Mgongano wa hoja: Ndoa za matajiri zina furaha na hudumu kuliko za maskini!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!

Nawakaribisha wadau kwenye mgongano wa Hoja, na mchango wako uongozwe na nguvu ya hoja juu ya hii mada!

Sheria!

Ni marfuku kumshambulia/kumjadili mtoa hoja bali hoja yake!

Matusi hayaruhusiwi! Swaumu kali saa hizi.

Mjadala huru yeyote anaweza kuchangia.


Mimi Naunga mkono hoja 100% sio tu kiushabiki maandazi bali kwa Hoja nzito zifuatazo.

1. FACT. Furaha hainunuliwi ila pia furaha haiji hivi hivi! Vya kufurahisha vina gharama yake.

2. FACT. Money brings peace, and ateasy. Hulazimiki kufanya maamuzi magumu kamakujiuza upate ada ya mwanao.

3. FACT. Mtazamo wa jamii juu yako (Peer pressure) unaweza kukunyima raha na kukushawishi uriconside maamuzi yako kama choice ya mume.

4. FACT. Money is a powerful Motivation to Stay! Hata kama huna raha kuacha ghorofa si mchezo mjue.

4. THEORY. Wanaume wengi hawajatulia. Sasa kuishi na mtu hajatulia na hana kitu inataka moyo mjue.

4. STATISTICS. Ndoa nyingi zinavunjika mume akifukukzwa kazi au kufilisika.

KARIBUNI KWA HOJA ZENU!
 
sikubaliani na mtizamo kwamba ndoa za matajiri zinafuraha na zinadumu kuliko za maskini.

ninavyojua mimi ktk hizo ndoa 2 inategemea furaha yako unaipimaje, so kote kote kunaweza kuwa na furaha au kusiwe na furaha kutegemea na mhusika mwenyewe. Then mtazamo huo ndo uta-determine kudumu au kusambaratika kwa ndoa.

So to me both situations are 50/50, huko vijijini kuna watu ni maskini lakini ndoa zao ni imara asikwambie mtu
 
4. FACT. Money is a powerful Motivation to Stay! Hata kama huna raha kuacha ghorofa si mchezo mjue.

4. THEORY. Wanaume wengi hawajatulia. Sasa kuishi na mtu hajatulia na hana kitu inataka moyo mjue.

4. STATISTICS. Ndoa nyingi zinavunjika mume akifukukzwa kazi au kufilisika.

KARIBUNI KWA HOJA ZENU!

lara 1 nimevutiwa mno na theory, fact na statistics ulizozitoa hapo juu. Najaribu kuziweka pamoja ili nipate kitu ....

Kutokana na theory yako ni kuwa baadhi ya wanaume hawajatulia. Na kwa sababu hiyo sasa, kutokana na fact kuwa "Money is a powerful Motivation to Stay" wanawake wengi huamua kuvumilia kwa kufuata pesa au uwezo wa mtu. Sasa majanga huanza kwa ndoa za namna hii pale ambapo mwanaume amefukuzwa kazi. Ndipo hapa tunapata statistics kuwa
"Ndoa nyingi zinavunjika mume akifukukzwa kazi au kufilisika"

Kwa hiyo nakuunga mkono kuwa kwa watu wasio na upendo wa kweli, ndoa inategemea sana pesa maana pesa na utajiri ndiyo kama kiunganisho na sababu ya msingi ya hiyo ndoa kushikamana. Hakuna upendo, hakuna amani, hakuna furaha, ila kuna pesa za kutafuta mambo hayo sehemu nyingine. Na hapo ndipo huja kuncept ya kukosa uaminifu na kuzaliwa nyumba ndogo kwa wababa na sugar mami kwa akina mama!

Imani yangu bado ipo pale pale, upendo huvumilia yote, hauhusudu, hauhesabu mabaya, hauangalii utajiri, huvumilia, upendo una kiasi nk nk!

Nakaribisha hoja mbadala!
 
wengi mtakataa lakin kwa vile hamna na mnataka kujifariji. pesa ndio kila kitu kwenye ndoa. pata picha shopping dubai.holiday united states. kutengeneza kucha paris. check up german kwa nin ndoa isidumu.

lakin ndoa za kimasikin kwanza mwanaume anajijua kuhudumia shida hivo anakuwa na wivu sana anais anaibiwa.

vurugu kila siku mara tumechoka matembele. pesa ndio kila kitu.

nasema hivo kwa uzoefu wengine toka tukiwa watoto full masafari kila siku mara japan.hongkong.states.german. china. sweden etc kwa nin family isiwe na furaha! !!!!
 
Ni Kweli pesa ndo kila kitu ila mwenye nazo ajue kuzitumia vizuri. Kuna wanaume wengine wanazo za maana lkn baghili, au msimbulizi au anazitumia kwa wengine wa nje zaidi klk kwa familia yake. Ikiwa atazitumia ipaswavyo pamoja na mwenziwake bs YES apo patakua na furaha na uvumilivu wa kutosha tuu hata kama m'ke utatukanwa maadhal Unajua pa kujipoozea kutoka kwa m'me Unajua ngumu
 
Pesa ndio mpango mzima, na hakuna mapenzi katika pesa kilicho ni movie tu. Mfano Liumba alivyowabutua butua kulikuwa hakuna mapenzi lakini dem alikuwa anamuita beib! Na uzee wote ule! K-lyn na Mangi unadhani kuna mapenzi pale?
 
kudumu yes
furaha ni very complicated subject

All in all mwanaume akiwa na pesa 'anavumiliwa' sana weakness zake kuliko bila pesa

Huo 'uvumilivu' una ukweli ndani yake, manake kuna ndoa 'zinazovumiliwa' ambazo zinaacha maswali mengi kuliko majibu....
 
Back
Top Bottom