Mgomo wa madaktari wanukia tena

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MADAKTARI huenda wakagoma tena baada ya kikao kati ya serikali na madaktari hao kuvunjika kutokana na kutokuelewana.
Hali hiyo imejidhihirisha baada ya kutokea kutoelewana baina ya wawakilishi wa madaktari hao na maofisa wa Serikali katika ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mgomo wa awali ulimalizika Februari 8, mwaka huu baada ya Pinda kufanya majadiliano na wawakilishi wa madaktari na kuwaomba warejee kazini, kwa maelekezo ya kushughulikia madai yao.
Mtafaruku huo wa sasa umetokea siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kupitia hotuba yake ya Februari kuwataka madaktari hao kuwa na moyo wa subira na kuendelea kutoa huduma kwa Watanzania wakati Serikali ikishughulikia madai yao.

Mtafaruku huo ulitokea juzi na madaktari hao waliamua kuondoka na kuvunja kikao kilichofanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, kujadili madai yao.

Kumekuwepo na mkanganyiko wa sababu zilizofanya madaktari hao kujiondoa kwenye meza ya mazunguzo baada ya taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kikao hicho kimevunjika kutokana na pande hizo mbili kutofautiana.

Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa moja ya sababu za kuvunjika kwa kikao hicho ni madaktari kupinga hoja ya kuhusisha makundi mengine kutoka sekta ya afya kama wafamasia na wauguzi.
Lakini Rais wa chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi aliliambia Mwananchi kuwa wao walikwenda katika ofisi za Waziri Mkuu kufuata majibu ya barua yao waliyoiwasilisha kabla ya mkutano, lakini hawakupewa barua ya majibu.

Alisema barua hiyo pamoja na mambo mengine ilikuwa na maswali kadhaa yanayotaka ofisi hiyo ijibu huku ikieleza namna wao wanavyotaka mkutano wa majadiliano baina yao na Serikali uwe.

“Sisi hatukwenda kukutana kwa ajili ya majadiliano na wahusika bali tulifuata majibu ya barua yetu tuliyowasilisha kwao kabla ya mkutano huo, taarifa ya kuwa sisi tulitoka kwenye mkutano kutokana na kukataa makundi mengine ni za uongo na wameamua kufanya propaganda katika hilo, lakini sisi ni watu wazima tunaelewa.

"Acha wao wafanye propaganda, sisi ni watu wazima tunajua itafika wakati tutakaa nao chini na kufanya uamuzi wenye kuzingatia masilahi yetu na ya umma,” alisema Mkopi.

Ofisi ya Waziri Mkuu
Kwa mjibu wa taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kikao hicho kilivunjika baada ya madaktari kutoka nje ya mkutano kupinga makundi mengine kujumuishwa kwenye mkutano na madaktari.


Madaktari kukutana leo DSM
Wakati hali ikiwa hivyo, madaktari wakiwa chini ya uongozi wa kamati ya muda wanatarajia kukutana leo jijini Dar es Salaam kujadili namna Serikali ilivyotekeleza madai yao waliyokubaliana kwenye kikao cha maridhiano cha Februari 8, mwaka huu na Waziri Mkuu Pinda.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dk Stephen Ulimboka aliliambia Mwananchi jana kuwa mkutano utazingatia makubaliana ya Februari 8, mwaka huu na utekelezaji wake na moja ya madai ilikuwa kutaka Waziri wa Wizara hiyo Dk Hajdi Mponda na Naibu wake Dk Lucy Nkya kuondolwa wizarani hapo.
Pia, Dk Ulimboka alisema mkutano uliovunjika ulioandaliwa na Ofisi ya waziri Mkuu haukuzingatia mahitaji ya pande zote mbili kwa sababu ulifanyika bila ya kuwashirikisha.

Tughe yaonya
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa safarini mkoani Ruvuma, Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ali Kiwenge alisifu hotuba ya Rais Kikwete kuwa imeonyesha serikali imetambua tatizo hilo, lakini akaonya watendaji wa serikali kwenda kinyume na maelekezo ya viongozi wao.
“Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete dhidi ya mgogoro baina ya madaktari na serikali imeonmysha njia sasa serikali inatambua kuwa kunatatizo na iko radhi kulishughulikia.
"Wito wangu na kwa mamlaka zinazohuisika na majukumu hayo yaani watendaji kutekeleza kwa vityendo,” alisema Kiwenge.
Kiwange alifafanua kuwa kitendo hicho ni hatari na kinaweza kurudisha nyuma dhamira nzuri ya Rais na viiongozi wengine ya kutaka kumaliza matatizo na badala yake kupadnikiza migogoro.
Mgomo wa madaktari
Januari 23 mwaka huu madaktari kupitia jumuiya yao waliyoiunda ilitangaza mgomo wa madaktari nchi nzima kufuatia msuguano uliodumu kwa muda wa miezi miwili bila mafanikio huku mamlaka za Serikali na madaktari hao zikishindwa kukaa pamoja.
Hata hivyo madaktari hao wanaingia katika kikao cha tathimini leo huku mengi ya madai yao likiwamo la kumtaka Rais Kikwete kuifumua wizara hiyo kwa kumwajibisha waziri wa Wizara hiyo Dk Hadji Mponda na Naibu wake Dk Lucy Nkya likiwa halijatekelezwa.
 
na leo walikuwa na kikao kikali kujadiliana madaktari wenyewe kwa wenyewe sjui wameafikiana vipi
 
Back
Top Bottom