Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Hakuna asiye jua kuwa kwa sasa kuna shida ya Maji na Umeme kwa baadhi ya maeneo hasa Mkoa wa Dar Es Salaam, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limechangiwa na upungufu wa mvua ambazo zilitakiwa ziwe zimeanza kunyesha toka mwezi September ili kuweza kujaza mito ambayo inamwaga maji yake katika mito inayotumika kama chanzo cha maji yanayotumika nyumbani na viwandani mfano Ruvu. Aidha, mabwawa yanayotumika kuzalisha umeme nayo yamepungua kina na hivyo kusababisha upungufu wa uzalishaji umeme.
Kwa miaka yote toka Tanganyika kupata uhuru na baadaye Tanzania kuzaliwa (baada ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika) tumekuwa tukitegemea mito na mabwawa kama chanzo kikuu cha maji yanayotumika nyumbani na viwandani, pia mabwawa kama chanzo cha uzalishaji umeme, ambavyo vyote vinategemea uwepo wa mvua za kutosha. Mabadiliko ya hali ya hewa duniani kote yamesababisha upungufu mkubwa wa mvua, hivyo kufanya mito na mabwawa mengi kukosa maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani.
Tatizo hili halijaanza jana wala juzi, tatizo hili ni matokeo ya kuwa na chanzo kimoja, hata kama Serikali ingekuwa inaongozwa na Chadema au ACT au chama chochote nje ya CCM hakuna namna ambayo wangeweza kutatua tatizo hili kwa siku mbili au ndani ya mwezi mmoja.
Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kuwa maji na umeme ni uhai kwa kila Mtanzania, imefanya juhudi za haraka na makusudi ili kuondoa tatizo hili, Serikali imepeleka fedha nyingi kuhakikisha miradi ambayo ilikuwa haijakamilika inakamilika na kuweza kutoa huduma kwa Mkoa wa Dar Es Salam. Serikali imeendelea kuchukua hatua za muda mfupi na za muda mrefu kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa moja kwa moja.
Watanzania kwa umoja wetu, tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu katika jitihada za kutatua changamoto za maji na umeme.
Tumuunge mkono Waziri wa Maji na Umwagiliaji -Juma Aweso pamoja na Wataalamu wake, ni muda sasa umefika kuanza kuangalia namna ya kufanya bahari kuwa chanzo kikuu cha maji yakutumika nyumbani na viwandani, Dunia iko mbali na Teknolojia iko mbali. Mito na mabwawa sio chanzo cha kuaminika tena katika dunia hii ambayo mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake si jambo la kuuliza tena.
Tumuunge mkono waziri wa Nishati -January Makamba pamoja na Wataalamu wake wakati huu wakipambana kuhakikisha tunapata vyanzo vya uhakika vya umeme. Kwa miaka yote tumekuwa tukitegemea maji kama ndio chanzo chetu cha uzalishaji wa umeme. Mheshimiwa January Makamba, pamoja na spana zote unazopigwa ambazo pengine hustahili kabisa, Mwenyezi Mungu atakulipa kwa kadri utakavyoiwezesha Tanzania kutoka katika umeme wa kutegemea chanzo cha maji, kwa namna mabadiliko ya hali ya hewa yalivyo nachelea kusema baada ya miaka 10 ijayo maji itakuwa ngumu saana kutumika kama chanzo cha kuzalisha umeme.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.