Mgogoro Arusha: Maaskofu bado hawamkubali Meya na Mary Chatanda!?

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Kuna uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru unaofanyika kimkoa katika kiwanja cha jengo la azimio la Arusha, jirani na mnara wa mwenge jijini Arusha. Viongozi wa halmashauri zote wamehudhuria wakiwemo madiwani na viongozi wa dini zote. Pia yupo Mary Chatanda na "Mstahiki Meya". Kati ya viongozi wa dini, hakuna Askofu hata mmoja wa majimbo yote ya Arusha. Badala yake wapo wawakilishi tu ambao ni wachungaji na mapadri.
Ninachojiuliza ni kwamba, bado wanaendelea na msimamo wao wa kutomtambua "Meya" na kutoshirikiana na Mary Chatanda?
Naomba kuwasilisha.
 
Wana majukumu mengine ya kidini ndiyo maana wakatuma wawakilishi wao.
Sidhani kama wangesusia wangekubali kuwakilishwa... huu ni mtazamo wanagu tu
 
Hata wakisusia ni sawa tu, maana kimsingi Meya bado hakubaliki, na huo ndiyo msimamo wa cdm-Taifa.
Ukirejea kauli yao siku ya mazishi ya kitaifa ya wapambanaji waliouawa na polisi, utakuta kuwa walitoa tamko kuwa hawataukubali uongozi ulioingia madarakani kwa njia haramu!
Kama hawapo kwa mtindo wa kususa, i personally support them, kwani wanasimamia wanachokiamini!
 
Kuna uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru unaofanyika kimkoa katika kiwanja cha jengo la azimio la Arusha, jirani na mnara wa mwenge jijini Arusha. Viongozi wa halmashauri zote wamehudhuria wakiwemo madiwani na viongozi wa dini zote. Pia yupo Mary Chatanda na "Mstahiki Meya". Kati ya viongozi wa dini, hakuna Askofu hata mmoja wa majimbo yote ya Arusha. Badala yake wapo wawakilishi tu ambao ni wachungaji na mapadri.
Ninachojiuliza ni kwamba, bado wanaendelea na msimamo wao wa kutomtambua "Meya" na kutoshirikiana na Mary Chatanda?
Naomba kuwasilisha.

Kwani wao wapo chadema?if yes watakuwa wameliona tamko la godbless lema na wana act!
 
Well, well, well, nimeshapata majibu humuhumu mtandaoni!
Madiwani Walioingia muafaka(bila ridhaa ya chama) ni hawa 3 chini:
-Estomi Mallah,
-John Bayo na
-Efatha Nanyaro.

Shame on them!
 
Yule wa kanisa katoliki Askofu JOSEPHAT LEBULU yupo Nairobi kuhidhuria mkutano mkuu wa AMECEA na uzindizi wa maadhimisho ya siku kuu ya miaka 50 ya AMECEA
 
Wana haki kama Watanzania CDM ni chama chao hawawezi kumtosa mwezao a loser Dk Slaa
 
Well, well, well, nimeshapata majibu humuhumu mtandaoni!
Madiwani Walioingia muafaka(bila ridhaa ya chama) ni hawa 3 chini:
-Estomi Mallah,
-John Bayo na
-Efatha Nanyaro.

Shame on them!
Mkuu sijakuelewa Nanyaro huyu ninayemfahamu mimi au mwingine? Kama ni yeye ni jambo la aibu sana kwake.
 
Kuna uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru unaofanyika kimkoa katika kiwanja cha jengo la azimio la Arusha, jirani na mnara wa mwenge jijini Arusha. Viongozi wa halmashauri zote wamehudhuria wakiwemo madiwani na viongozi wa dini zote. Pia yupo Mary Chatanda na "Mstahiki Meya". Kati ya viongozi wa dini, hakuna Askofu hata mmoja wa majimbo yote ya Arusha. Badala yake wapo wawakilishi tu ambao ni wachungaji na mapadri. Ninachojiuliza ni kwamba, bado wanaendelea na msimamo wao wa kutomtambua "Meya" na kutoshirikiana na Mary Chatanda? Naomba kuwasilisha.
mkuu yaelekea wewe ni mmojawapo wa madiwani wasaliti.kwani diwani wa cdm kaloleni anaitwa charles philipo(rasta) na wewe username yako inaendana na jina la diwani huyu!
 
Maaskofu bwana! mimi nadhani siku zote wanasimamia amani, upendo sasa wamesusa!!!!!! Kweli nyakati za mwisho tutaona mengi
 
Maaskofu wana hasira sana yule mgombea wa Urais Padri Mstaafu ambae hajaoa alipigwa kwa election na JK! Nimemuona jana Ofsi za CDM amenyoa upala na Gwanda lake basi kama kikatuni! Na mkono wake naona ule hauponi tena!
 
Mimi sio diwani wala sio kiongozi yeyote wa chama wala serikali! Na jina la Philipo sio Surname yangu. Nilipita kwenye hilo eneo nikawaona na ndio wageni walikuwa wanatambulishwa. Majina yatakuwa yamefanana tu! @Jack
 
@ Jack,
Mkuu uclazimishe! Nimekwambia mimi sie. Jmosi kuna kikao cha wana JF ambao ni wakazi wa hapa Arusha pale Soweto Garden saa 11. Njoo utaniona!
 
Back
Top Bottom