Mh. Pinda alazimika kutumia PIPOZIII...POWER kumaliza hotuba yake

Mnafikiri waziri mkuu ni wa kuwatumikia CCM pekee? Kweli Tanzania tuna safari ndefu sana.
 
mkuu hebu tudadavulie vizuri nimeishughulisha akili yangu nilichokiona labda ni ni umri wa wabunge husika i.e Mbeya,Mz na Musoma zaidi ya hapo cjaambulia kitu

Mkuu maeneo mapya ya upinzani kama Mwanza, Mbeya, Shinyanga, n.k. ni sehemu ambazo watu wake wameteswa na kufukarishwa na CCM kwa kila namna na kwa muda mrefu. Ni hivi karibuni wameanza kuonja matunda ya siasa za upinzani hivyo kuwapelekea wanasiasa wa CCM ni kama kutonesha kidonda kilichoanza kupona; lazima wapige kelele. Ni sawa na kutokewa na jinamizi usingizini lazima utapiga mayowe.

Kwa maeneo walikozoea upinzani kwa muda mrefu, kiongozi yeyote wa CCM anaonekana kama kituko tu na hupuuzwa kistaarabu kwani mara nyingi hawana jipya; na ndivyo ilivyo huko Moshi au Pemba.
 
Ukweli husemwa:

Waziri alikuwa na ratiba ya kuhutubia wananchi viwanja vya Sahara, katika kuhutubia kwake, maneno yote ya chama chake hayakupokelewa na wananchi walikusanyika kumsikiliza, ilimbidi atumie maneno ya CHADEMA kumaliza hotuba yake.

CCM OYEE......watu kimya, PIPOZIII......power tena kwa shangwe kubwa.

Na ilikuwa ajbu pale Wenje alipotaka kuhutubia kwani alifikishwa jukwani kwa kubebwa.

Waziri Mizengo Pinda hawezi kusema maneno ya chama wakati yuko kazi kiserikali kama Waziri Mkuu. Na huo haukuwa mkutano wa chama bali wa wananchi ambao siyo wa vyama vya CCM na CHADEMA pekee. Watanzania bana, kwa sasa kila kitu ni siasa.

Tuacheni majungu ya kisiasa.
 
Ukweli sasa unaanza kuwa wazi sana, siku za usoni mambo haya yanayo fanywa na CCM na kushbikiwa na wakina zombe yataanddikwa kwenye vitabu mashuleni, ili kuweka kumbukumbu, kama tunavyo soma habari za wakoloni.. sasa ole wako chagua upande wa haki ili usi aibike milele kwa hakuna uwezacho kumficha Mungu. uchafu wote juu ya waliyo fanyiwa akina Mwangosi, ilimboka.. na mashujaa wengu tu waliyo hai na waliyo kufa. itakuwa ni aibu kwa vizazi na vizazi kwa watu waliyo husika na damu sizizo na kosa. tatizo tu ni kusema ukweli. KOSA KUBWA INLOLIFANYA SISIEMU NI KUMALIZA MATATIZO YA WATU KWA KUWAZIBA MIDOM, LAKINI MIMI NAFANANISHA NA TABIA HII NA SAWA NA KUFAGIA CHUMBA KISHA UCHAFU UKAUFICHA CHINI YA KITANDA. SIKU UKIANZA KUOZA HARUFU MBAYA ITAKUUMBUA[/SIZE][/FONT]
 
kwa hali hii inaonesha,bora kukifuta CCM,watz watakuchukulia poa kuliko CDM.
 
Anaye hisi kuwa ni propaganda pole sana, watu ndivyo walivyofanya jana kwa pm wetu.
 
Hapo mtoto wa mkulima kaupata ujumbe na kujua Chadema ikoje moyoni mwa watanzania wa sasa, na atatoa taarifa murua kwa magamba wenzake
Haya yote wanayajua yeye na wenzake tangu wakati wa uchaguzi wa 2010
 
Hizo ni habari za uongo, Mimi nilikuwepo haikuwa hivyo wewe Mwongo, cdm ni kweli mwz,Arusha,mby na shinyanga Lakini sehemu wanaokoteza tu. Poleni viongozi wa cdm.slaa na mbowe.
 
Binafsi nimesikiliza marudio ya hotuba hiyo kupitia Metro FM leo asubuhi nikasikia jinsi hotuba hiyo ilvyokuwa inaingiliwa na vibwagizo vya Wenje Wenje mpka pm akaomba utulivu haikusaidia akaingia mkuu wa wlaya haikufua dafu akaja mkuu wa mkoa bado mambo yakawa magumu ikabidi kuikatiza hotuba kabla ya muda wake pamoja na pm kurusha madongo kwa cdm ameondoka na picha halisi kuwa Mwanza sio Dodoma

wanabahati hakuna aliyejipanga kuchukua matukio katika ziara hiyo kwa kuamini hakuna jipya litakalojitokeza. kwani hadi narusha uzi huu, nimehangaika sana kuitafuta taarifa hii kwenye media zetu bila mafanikio. Mwisho nimejiuliza, Mwanza hukuna watumiaji wa JF? Ndipo nilipoamua kuirusha just kuwataarifu wadau wa kupashana habari juu ya suala hili.

Ubarikiwe mkuu kwa kutoa source ya info kuwa umesikia metro FM, 99.4
 
Hawa wazee wanafanya kazi katika mazingira magumu kweli kweli, hivi hakulia kweli?
 
Dah chagulani namuonea huruma cdm tusamehe huyu dogo.
Nakubaliana nawe, Chagulani anasameheka; alikengeuka na kuchafua mambo lakini ni kijana mzuri aliyetumia haki yake ya msingi ya kukosea na kujifunza kutokana na makosa yake. CDM please msameheni huyu dogo; yuko vizuri na ataendelea kujifunza!
 
Mizengwe Pinda kiguu na njia anazunguka na mikasi mkononi,mwenge nao unazunguka wanakula kodi zetu bila huruma,hivi hawa ccm ni laana gani wanayo?hakika wana mwanza nawashukuru kwa hilo na kuonyesha yaliyo moyoni mwenu na hakika chini ya haya magamba tutashuhudia upuuzi kama huu wa ifujaji wa pesa zetu.
ongezea kuwaambia kwamba wazidi kuiwaza kaskazini na uwasisitizie kwamba mwanza nayo ni kaskazini maana wana macho lakini hawaoni.peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees.
 
wanabahati hakuna aliyejipanga kuchukua matukio katika ziara hiyo kwa kuamini hakuna jipya litakalojitokeza. kwani hadi narusha uzi huu, nimehangaika sana kuitafuta taarifa hii kwenye media zetu bila mafanikio. Mwisho nimejiuliza, Mwanza hukuna watumiaji wa JF? Ndipo nilipoamua kuirusha just kuwataarifu wadau wa kupashana habari juu ya suala hili.

Ubarikiwe mkuu kwa kutoa source ya info kuwa umesikia metro FM, 99.4
kaka tanzania daima wameiandika japo sio kwa undani.
 
Binafsi nimesikiliza marudio ya hotuba hiyo kupitia Metro FM leo asubuhi nikasikia jinsi hotuba hiyo ilvyokuwa inaingiliwa na vibwagizo vya Wenje Wenje mpka pm akaomba utulivu haikusaidia akaingia mkuu wa wlaya haikufua dafu akaja mkuu wa mkoa bado mambo yakawa magumu ikabidi kuikatiza hotuba kabla ya muda wake pamoja na pm kurusha madongo kwa cdm ameondoka na picha halisi kuwa Mwanza sio Dodoma

kwa tuliosikia kupitia metro fm leo asubuhi hakika ccm imechokwa mwanza.hali ilikuwa ni mbaya kwa waziri mkuu ilibidi mkuu wa mkoa aingilie kati kuwatuliza wananchi kwa wamechoshwa na propaganda za ccm
 
Mkuu, jibu la hilo lipo wazi, hawaelewi wakikaa ofisini wafanye nini, kwasababu ofisini kuna kazi nyingi while wao hawazioni then wanajikuta hawana cha kufanya hence wanakua bored halafu wanasinzia.

Ili kutoa usingizi bora waende safari kama hizo, baadhi ya mizigo ya safari ndo hiyo mikasi, Nina maana ya mikasi hii ya kukatia sio mikasi ile ya vijana.

Waziri wetu mkuu hana ubaya na mtu, it is just that he is not revolutionary...was never one! Sasa msimtuhumu sana kwa kile kinachoendela. He is a naive leader who just do things with a flow.
Oh, bye the way, Umenichekesha sana na kauli yako hapo ili watu wasije kuku-quote vibaya!
 
If you can not fight them join them....Pinda with ur gov ur not late
 
Ngoma unapiga mwenyewe, kuimba uimbe mwenyewe na kucheza pia ucheze mwenyewe, khaa!? Chadema bana!!?
Hivi cdm mna lipi la kuwaeleza wa-tz 2015? Au ni hayo mayowe ya ukombozi wa nchi iliyo huru?


umeuliza vizuri ila umemalizia vibaya. uhuru una mapana yake ambayo ukiyachanganua na kufananisha na nchi husika utagundia kiwango cha uhuru uliopo. nchi kujitawala yenyewe haimanishi kwamba ipo huru kwasababu hali hiyo inaweza kuwa uhuru wa bendera ili hali huwezi kufanya maamuzi yako mwenyewe. kwa wananchi uhuru ni kufanya mambo yao ya kila siku kwa mujibu wa sheria ambazo hazina vizuizi kandamizi, kwa mfano haki ya kuandamana haiitaji kibali bali matakwa ya wananchi pale wanapoona inabidi kufanya hivyo
 
Hamna kitu hapo. Hao ni wavuta bangi waliokusanywa na kulipwa na Wenje ili kumfanyia fujo waziri mkuu. Watu wenye heshima zao walikuwa kimya wakishuhudia vibaka wakitekeleza maagizo ya Wenje. Subiri kura halisi Uje uone.
 
Back
Top Bottom