Mgogoro ziwa Nyasa: Tahadhari kwa watanzania, hasa watumiaji wa JF

Wakuu,

Pamoja na mijadala kadhaa inayoendelea hapa JF kuwa na hoja zilizo nzuri kwa maslahi ya taifa letu, upo uwezekano mkubwa kwamba, maadam mchokozi na watu wake nao wanajua Kiswahili, pengine wako nasi mtandaoni wakifuatilia kila kinachoandikwa kwa sababu zao za kiintelijensia.

Hivyo tunapoendelea kujadili, si vibaya kutahadhari tusijikute tumesaidia kumweleza adui kila udhaifu tulionao. Badala yake, tunaweza kujikita katika kuanika kile anachoendelea kufanya katika eneo letu na kile anachokusudia kufanya baadaye.

Wazee wa kule kanda ya ziwa Nyanza wana msemo; Zamani chui alikuwa hajui kukamata shingo la mawindo yake, alijifunza baada ya kusikia mawindo ya kinong’ona kwamba; ‘tunachomoka maana anakamata mikia, siku akikamata shingoni, tumekwisha’

Jamani ni kitu gani tunachojadili humu kitasaidia Wamalawi Kiitelijensia? Wengine hata hatuko Bongo tunaongelea

Maoni yetu kweli itahatarisha Usalama wa Taifa letu? Kweli tumeanza kuwa na maisha ya kiuwalakini? sasa hata jani

likitugusa tunaruka tunadhani ni NYOKA? tumekuwa DHAIFU kiasi hicho?

How Shocking... Hembu tueleze UDHAIFU gani humu Jamii Forums tutamueleza MMALAWI atumalize taifa la watu

MILIONI 40? na wao MIL 7? OH wana NUCLEAR BOMB?

TAFADHALI USITUNYIME UHURU WA KUCHANGIA HUMU KWENYE JAMII FORUMS; THE ONLY PLACE ANGALAU TUNAONGEA

KWA UHURU WETU...
 
Kwa mujibu wa CIA, jamaa wako hivi;

​Nguvu za Kijeshi za Malawi

Malawi Defense Forces (MDF): Army (includes Air Wing, Marine Unit) (2009)
Military service age and obligation:
18 years of age for voluntary military service; standard obligation is 2 years of active duty and 5 years reserve service (2007)
Manpower available for military service:
males age 16-49: 3,514,809 (2010 est.)
Manpower fit for military service:
males age 16-49: 2,132,909
females age 16-49: 2,043,925 (2010 est.)
Manpower reaching militarily significant age annually:
male: 183,683
female: 183,028 (2010 est.)
Military expenditures:
1.3% of GDP (2006)
country comparison to the world: 112

tuwekee na ya Tanzania mkuu
 
Malawians at their boiling point now,they stick to their guns claiming the entire lake belongs to them.Iam very sceptical if diplomatic approach will bring a common understanding between the two countries involved taking into account Malawians are current exploring oil and gas in the lake. And this is being fueled by foreign oil companies which has lobbed their govt.The only remaining approach is Tz must begin a military campaign against their government
 
Kabla ya mazungumzo jeshi likague uvamimizi wa aina yoyote na kuushughulikia halafu mengine baadaye
 
najikuta nasikitika tu, heshima ya mtanzania imeshuka kiasi hiki??? loh!
sana! kwa sababu utaifa haupo tena, watu wanajali zaidi ulafi wa mali hasa viongozi, halafu tujifunze kitu hapa, ni vyema kusema ukweli!!!!!tukiwage vita na hawa jamaa sasa hivi hatushindi!!! amini usiamini, we r so divided! na hawa wanajua hili, tunaweza kuanza vzr but adui anaweza tumia udhaifu tulio nao mf. anaweza amua kuwavisha kanzu war casualties na kuonesha misikiti imepigwa mabomu the other day utaona watu hapa ndani wanasema bora tuwape malawi ushindi kama vita ndio viko hivyo! lkn pia tuko hoi, uchumi wetu uko kwny mawe, viongozi wetu hawana majibu ya matatizo tuliyo nayo km mishahara isiyokidhi na wanasema serikali haina uwezo kulipa mishahara wanayostahili wafanyakazi, sasa sijui wanabaki hapo kufanya nini???? mtu akikiri hawezi fanya jambo fulani si anatoka wanakuja wale watakaoweza!!
 
hivi tukipigana na Malawi ndio itakuwaje?

Mkuu, hakutakuwa na vita.

Ni suala la malumbano tu lakini suala la diplomasia ndio lipewe nafasi lifanye kazi yake.

Haya mambo ya vita waachiwe wenye kupenda vita maana kuna mataifa yamebinafsisha vita na kila kukicha wanatengeneza silaha za kutumiwa katika vita.

Juzijuzi jamaa wamepewa kiasi cha K10.7 bilioni kutoka Germany na ndizo zinawasumbua maana wakati wa enzi ya Mutharika walikuwa hawaoni hata senti ikitumika kuleta maendeleo.
 
Hata hujui unaongea nini
tena mwambie akome kabisa hivi alijua pale gongo la mboto kulikuwa na vitu heavy? kwenye swala hili wa tz wote tupo pamoja bila kujali chama kikwete kwenye hili tupo pamoja sema neno moja tu na roho zetu zitapona
 
kwa hili, hatakamasitakuwa na silaha nitakwenda ziwa nyasa kumwondosha huyu mama kwa bakora bila kujali ana askari wenye silaha za aina gani.
 
It is noted that rumors of war ignite an imbecilic passion for confrontation and suppresses all aspects of civilized intellectual analysis, on both sides.

I hope cooler heads will prevail up the food chain.
 
tuwekee na ya Tanzania mkuu

Nilichelea kuweka za kwetu maana itakuwa ni kuwarahisishia kazi. Hata hivyo wanazijua tu, maana takwimu za mitandaoni ni accessible.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, tunawazidi sana tu. Kama hawana kiburi cha 'mtu' fulani nyuma yao, wanajitafutia tu matatizo.

Tanzania People's Defense Force (Jeshi la Wananchi la Tanzania, JWTZ): Army, Naval Wing (includes Coast Guard), Air Defense Command (includes Air Wing), National Service (2007)
Military service age and obligation:
18 years of age for voluntary military service (2007)
Manpower available for military service:
males age 16-49: 9,985,445 (2010 est.)
Manpower fit for military service:
males age 16-49: 5,860,339
females age 16-49: 5,882,279 (2010 est.)
Manpower reaching militarily significant age annually:
male: 512,294
female: 514,164 (2010 est.)
Military expenditures:
0.2% of GDP (2005 est.)
country comparison to the world: 169

lakin kwa Tanzania ya leo malawi wanahitaji kweli kutumia nguvu? kuna mafisadi yakipewa hela yanauza hilo ziwa bila tatizo, vijisenti tu vinatosha kuuza nchi
 
Jamani ni kitu gani tunachojadili humu kitasaidia Wamalawi Kiitelijensia? Wengine hata hatuko Bongo tunaongelea

Maoni yetu kweli itahatarisha Usalama wa Taifa letu? Kweli tumeanza kuwa na maisha ya kiuwalakini? sasa hata jani

likitugusa tunaruka tunadhani ni NYOKA? tumekuwa DHAIFU kiasi hicho?

How Shocking... Hembu tueleze UDHAIFU gani humu Jamii Forums tutamueleza MMALAWI atumalize taifa la watu

MILIONI 40? na wao MIL 7? OH wana NUCLEAR BOMB?

TAFADHALI USITUNYIME UHURU WA KUCHANGIA HUMU KWENYE JAMII FORUMS; THE ONLY PLACE ANGALAU TUNAONGEA

KWA UHURU WETU...

Mkuu nadhani hatujaelewana. Sijazuia kujadili na wala simyimi mtu yeyote uhuru (sina nia, mamlaka, wala uwezo wa hilo). Nimetoa tu tahadhari ili anayekwambia atakupiga mateke usimwambie au kumwonesha sehemu gani ya mwili wako kuna kidonda. Kama hujasoma posts zote kwenye uzi huu, nirudie tu kwa ajili yako kutoa taarifa kwamba magazeti yao tayari yanaandika habari kwa kutumia jamiiforums kama chanzo cha taarifa.
 
Ukweli ukidhihiri uwongo hujitenga! Huu wizi wa kuchukua mali za watu utamalizika lini? Wanyasa wanayohaki ndio wakaidai na nina mategemeo makubwa watashinda mbio zao! M/mungu hayupamoja na wanaodhulumu! Ikiwa wanyasa madai yao ni kweli watathibiti! Nyasa inatumika nguvu znz imetumika ghilba na nguvu. Ya rabbi wadamirishe madhalimu. Amin

Mkuu abousalah, haki ipi ya wanyasa unayoizungumzia? Kumbuka kingo za mto, ziwa hata bahari hubadilika (fikiria kama ikitokea karne kadhaa zijazo hilo ziwa likafifia au likapanuka hadi Mbeya mjini).
Rejea pia Azimio la umoja wa mataifa la mwaka 1982 kuhusu mipaka ya nchi katika maji. katikati ya maji ndio mpaka (labda iwe imekubalika vinginevyo).
 
Msimamo wangu uko pale pale

Kama wa TZ tunataka kupigwa adi kupelekwa utumwani malawii tujaribu kujitumbukiza kwenye vita hii, kwani jeshi letu liko hoi kabisaa kama sio goi goi, silaha zote nzito nzito zililipuka mbagala na gongo la mboto, pesa za kununulia silaha hakuna! watanzania na hasa sisi vijana tuko demoralised hivyo hakuna anaye kubali kwenda vitani ( labda uvcccm)
 
waambie hao! vita sio maneno na propaganda mufilisi, tunajipanga, ifike mahali, mchakato unaendelea, tumeliona...such rubbish, hao usalama wa ccm wanapoteza muda mwingi kulumbana jf waulize strategies zozote hawana! km taifa tmeshindwa in every front!!!uwekezaji na ma-conmen, mishahara hewa, uzembe wa kufikiri, ubnafsi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola kwanza ni dharau malawi kutaka kuwage battle na sisi lkn wanatujua vzr tz ya 1980s si ya sasa..ndo tulipofika kama watu hata humu jf hawawezi ona dalili zote za taifa dhoofu utashinda vita hapo! kwa njia gn? wingi wa jeshi si kushinda vita! unaweza kuwa na jeshi kubwa la wajinga tu! mara ngp jeshi letu linatumiwa kisiasa? sasa kuna umoja hapo!
 
i smell war,.they talk with confidence they must have a strong western backing,because if not mwamunyange will smash this little country like a roach

Mimi Gwamahala,akina Mwamunyange,Mwakyembe,Mwandosya na wengine wote LAZIMA tuwatetee ndugu zetu wa Malawi!
 
Msimamo wangu uko pale pale

Kama wa TZ tunataka kupigwa adi kupelekwa utumwani malawii tujaribu kujitumbukiza kwenye vita hii, kwani jeshi letu liko hoi kabisaa kama sio goi goi, silaha zote nzito nzito zililipuka mbagala na gongo la mboto, pesa za kununulia silaha hakuna! watanzania na hasa sisi vijana tuko demoralised hivyo hakuna anaye kubali kwenda vitani ( labda uvcccm)

yawezakana ukawa hulijui JWTZ,lina silaha nzito sana pia lina Kambi mpaka za Makomando. Ushawahi kuisikia Kambi inaitwa Ngerengere? Achana na hiyo kuna kambi zinatengeneza SILAHA hapa Tanzania na siwezi kuzitaja.
 
Kaka lakini ni kweli kwenye mambo kama haya tuwe waangalifu sana, security ya nchi ni kitu sensitive sana, hapa hakuna kujadili udhaifu tena, ni strengths tu, vita ya argetina na uingereza, waingereza walishinda kwa maneno tu akini walishapigwa, tuwe makini sana.

Back
Top Bottom