Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 3,464
- 4,239
Inawezekana kuna aina fulani ya maisha tunaanza kuzoeshwa Watanzania, ni aina ya hakuna itakachowezekana bila migomo na maandamano. Maisha ya sasa yamekuwa hata wanafunzi wa chekechea huandamana kudai kuwekewa matuta kwenye barabara zilizo jirani na shule zao.
Ndipo tulipo, na wapo waliofanya tuwe hapa, ambao ni viongozi wasiotaka kutimiza wajibu wao hadi wasukumwe na makamanda wa Chadema, kelele za Bunge na maandamano na migomo ya jamii.
Hili lilisababisha madaktari kugoma, na matokeo yake kiongozi wa madaktari Dr. Steven Ulimboka aliishia kutekwa na kuteswa vibaya hadi kukaribia kifo, kisha kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande.
Kwa kipindi kirefu waalimu wamekuwa na mgogoro na serikali, na kwa bahati mbaya kwa kipindi chote hicho hakukuwa na kiongozi yeyote wa serikali aliyeonesha nia ya dhati ya kumaliza mgogoro huo, na badala yake wakawa wakiuhairisha tu.
Na ndio maana nimeanza kujiuliza ni nani itakuwa zamu yake sasa kwa kuteswa na kwenda kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande kutokana na mgomo wa huu wa waalimu?