Ya Mwinyi na mgomo wa Muhimbili kukimbilia dansi la Kanda Bongoman na Samia na mgomo wa kariakoo na kuzindua minara ya Azam.

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Miaka ya nyuma nchi ikiwa chini ya utawala wa Ali Hassan Mwinyi ilikumbwa na mgogoro mkubwa wa Wauguzi na Waganga kugoma kutibu watu katika hospital kubwa ya Muhimbili. Mgomo ulikuwa mkubwa sana, sasa ikapangwa Mkuu wa nchi aende kuweka sawa mambo. Lakini akakimbia kikao na akaenda kucheza kwasakwasa ya kanda Bongoman. Takriban miaka 30 na ushee imepita, nchi imekubwa na mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo nao wakawa na kauli ya kutaka kuongea na Rais, matokeo yake Rais akamtuma Waziri Mkuu mara mbili. Kitendo cha kushangaza siku iliyofuata Mkuu wa nchi anaenda kuzindua minara ya urushaji matangazo ya kituo cha Azam huku alikimbia kuongea na wafanyabiashara. Je kuna umuhimu upi kwa Taifa kukimbia Kariakoo na kwenda Azam?
IMG-20230518-WA0028.jpg
IMG-20230518-WA0026.jpg
 
Miaka ya nyuma nchi ikiwa chini ya utawala wa Ali Hassan Mwinyi ilikumbwa na mgogoro mkubwa wa Wauguzi na Waganga kugoma kutibu watu katika hospital kubwa ya Muhimbili. Mgomo ulikuwa mkubwa sana, sasa ikapangwa Mkuu wa nchi aende kuweka sawa mambo. Lakini akakimbia kikao na akaenda kucheza kwasakwasa ya kanda Bongoman. Takriban miaka 30 na ushee imepita, nchi imekubwa na mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo nao wakawa na kauli ya kutaka kuongea na Rais, matokeo yake Rais akamtuma Waziri Mkuu mara mbili. Kitendo cha kushangaza siku iliyofuata Mkuu wa nchi anaenda kuzindua minara ya urushaji matangazo ya kituo cha Azam huku alikimbia kuongea na wafanyabiashara. Je kuna umuhimu upi kwa Taifa kukimbia Kariakoo na kwenda Azam?View attachment 2626427View attachment 2626428
Mwinyi akasema Nyinyi mnakwenda Mlimani Park, mimi sisemi kitu, Morogoro jazz sisemi kitu, Makasi sisemi kitu, mimi kwenda Isambe moja tu kelele mji mzima
 
Mwinyi akasema Nyinyi mnakwenda Mlimani Park, mimi sisemi kitu, Morogoro jazz sisemi kitu, Makasi sisemi kitu, mimi kwenda Isambe moja tu kelele mji mzima
Haaahahahahaha hivi alisema haya.
 
Back
Top Bottom