Mh. Rais, sasa ni zamu ya watumishi wako

pemgtoonet.com

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
880
618
Kwa nyakati tofauti, tumeshuhudia upendo wa Mh. Rais kwa wananchi wake akiwazawadia mihela kama yote.

Kila ziara amekuwa akigawa pesa kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiuchumi.

Mfano, ni pale muhimbili aliwasaidia wahanga wa moto laki 5 kila mmoja.

Madaktari na nesi pia aliwapa chochote.

Pia kila ziara amemwaga pesa, Tanzania ni nchi tajiri kama asemavyo yeye.

Sasa ni zamu ya watumishi wa umma wote kuboreshewa mishahara yao. Maana toka 2015, waliorekebishiwa madaraja hata robo hawafiki.

Wengi wamepewa barua tu za kupanda madaraja, ila no. Mabadiliko ktk mishahara yao.

Pia, kuhusu kubadili muundo wa salary bado kimya, au wangoje hadi Yesu arudi kwa mara ya 2?

Rais wetu inaonekana una huruma sana, basi hiyo huruma pia iwafikie na wanao ambao ni watumishi wa umma.

Wanalia sana huku mtaani pia wanadharauliwa kinyama.

Wape furaha ya kweli watumishi wako.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.

#ova
 
Mwaka kesho mishahara itapanda kwa 50% ,baada ya ujenzi na kupindua meza ya uchaguzi mapema ,kura za wafanyakazi na families zao ni muhimu na bila kuongeza mishahara ngoma itakuwa ngumu
 
Kwa nyakati tofauti, tumeshuhudia upendo wa Mh. Rais kwa wananchi wake akiwazawadia mihela kama yote.
Kila ziara amekuwa akigawa pesa kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiuchumi.
Mfano, ni pale muhimbili aliwasaidia wahanga wa moto laki 5 kila mmoja.
Madaktari na nesi pia aliwapa chochote.
Pia kila ziara amemwaga pesa, Tanzania ni nchi tajiri kama asemavyo yeye.
Sasa ni zamu ya watumishi wa umma wote kuboreshewa mishahara yao. Maana toka 2015, waliorekebishiwa madaraja hata robo hawafiki.
Wengi wamepewa barua tu za kupanda madaraja, ila no. Mabadiliko ktk mishahara yao.
Pia, kuhusu kubadili muundo wa salary bado kimya, au wangoje hadi Yesu arudi kwa mara ya 2?
Rais wetu inaonekana una huruma sana, basi hiyo huruma pia iwafikie na wanao ambao ni watumishi wa umma.
Wanalia sana huku mtaani pia wanadharauliwa kinyama.
Wape furaha ya kweli watumishi wako.
Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.

#ova
Hiyo haipo..
 
Hii picha inaeleza
IMG-20191018-WA0023.jpeg
 
Back
Top Bottom