Mgogoro kutokea UKAWA

Robethn

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
2,103
352
MAMBO NYETI WASIYOJUA CHADEMA KUHUSU LOWASA:

Nikiwa kijijini Kolo Kondoa, nimeamua kuwaandikia jirani zangu wana Chadema. Japo niwasaidie kujua kuwa mbeleni wanayo ya kutarajia.
Chama cha Demokrasia na maendeleo kimeamua kufanya uamuzi wa karne wa kumkaribisha mtu kutoka chama kingine na kumkabidhi dhamana ya kugombea Urais ndani ya siku mbili tu.
Hii inapaswa kuingia kwenye rekodi za dunia maana haijawahi kutokea katika historia ya demokrasia duniani.
Lakini pamoja na uamuzi huu unaofananishwa na kumualika Simba kijijini muishi nae, yako mambo nyeti ambayo wana Chadema hawayajui na watakuja kuyajutia mbeleni, na in fact wameanza:-

1 . Edward Lowasa sio mtu, ni taasisi. Ni taasisi kamili yenye watu walioahidiwa vyeo vyote vya kitaifa kuanzia watendaji wa vijijini, maafisa tarafa, wakuu wa wilaya na mikoa, makatibu wa chama, wajumbe wa bodi mbalimbali n.k.
Lowasa hahitaji wasaidizi wala washauri wa Chadema, ana vyombo vyake atakavyovitumia. Ukiangalia wakati anakwenda kuchukua fomu ya Urais, utamuona mzee mmoja ana mvi anaitwa Chizii, huyu ndiye mshauri wa Lowasa wa mambo ya uchaguzi. Sio mwana Chadema, bali aliingia Chadema siku moja na Lowasa. Leo ni mshauri wa mgombea.Ajabu.
Wana Chadema wasijiroge kuwaza kuwa mipango ya Lowasa itaamuliwa na kamati kuu yao au kampeni zitaratibiwa na Chadema. La hasha.

2. Kitu pekee kinachowaunganisha Chadema na Lowasa ni Urais. Hakuna mfanano wa itikadi, falsafa na hata mfumo wa uendeshaji wa chama. Siku mbili zisingetosha kuleta uwiano huo.Ndio maana Lowasa anaona kinyaa hata kuvaa kombati la Chadema. Tazama picha na video zote, hutamuona na kombati, labda aanze leo baada ya makala hii.

3. Baada ya Oktoba 25 ya uchaguzi mkuu, patakua na Chadema asili na Chadema Lowasa. Lowasa na timu yake wataiteka Chadema. Hapa timu Lowasa, 4u movement n.k ndio watakaobeba vyeo na nafasi za maamuzi zinazoshikiliwa na Chadema asilia. Mfano mkubwa ni Dr. Slaa alivyotolewa sadaka pamoja na jasho lake lote kujenga Chadema. Chezea nguvu ya Lowasa!

4. Lowasa ana kiu ya kutaka mamlaka isiyokwisha hata anywe maji ya bahari.
Atahakikisha anaiteka kamati kuu ya Chadema na vyombo vyote vya maamuzi kwa kutumia nguvu ya pesa vimtumikie yeye. Mbowe,Mtei watajikuta hana tena uwezo wa kuamuru (command) ndani ya chama. Kila jambo litaamuliwa kama Lowasa atakavyo.Hayo ndiyo aliyoyataka CCM akayakosa.

5.Lowasa ni katili, na ana visasi. Hatamsamehe Dr Slaa na wengine wote asiowataka atawaondoa Chadema. Hivyo wale wenye viherehere huko wajiandae kufunga virago.

6.Lowasa ataifanya Chadema iwe na sura yake, tutashuhudia rushwa kupindukia kwenye chaguzi za Chadema, maana kila mtu atataka kuwa karibu na Lowasa ili apate ulaji.

Kwa mtazamo wangu Chadema itakua imeisaidia sana CCM kuendelea kushika dola kwa muda mrefu mwingine, maana sasa tabia zote za kiLowasa zitakua zimehamia Chadema. Kwa mara ya kwanza katika historia chama cha upinzani kitakwenda kwenye uchaguzi kikiwa kina masuala ya kujibu kuhusu ufisadi wa mgombea wao wa Urais. Wanachama na viongozi wa Chadema wajiandae kumfuata Dr. Slaa nje ya mfumo. Hongereni timu Lowasa na wana 4u Movement, maana sasa mtakamata hatamu ndani ya chama kipya. Makamanda wajiandae kisaikolojia. ACT itaibuka kuwa Chama kipya cha upinzani ifikapo mwaka 2020. Chadema na wana UKAWA watafutika katika ramani, maana baada ya Lowasa hakuna tena atakaekuwa na uwezo wa kukiendesha chama.Itakupasa uwe tajiri kama Lowasa tena.
Namshukuru Mungu mimi si mwana Chadema.
Tafakari na fanya maamuzi
 
Very stupid post.. mbaya zaidi umeanzia kolo, wanaowajua warangi wa kolo wanaelewa why umerefer hiyo location... Very simple reason, next post utakuja nayo ni ya dini, na utalenga hadi mgombea wa ubunge, mwisho kabisa utahamia ukawa fully as if you were ccm

busted

very cheap
 
CCM itazidi kushinda kutokana na kupiga vita migogoro isiyokuwa ya lazima.
 
Sasa wewe mambo ya CHADEMA yanakuhusu nini? Kwanini usingekaa kimya na kuendelea kujenga chama chako?
 
Cybercrime ikianza kazi itaanza na wewe.. Potelea mbali, Alete maendeleo asilete nita$chagua Lowasa kuonyesha dunia kwamba Tanzania sio kwa ajili ya CCM pekee, ni kwa ajili ya watanzania wote.
 
Vyama vya upinzani ni njaa tu, vinatulaghai wanainchi, tuwe makini sana.
 
Hizi ID mwaka huu,mtoa mada ana siku 10 tu JF lakini keshakuwa mwenyeji- Huyu Lowassa naona kawakalia pabaya kuwa taasis cha ajabu nini,mbona alikuwa mkubwa kuliko CCM yenyewe ikabidi akatwe kwa hila
 
Kwani alikokimbilia Lowassa ndo kuna demokrasia? yeye aliteuliwa kwa misingi ya kidemokrasia? njaa ya madaraka inamhandama Babu Lowassa
 
Hamna haja wa kuwa na hili jukwaa sasa,kama pumba kama hizi zina wekwa hapa,,????
 
kwamba lowasa atahodhi madaraka hilo liko wazi,kama makamanda hawakuliona pole zao.
ndo maana saa ingine nataka huyu ashinde nijionee senema.

najua akishinda lowasa,uwezekana wa duni kuwa rais ni mkubwa sana....
 
MAMBO NYETI WASIYOJUA CHADEMA KUHUSU LOWASA:

...Kitu pekee kinachowaunganisha Chadema na Lowasa ni Urais. Hakuna mfanano wa itikadi, falsafa na hata mfumo wa uendeshaji wa chama. Siku mbili zisingetosha kuleta uwiano huo.

...Baada ya Oktoba 25 ya uchaguzi mkuu, patakua na Chadema asili na Chadema Lowasa. Lowasa na timu yake wataiteka Chadema. Hapa timu Lowasa, 4u movement n.k ndio watakaobeba vyeo na nafasi za maamuzi zinazoshikiliwa na Chadema asilia. Mfano mkubwa ni Dr. Slaa alivyotolewa sadaka pamoja na jasho lake lote kujenga Chadema. Chezea nguvu ya Lowasa!

Mkuu! sio vizuri kuongea ukweli kipindi hiki cha mihemko.
 
Back
Top Bottom