Waananchi wa Visegese, Kisarawe wamtaka Makonda aende kutatua mgogoro ulioko kati Yao na Halmashauri ya kisarawe

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,214
4,623
Waananchi wa Visegese, Kisarawe wamtaka katibu Mwenezi wa CCM Makonda aende kutatua mgogoro ulioko kati Yao na Halmashauri ya Kisarawe

Mgogoro huo unatokana na makubaliano waliyokubaliana na Halmashauri Kwa ajili ya wanakijiji kutoa eneo lao lichukuliwe Kwa ajili ya uwrkezaji wa viwanda
Ni miaka 10 Sasa hakuna kinachoendelea zaidi ya porojo tu zisizoisha za viongozi wa Halmashauri hiyo

Katika kikao kilichofanyika siku ya jumanosi tarehe 18 mwezi huu wa 11, 2023 wanachi waliomba Mheshimiwa Makonda aende akaongee na mamia ya wananchi waliotoa ardhi Yao Kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda Kwa moyo mweupe wakiunga mkono juhudi ya serikali ya Tanzania ya viwanda na kuruhusu Kwa roho nyeupe bila mgogoro ardhi Ichukuliwe ili na eneo la Kisarawe nalo lifurike viwanda

Shirika kama Tanesco wametoa ushirikiano mkubwa mno kuhakikisha eneo Hilo linakuwa na umeme na ulishawekwa tayari umeme mkubwa wa kuhimili viwanda

Shida Iko kwenye uongozi Halmashauri ya Kisarawe

Mheshimiwa Makonda unasubiriwa kule Visegese, Kisarawe.

Wananchi wanakungoja Kwa hamu wanaamini ukiwa kiongozi juu wa CCM waweza saidia kutatua hili
 
Back
Top Bottom