Mgongano wa hoja: Ndoa za matajiri zina furaha na hudumu kuliko za maskini!

mmmmh ama kweli duniani kuna mambo, money cant buy hapiness but ila hela inachangia sana kwenye ndoa kwani unakuta asilimia kubwa ya watu wengine anajilazimisha kuolewa na mtu kisa pesa mengine yatajulikana mbele ya safari
 
Wakuolewa huwa wanatafuta security. Zamani kuolewa na mwanaume shujaa, mfalme ilkuwa mpango. Leo security ipo kwenye pesa so mtu anachagua kucompromise personal wishes ambazo huleta furaha ili apate security. then money become the basic factor to keep the marriage with or without happiness.
 
Mi nilidhani upole ndo mpango daa sioi hadi niwe na hammer aisee ila wanawake mnakosea sana kutubagua sisi maboy maskini sikieni kilio chetu jamani
 
Nilikuwa nasoma jarida la "Vanity Fair" la mwezi huu unaokuja. Lina makala moja inaelezea jinsi matajiri walio na majumba yenye thamani za makumi ya mamilioni ya dola za Kimarekani fukweni huko Malibu California (Hollywood stars mostly) na Nantucket Massachusetts (Northeast brahmins and bluebloods) wanavyopata matatizo baada ya majumba yao ya fukweni kuanza kufikiwa na bahari baada ya "beach erosion" ambayo itafanya pale Ocean Road paonekane mchezo wa kitoto.

Hata matajiri wana matstizo yao, pesa hazinunui kila kitu.

Wengine wanasema "More money, more problems" kama B.I.G.

Hook.

I don't know, what they want from me.
It's like the more money we come across, the more problems we see
 
Nilikuwa nasoma jarida la "Vanity Fair" la mwezi huu unaokuja. Lina makala moja inaelezea jinsi matajiri walio na majumba yenye thamani za makumi ya mamilioni ya dola za Kimarekani fukweni huko Malibu California (Hollywood stars mostly) na Nantucket Massachusetts (Northeast brahmins and bluebloods) wanavyopata matatizo baada ya majumba yao ya fukweni kuanza kufikiwa na bahari baada ya "beach erosion" ambayo itafanya pale Ocean Road paonekane mchezo wa kitoto.

Hata matajiri wana matstizo yao, pesa hazinunui kila kitu.

Wengine wanasema "More money, more problems" kama B.I.G.

Hook.

Hao wanaoitwa 'Brahimins na Bluebloods'
ni sawa sawa na wale wanaoitwa 'old money' ?
 
We ukiwa tajiri utamtimua mumeo?

No.. Lkn reality ni kwamba wanaume wengi wanapenda wao ndio wawe 'breadwinners' na hivyo mwanamke akiwa tajiri au wote wawili, huwa receipe for disaster (mwanamume labda hatajiamini na wote wakiwa 'moneybags' hamna atakayeweza kujishusha). Ndo maana 'hollywood' ndoa hazidumu na wkti mwingi ni show. Hata hapa kuna mifano hai ya rich couples that never lasted.

Hata hivyo pale ambapo uaminifu zero, maskini au tajiri ndoa huvunjika. Kutodumu kwa ndoa sio lazima talaka...
 
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!

Nawakaribisha wadau kwenye mgongano wa Hoja, na mchango wako uongozwe na nguvu ya hoja juu ya hii mada!

Sheria!

Ni marfuku kumshambulia/kumjadili mtoa hoja bali hoja yake!

Matusi hayaruhusiwi! Swaumu kali saa hizi.

Mjadala huru yeyote anaweza kuchangia.


Mimi Naunga mkono hoja 100% sio tu kiushabiki maandazi bali kwa Hoja nzito zifuatazo.

1. FACT. Furaha hainunuliwi ila pia furaha haiji hivi hivi! Vya kufurahisha vina gharama yake.

2. FACT. Money brings peace, and ateasy. Hulazimiki kufanya maamuzi magumu kamakujiuza upate ada ya mwanao.

3. FACT. Mtazamo wa jamii juu yako (Peer pressure) unaweza kukunyima raha na kukushawishi uriconside maamuzi yako kama choice ya mume.

4. FACT. Money is a powerful Motivation to Stay! Hata kama huna raha kuacha ghorofa si mchezo mjue.

4. THEORY. Wanaume wengi hawajatulia. Sasa kuishi na mtu hajatulia na hana kitu inataka moyo mjue.

4. STATISTICS. Ndoa nyingi zinavunjika mume akifukukzwa kazi au kufilisika.

KARIBUNI KWA HOJA ZENU!

Mfanyabiashara tajiri wa madini Arusha anusurika kuuawa na mkewe wa ndoa ili arithi mali!! Pia huyo mkewe alipanga kuua mtoto wa kufikia wa mumewe!! Where did love go despite their wealth?? MORE MONEY, MORE PROBLEMS!!?
 
money can buy happines
money can buy peace
money can buy freedom
money can buy anything.
even money can buy a happy marriage.

But with all your money you just die as cockroaches do!!! Why not stop death using your money?
 
2. FACT. Money brings peace, and ateasy. Hulazimiki kufanya maamuzi magumu kamakujiuza upate ada ya mwanao.

4. FACT. Money is a powerful Motivation to Stay! Hata kama huna raha kuacha ghorofa si mchezo mjue.

5. THEORY. Wanaume wengi hawajatulia. Sasa kuishi na mtu hajatulia na hana kitu inataka moyo mjue.

6. STATISTICS. Ndoa nyingi zinavunjika mume akifukukzwa kazi au kufilisika.


Napinga maudhui ya hoja, kwa sababu zifuatazo:

2. Pesa ni kitu cha msingi, sote tunakiri but, we all live under the similar sense of fear katika maisha yetu...kama ni ofisini unaogopa kuharibu kazi ili usifukuzwe, kama ni kiimani unaogopa kufanya dhambi waziwazi ili usitengwe na waumini wenzako...WE ARE ALL SINNERS...hivyo tusijadili hili kinafiki.

Kama ilivyo ofisini kwa yule mfanyakazi mwenye miradi yake iliyosimama vizuri...most of the times huwa overconfident...na sote tunajua madhara ya kuwa-overconfident. Kama ilivyo ofisini and elsewhere, ndivyo itakavyokuwa hata kwenye ndoa. PESA huzaa kiburi...pesa huondoa that sense of fear...hujenga kiburi kwa upande wowote, iwe mume au mke..hapo ndipo shida huanza.

In other words, i can argue that money does not bring harmony, infact harmony and money are incompatible to one another, the earlier leave the house when the later comes in, sometimes via the window or crosspass at the doorstep

4.Motivation to stay kwenye ndoa inategemea malezi ya mwanandoa tangu utoto wake .....na hasa nini anaamini kwenye dhana nzima ya marriage institution...siyo fedha...hata kidogo

5. Wanaume wengi hawajatulia??!! where do you get that??...according to takwimu zipi?...naomba source...what if i say wanaume wengi wametulia...will you dispute...hiyo hoja bado haiwezi kuwa moja ya hadidu za rejea kwa mdahalo huu...unless you provide the source of your argument

6. Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na wandoa wenyewe kutojua thamani ya ndoa...ndoa huwezi kuithaminisha na kiasi cha fedha walichonacho wanandoa...mara nyingi ndoa huvunjika kutokana na tofauti ambazo ni unresolved for very long time kati ya w
anandoa ... na mengine ambayo mimi na wewe hatuyafikirii at the moment...

Ndoa is full of surprises my dear...hii kitu ni ya ajabu sana... believe me... i have seen this first hand and you know what ...ndoa ni subject ngumu sana kudraw conclusion on its stability


Naomba kutoa hoja
 
wengi mtakataa lakin kwa vile hamna na mnataka kujifariji. pesa ndio kila kitu kwenye ndoa. pata picha shopping dubai.holiday united states. kutengeneza kucha paris. check up german kwa nin ndoa isidumu.

lakin ndoa za kimasikin kwanza mwanaume anajijua kuhudumia shida hivo anakuwa na wivu sana anais anaibiwa.

vurugu kila siku mara tumechoka matembele. pesa ndio kila kitu.

nasema hivo kwa uzoefu wengine toka tukiwa watoto full masafari kila siku mara japan.hongkong.states.german. china. sweden etc kwa nin family isiwe na furaha! !!!!


Mimi naishi uswahilini, ikitokea siku sijapokea simu yako...unapelekwa regency na kuwekwa mapumziko....

Furthermore, cha kusikitisha au kufurahisha ni kwamba unapelekwa kutengeneza kucha paris na bado unakuja uswahilini kunipatia pesa in terms of millions as a grant kwa matumizi yangu madogo madogo...

 
furaha inaweza isiwepo kote kote, we unadhani maskini wanafuraha? ni kwamba wanavumilia tu sawa na yule anayeweza kuvumilia kero za wenye nazo

Ni kweli, furaha unaweza usiipate hata ukiwa tajiri kiasi gani, kwenye ndoa kuna matatizo ya kila aina, cha muhimu uvumilivu tu
 
Back
Top Bottom