi kwa hofu hivi kwenye nchi yetu wenyewe Mh Rais?Tuko jirani na Waziri Mkuu Pinda, ana eneo kubwa sana lkn eneo lake halijaguswa, wanakuja kwa walalahoi mwenye kiwanja cha hatua 20 kwa 20, kwa nn Mh Rais?Kuna maeneo ya wazi ya akina OilCom, Hamidu, Akiberali na Baghdad tajiri wa Dar es Salaam Zoo, maeneo yao hayajaguswa na ni mapori hayajajengwa na ni maelf ya ekari, lakini wanakuja kwetu ambako tayari tumeshajenga na tunakaa na familia zetu?kwa nn lakini Mh Rais?Kwa nn uporaji huu wa ardhi unafanywa na viongozi uliowateua Mh Rais?Sisi wakazi wa Kigamboni tumemkosea nini huyu Mkuu wa wilaya?Sasa hivi Mkuu wa wilaya ametuma watu wanapita kwenye makazi yetu kushawishi watu waukubali huu mradi na kutoa vitisho kuwa watakaokataa watabomolewa bila fidia. Hii ni haki kweli Mh Rais? Mh Rais, Tarehe 29 Jan 2015, siku ya alhamisi Mkuu wa wilaya ya Temeke anakuja hapa Kisarawe II eneo la hospitali kuongea na sisi rasmi, naomba mh Rais utume watu wako waje wasikilize ubabe, dhuluma na unyanayasaji wa huyu mteule wako ambaye amegeuka kuwa dalali wa wachina. Samahani sana kama nitakuwa nimeongea kwa lugha isiyofaa, nahitaji msaada wako Mh Rais, tamka neno moja tu mh Rais juu ya huu uporaji wa ardhi unaofanywa na viongozi hawa siyo Kigamboni tu bali hata nchi nzima, na Mungu atazidi kukubariki Mh Rais.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu ibariki Kigamboni
 
Hamidu city anauza viwanja kwa watu binafsi eneo hilohilo square mita moja elf 33...sasa hiyo ya elf 10 Mkuu wa wilaya kaitoa wapi???
 
Hataki usumbufu saivi anamalizia muda wake akapumzike msoga! Subirini rais toka UKAWA!
 
Mkuu mi nafikiri kuna mambo mengine yanafanyika Mh Rais hayuko well informed na saa zingine viongozi wa chini wanatoa taarifa za uongo,,,,Rais mwenyewe ameshasema Kigamboni hakuna mwananchi atakaye hamishwa, still sheria ya ardhi inataka kulipwa prompt and fair compesation,,hapa ni wanachi wenyewe wa Kigamboni kukomaa tu na kukataa hii dhuluma.
Hataki usumbufu saivi anamalizia muda wake akapumzike msoga! Subirini rais toka UKAWA!
 
Mwaka wa uchaguzi huu komaeni, pigeni kelele watakuja tu kuwasikiliza, bunge linaanza kesho waziri wa ardhi ni mpya tena mwanasheria mtupieni mzigo mbunge.komaeni na bei ya soko.
NB: Sorry nili-confuse Simbachawene na Lukuvi , Lukuvi ni moja ya mawaziri wa ovyo kabisa but komaeni tu.
 
Mh Rais sina njia nyingine bora ya kuwasiliana na wewe zaidi ya hii niliyoipata, naandika barua hii nikiwa nyumbani sijaenda kazini kwani sioni tena hata faida ya kuendelea kufanya kazi. Naomba kukutaarifu tu kuwa eneo la kisarawe II kibada kigamboni, linatarajiwa kuchukuliwa na mwekezaji mchina kwa ajili ya kujenga makazi ya kisasa chini ya usimamizi wa Manispaa ya Temeke. Mimi kama mwanachi na mkazi wa Kisarawe II ninayependa maendeleo sina tatizo na huo mradi isipokuwa mbinu zinazotumika na Mkuu wa wilaya za ubabe, dhuluma, kinyonyaji na kidalali anazozifanya kuwasaidia wachina hawa kupora makazi yetu. Mh Rais rejea hotuba yako moja mwaka juzi ya tabia ya baadhi Halmashauri na Manispaa kupora ardhi kwa bei ya chini kwa wananchi na kuiuza kwa wawekezaji kwa bei ya juu.

Hicho ndicho kinachoenda kutokea kutokea kisarawe II mh Rais. Tumetangaziwa na Diwani kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya kuongea na uongozi wa serikali ya kijiji mtaa wa kichangani kuwa kuanzia April mwaka huu mradi huo unaanza na mwananchi atalipwa fidia ya ardhi tsh elfu kumi kwa square mita moja.

Fidia hii sit u ndogo bali ni ya dhuluma ukilinganisha na thamani ya maeneo tuliyopo na bei ya soko huria, na inatoa picha kuwa hata fidia ya nyumba na mali zetu kama mazao itakuwa ni ya ya dhuluma. Hayo yote ya mradi kuanza Mwezi April na kiwango cha malipo hatujashirikishwa mh Rais kama ambavyo Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya utwaaji ardhi kwa manufaa ya nchi na Sheria ya mipango miji. Mh Rais hii ni dhuluma inayofanyika chini ya utawala wako na tunaomba msaada wako. Kwa juhudi zako umefanikiwa kuboresha maisha ya wafanyakazi hasa idara ya Mahakama, mishahara toka umeingia madarakani imepanda kwa zaidi ya asilimia 200, na hii ndo imetuwezesha kununua ardhi na kufanikiwa kujenga nyumba, leo hii Mkuu wa wilaya anakuja anataka kuwapa wachina eneo tunaloishi kwa bei ambayo inatia dosari juhudi zako za kuhakikisha sisi wafanyakazi tuna maisha na makazi bora.

Mh Rais awali eneo tuliloambiwa kuwa limetengwa kwa ajili ya mwekezaji lilikuwa ni eneo linaloitwa Lingato, eneo hili ni pori kubwa linalopakana na mtaa wetu na lina ukubwa wa ekari zaidi ya 400, na wamiliki wake hawazidi hata 10. Ilikuwa ni rahisi sana kwa mradi huo kufanyika huko kwani sehemu kubwa ya eneo ni pori na wamiliki ni wachache, lakini ghafla Mkuu wa wilaya anasema hata eneo la makazi nalo litatwaliwa. Ok haina shida lakini kwa nini hatushirikishwi? kwa nini watwae ardhi kwa bei ya dhuluma?

Kwa nini tuambiwe kuwa mwezi wa nne tunatakiwa kuondoka wakati tuna watoto shule ambao wengine tumelipa ada mpaka za mwaka mzima na sisi sio sio wakimbizi wala wavamizi katika ardhi hii?Kwa nini kama mwekezaji anajenga makazi sisi tuondolewe?Kwa nn waache pori waje kwenye makazi? Mh Rais, mimi nimehamia makazi yangu mapya Jan 11 Mwaka huu, nimenunua kiwanja hiki mwaka 2012 baada kuhama maeneo ya uvumba tulipoambiwa kuwa eneo hilo linachukuliwa na mwekezaji, wakati hata fidia ya eneo la uvumba hatujalipwa karibu mwaka sasa, huku nako naambiwa nihame tena kwa fidia ya dhuluma!!!Kabla ya kununua eneo hili la Kisarawe II nilienda manispaa kuulizia kama eneo hilo liko kwenye mipango yoyote ya kutwaliwa, nilijibiwa kuwa eneo hilo ni la makazi ya kawaida na nikaoneshwa mchoro wa makazi uliokuwa umeandaliwa na Ifakara Health Institute, ndo ikafanya maamuzi ya kununua na kujenga eneo hili kulingana na mchoro wa manispaa, na hivi baadhi ya wenzangu wameshapimiwa na wana hati miliki. leo tena naambiwa nihame? Niende wapi Mh Rais?

Ardhi ndio rasilimali pekee niliyonayo,,niende wapi mimi leo? Tena kwa fidia kidogo ya kidalali kama hiyo?Hii nchi mbona mheshimwa watendaji wako wanatunyanyasa sana? Kwa nini tunaishi kwa hofu hivi kwenye nchi yetu wenyewe Mh Rais?Tuko jirani na Waziri Mkuu Pinda, ana eneo kubwa sana lkn eneo lake halijaguswa, wanakuja kwa walalahoi mwenye kiwanja cha hatua 20 kwa 20, kwa nn Mh Rais?Kuna maeneo ya wazi ya akina OilCom, Hamidu, Akiberali na Baghdad tajiri wa Dar es Salaam Zoo, maeneo yao hayajaguswa na ni mapori hayajajengwa na ni maelf ya ekari, lakini wanakuja kwetu

labda atakusaidia lakini sisi kina gogo la shamba tunawasiwasi wa wewe kupata msaada maana walioiba mapesa mengi ya wananchi mpaka sasa wanapeta mitaani
 
madalali hapo ni Mkuu wa wilaya,diwani wa ccm na wenyeviti serikali za mtaa za mtaa wanatokea chadema. Mwenyekiti wa wa serikali anatoka chadema akishirikiana na diwani wa ccm wa eneo hilo waliishapiga dili na dawasco wakapata mamilioni ya pesa sasa wamekolea wanapiga udalali kwa mwekezaji wa kichina wanawahadaa wananchi sq mita Tsh 10 000 huku kwenye vitabu wanaandika Tsh 80 000. Msikubali wakikaribia eneo hilo wapigeni mawe. Hivi muwekezaji lazima apewe maeneo yenye watu tayari,si waende maporini huko wakaanzishe miji. Wanasiasa wa Tz wote baba moja mama moja ni waizi. Wanawahi maana 2015 mtikisiko mkubwa hivyo Chukua Chako Mapema ( CCM )
 
Back
Top Bottom