Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,306
- 2,081
kama tatizo ni ukame awaombe wahisani waumalize ukame mvua zinyeshe mgao uishe
tumechoshwa na sababu za mwaka 47!
Hebu jikumbushe vijipande vidogovidogo jinsi Waziri Mkullo alivyogusia Umeme kwenye bajeti aliyosoma ya 2011/12
Mheshimiwa Spika,Upungufu wa Nishati ya umeme
Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokanana kiwango kidogo cha uzalishaji usioendana na mahitaji. Kwa kuzingatia kuwa umeme una umuhimu wa kipekee katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali itachukua hatua kadhaa za kukabiliana na upungufuhuu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza; kuiwezesha TANESCO kupata mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa kwa ajili yakununulia mitambo ya uzalishaji na kuangalia upya namna ya kugawanya shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji; kwa lengo la kuiachia TANESCO kujikita kwenye eneo ambalo ina uwezo nalo kiushindani na hivyo kuleta ufanisi katika sekta nzima ya umeme.(Mimi nahisi hapo penye red TANESCO anatengenezewa Jeneza)
Aidha, kutokana na kukamilishwa kwa sera, sheria na kanuni za ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP),Serikali itaandaa utaratibu wa kuhusisha sekta binafsi katika sekta ya umeme na inatarajiwa kwamba baadhi ya miradi ya uzalishaji umeme itatekelezwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.
(Sijui kama kweli zitakuwa sekta binafsi)
Serikali imeshaanza majadiliano na wawekezaji katika uzalishaji wa umeme kwa ubia katika miradi ifuatayo; Mtwara MW 300, Mpanga MW 144, na miradi ya usafirishaji umeme wa kV 400 ya Morogoro-Tanga-Kilimanjaro-Arusha km 682 na upanuzi wa Gridi ya Kaskazini Magharibi kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa - km 1000.
………………………………………………………………………………………………………………………………………..........................................................................................
Serikali inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na biogesi pamoja na kutumia kwa uangalifu nishati ya umeme iliyopo.
(Asante Mkullo kwa kutufumbua macho wadanganyika)
……………………………………………………………………………………………………………..................................................................................................................
baina ya viwanda vya nguo na sekta ya kilimo. Juhudi zinazoendelea za kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa maji na mafuta ambavyo ni upepo, jua na biogesi, zitasaidia kufanikisha mpango wa uzalishaji wa bidhaa viwandani. Kadhalika, Serikali itaboresha mazingira ya sekta ya viwanda (vikubwa, vidogo na vya kati), ili
kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
(Ngeleja baada ya wiki tatu uje utupatie bajeti uliyotenga ya Umeme wa upepo, Jua, na Biogesi)
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
MheshimiwaSpika,
vii) Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 200 kama sehemu ya gharama kwa ajili ya ununuzi wa genereta zenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 60 kwa mkoa wa Mwanza na megawati 100 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
(Tumeona lakini isije kuwa Dowans nyingine)
e) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi za kutengeneza vifaa vinavyotumia mionzi ya jua (inputs for manufacture of solar panels) kwa lengo la kuhamasisha uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini.
(Mhhh,....Kweli hako sio kamradi ka mtu?...tutajua tu kwani sasa hivi kila mtanzania ni Thomaso)