Anajigonga ili kesho keshokutwa awe mkuu wa wilaya kama Halima Kihemba. Hajui wenzake walibanduliwa kwanza
kuna kitu inaitwa KUBLER ROSS. Huyu jamaa inamkabili ndo maana maongezi yake mengi ni ya aina hiyo. He is fighting. Isome aafu usiniulize kwa nini nimesema hivyo!!
Namuunga mkono Kibs 200%.
Walichofanya madaktari ni zaidi ya utovu wa nidhamu. Ni utoto!
Inawezekana ni kweli wana madai ya msingi.
Walikataa katakata kuonana na mtu mwingine yoyote isipokuwa mtoto wa mkulima.
Pinda huyooo kachomoza tar.29, madaktari hawapo!
Wamekula mpenyo na kumeza uchochoro,
Pinda kabaki pekeyake,madaktari hawapo!
Kwann asipande kwenye maik?
Ana sababu gani asiitendee haki maik?
Kasema aliyosema, hakuna wakumbishia.
Waliopaswa kubishana nae wamemkimbia.
Kwann wananchi tusimsikilize na kuyaamini yale anayoyasema Waziri wetu mkuu Pinda.
Yes, madaktari si wamekimbia?
Madaktari acheni porojo na kudanganyana, rudini kazini!
Inatuambia nini kuhusu wasikilizaji wa Tanzania na medani ya habari kwa ujumla, kwamba Ephraim Kibonde, kati ya wote, ndio the single most prominent social political commentator and news analyst towering over rush hour airwaves of Dar-es-Salaam?
Naona hujanielewa kidogo hapo, au sikueleza vizuri. Hicho ulichosemea "yes," ambayo ndio ilikuwa premise ya swali langu, inatuambia nini kuhusu umma wa Watanzania, kwamba mtu kama Ephraim Kibonde akiwa ndio the most visible opinion leader aliyeko hewani kwenye radio za Tanzania, anaetuchambulia current affairs, je hilo jambo linaashiria nini kuhusu Watanzania na choices tulizonazo katika waandishi wachambuzi nchini?Judging by the amount of threads started about what he says on radio, I say yes.
Naona hujanielewa kidogo hapo, au sikueleza vizuri. Hicho ulichosemea "yes," ambayo ndio ilikuwa premise ya swali langu, inatuambia nini kuhusu umma wa Watanzania, kwamba mtu kama Ephraim Kibonde akiwa ndio the most visible opinion leader aliyeko hewani kwenye radio za Tanzania, anaetuchambulia current affairs, je hilo jambo linaashiria nini kuhusu Watanzania na choices tulizonazo katika waandishi wachambuzi nchini?
Kibondo ni she or he?
Kibonde is just an entertainer/ shock jock.
Sasa sielewi kwa nini watu hutokwa na povu pindi Kibonde atoapo maoni yake kuhusu jambo fulani wakati kituo cha redio anachokitumikia format yake ni burudani zaidi!!
Burudani mpaka kwenye serious issue kama hizi? Burudini zihishie humo humo kwenye kuwaibia wasanii
Anakoelekea sasa atakua she
hivi kweli rafiki yangu inawezekana mtu akupangie siku anayotaka yeye ili aongee/akutane na wewe? waziri mkuu huyu aliwapangia madaktari wakutane hiyo tarehe 29 lakini wao madaktari wakataka kukutana nae tarehe 30; sasa kama kweli huyu waziri mkuu anaejiita mtoto wa mkulima kwanini asiwasikilize watoto wa wakulima wenzake?
Huyu jamaa anajiita mtoto wa mkulima lakini hana sifa za kuitwa mtoto wa mkulima kwasababu anashindwa kutatua matatizo ya watoto wa wenzake ila kwake yeye ni mraisi kuidhinisha posho za wabunge ambao sio watoto wa wakulima, je sheria inaruhusu yeye waziri mkuu kuziidhinisha posho za wabunge kama alivyoachiwa mzigo na huyu mkosa dira ambaye ni mkuu wa nchi?
Huyu mkuu wetu ni mtu ambaye hana mapenzi mema kwa taifa letu ndio maana keki ya taifa alikula na lowassa na rostam na magamba wengine kwenye epa, richmond, kagoda, meremeta, dowans! Sasa anakula na huyu waziri mkuu eti kauli ikiwa pesa za wabunge zinaisha kwaajili ya maendeleo ya jimbo? Mshahara wa mtu kuendesha jimbo?
Na je huyu waziri mkuu kisheria ana uwezo wa kuanika profile la mtu hadharani? Yani serikali yetu kwa sasa ina viongozi mfu wasiofuata utawala wa sheria wala kujali sheria inasema nini kuhusu haki za binadamu!!