Paulo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 350
- 66
Ndugu wana JF. Kwenye baya tukemee na kwenye jema tupongeze. Mimi nampongeza Raisi wa Jumuia ya wanafunzi wa kiislamu kwa kufanikisha madai ya wanafunzi hao kwa njia ya amani. Ila tusiache hili jambo lipite hivihivi kabla ya kulijadili. Chini ni picha ya Raisi wa jumuiya hiyo, hivyo naamini na yeye ni mwanafunzi pia. Swali langu ni kwamba hii jumuiya ni ya wanafunzi wa secondary & primary schools tu ama inajumuisha hadi vyuo? Kama haijumuishi na vyuo basi ninamashaka na huyu raisi kwani anaonekana ni mtu mzima na sio wa level ya sekondari. Pia anafuga tu-ndevu kitu ambacho sii ruhusa kwa wanafunzi ambao sii wa college. Hivyo pamoja na pongezi kwake naomba tujulishwe ni mwanafunzi wa level gani. Mwisho, CDM hakikisheni mnampa kadi ya uanachama huyu raisi kabla magamba hawajamhonga!
Source:http://www.issamichuzi.blogspot.com/
Source:http://www.issamichuzi.blogspot.com/