Mh. Pinda alazimika kutumia PIPOZIII...POWER kumaliza hotuba yake

umeuliza vizuri ila umemalizia vibaya. uhuru una mapana yake ambayo ukiyachanganua na kufananisha na nchi husika utagundia kiwango cha uhuru uliopo. nchi kujitawala yenyewe haimanishi kwamba ipo huru kwasababu hali hiyo inaweza kuwa uhuru wa bendera ili hali huwezi kufanya maamuzi yako mwenyewe. kwa wananchi uhuru ni kufanya mambo yao ya kila siku kwa mujibu wa sheria ambazo hazina vizuizi kandamizi, kwa mfano haki ya kuandamana haiitaji kibali bali matakwa ya wananchi pale wanapoona inabidi kufanya hivyo

Kwahiyo maendeleo ya nchi kwako ni maandamano ya toka uchaguzi hadi uchaguzi yanayosababisha mauaji kwa watanzania sio??
Watanzania wanahitaji sera zenye kuleta maendeleo kwao na sio kutangaza siasa za chuki na maandamano ya kila siku yasiokuwa na tija, badala yake kusababisha mauaji ya watanzania wasio na hatia. Au wewe unafaidika na vifo vya watanzania nini, kwamba akiuliwa mtanzania na polisi kwako ni nafasi ya kujizolea umaarufu kwa kuishutumu serikali!!!!
I don't understant u guys taking "pipoz powa"!
 
eti wanasema kuwa waliokuwa wakizomea walinunuliwa viroba ili wamzomee mtoto wa mkulima , ila wanasahau kuwa hao hao wanaowaita wavuta bangi na wanywa viroba ndio walimwondoa masha,ccm,nyamagana na ndio wataiondoa ccm ikulu 2015.
 
mmeacha sema Kilimanjaro?mlikwenda pia na arusha,baadaye mbeya, baadaye sijui mtasema dar kwa vile napo wana ushawishi mnono.soon moro,bila kusahau iringa walipobidi muua mwangonja.
na avatar yako ina picha ya mwana chadema alafu unaponda kimoyomoyo tehetehetehetehe poke mkuu
 
Najaribu ku-imitate sasa Pinda alivyokuwa ansema huku moyoni anawatukana....Pipoz.... naamini hajarudia mara mbili
 
ongezea kuwaambia kwamba wazidi kuiwaza kaskazini na uwasisitizie kwamba mwanza nayo ni kaskazini maana wana macho lakini hawaoni.peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees.
Ukiwa gamba inabidi uwe chizi hata kama huokoti makopo,nadhani safari hii hata mtwara na songea watasema ni kaskazini.....wanalo na laana yao mkuu.
 
Ukweli husemwa:



Waziri Mizengo Pinda hawezi kusema maneno ya chama wakati yuko kazi kiserikali kama Waziri Mkuu. Na huo haukuwa mkutano wa chama bali wa wananchi ambao siyo wa vyama vya CCM na CHADEMA pekee. Watanzania bana, kwa sasa kila kitu ni siasa.

Tuacheni majungu ya kisiasa.

Na wewe nae shugulisha akili yako pia, kama ni mkutano wa serikali why aseme ccm oyeee, akili zingine bana
 
Hapo PM anapoligharimu Taifa kwa msururu wa misafara yake ndipo palikotia nyongo furaha yangu.

Hivi kama hii nchi ni ya amani kweli kama wanavyosema CCM, je ni kwanini basi viongozi wao/serikali wasiwe na misafara midogo na tena yenye askari/walinzi wachache tu? Utakuta msafara una askari zaidi ya 100, magari ya usalama zaaidi ya 8, bado magari ya halmashauri, mikoa, na serikali kuu nk jumla utakuta zaidi ya magari 25.

Heche alisema hivi, namnukuu "....utakuta waziri mzima ametoka Dar na msafara wake wanakwenda Rukwa kuzindua mradi. Sasa waziri na msafara wake wanatumia shs milioni 80, au 100.....halafu mradi wenyewe wanaoenda kuuzindua ni wa milioni 4, au ni jengo la darasa ambalo halizidi milioni 20! Mkifanya mchezo watawauza na ninyi wananchi ili walipie matanuzi yao. Mshukuruni Mungu CHADEMA ipo inayapigia kelele...vinginevyo hawa jamaa wangekuwa wameshawauza..."

Huu ni ubadhirifu uliohalalishwa lakini lazima tuushughilikie, muda ni sasa.
 
Weka Audio na sisi tusikilize kama alikuja kwenye ziara ya serikali CCM hoyee ilitoka wapi? na Pipooooz power ilitoka wapi?

Bado sijakuelewa labda nisikilize mimi mwenyewe audio.

Ukweli ni kuwa kulikuwa fujo, hata mawe yalirushwa....kwa ujumla hali haikuwa shwari
 
CCM ni Wastaarabu na ndiyo maana wanaheshimika hata ugenini na wana sera siyo matusi wawapo majukwaani tofauti na CDM na vurugu, kukosa sera na matusi majukwaani.

Ni mikutano ipi hiyo ya ccm ambayo unaisemea umesahau ya mwigulu na kibajaji kule meru au kutoleana silaha kwenye mikutano ya ndani ndio ustaarabu unaosema?
 
hapo pm anapoligharimu taifa kwa msururu wa misafara yake ndipo palikotia nyongo furaha yangu.

Hivi kama hii nchi ni ya amani kweli kama wanavyosema ccm, je ni kwanini basi viongozi wao/serikali wasiwe na misafara midogo na tena yenye askari/walinzi wachache tu? Utakuta msafara una askari zaidi ya 100, magari ya usalama zaaidi ya 8, bado magari ya halmashauri, mikoa, na serikali kuu nk jumla utakuta zaidi ya magari 25.

Heche alisema hivi, namnukuu "....utakuta waziri mzima ametoka dar na msafara wake wanakwenda rukwa kuzindua mradi. Sasa waziri na msafara wake wanatumia shs milioni 80, au 100.....halafu mradi wenyewe wanaoenda kuuzindua ni wa milioni 4, au ni jengo la darasa ambalo halizidi milioni 20! Mkifanya mchezo watawauza na ninyi wananchi ili walipie matanuzi yao. Mshukuruni mungu chadema ipo inayapigia kelele...vinginevyo hawa jamaa wangekuwa wameshawauza..."

huu ni ubadhirifu uliohalalishwa lakini lazima tuushughilikie, muda ni sasa.

wengine hawatakuelewa, watasema ni protocal. Mh. Msigwa aliwahi kulitibua bungeni kuwa msafara wa pinda iringa ulikuwa na magari 26, serikali iltaka kubisha, sijui walimalizaje. Sasa kwa hapa mwanza, magari yalikuwa kama 24, wote walipewa walipewa allowances, kila siku wanasign lita 150 za mafuta, hakuna anayejali zimeisha au bado zipo. Ukipiga hesabu ni pesa ndefu mno
 
Leo ukiamua kubweka haitakufanya uwe mbwa.....na siyo kila kilicho na mbawa na kuruka ni ndege vingine ni mapopo.
 
Deep down his heart,anajuwa ile kauli yake ya "liwalo na liwe",ndo ilipelekea polisi kujichukulia sheria mkononi na kufanya mauwaji.Sasa anachofanya ni unafiki tu.
 
Back
Top Bottom