Mgawo wa Umeme unaweza kuisha kwa kuanzisha Shamba la Kuvuna umeme wa Jua

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Kauli za Serikali kuhusu swala la Mgao wa Umeme zimekuwa kero zenyewe, maana kila siku kuna Vijisababu ambavyo havina majibu.

Sasa mimi nashauri Serikali iangalie namna ya kupata mwekezaji, ambaye atatuletea huduma hii ya kuvuna umeme wa jua na kwa hili jua la Dar yaani umeme utakuwa unanguvu sana. Baada ya Jua kuchoma Wananchi lichome Solar Pannels sisi tupate umeme, na hii itashusha Gharama za umeme kabisa.

Pia inaweza kutumika kama 'backup' ya umeme wa sasa huu umeme wa kupigizana kelele.

Naomba mamlaka husika mfikirie hili ili tupate suluhu rafiki kwa swala hili. Huu mradi tunaweza ufanya hata wenyewe.

american-public-power-association-fm5_vCUa-Bc-unsplash.jpg
 
Back
Top Bottom