Mgao wa Umeme: Tatizo ni UKAME - Kikwete akihojiwa na BBC

kama tatizo ni ukame awaombe wahisani waumalize ukame mvua zinyeshe mgao uishe
tumechoshwa na sababu za mwaka 47!

Hebu jikumbushe vijipande vidogovidogo jinsi Waziri Mkullo alivyogusia Umeme kwenye bajeti aliyosoma ya 2011/12


Mheshimiwa Spika,Upungufu wa Nishati ya umeme
Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokanana kiwango kidogo cha uzalishaji usioendana na mahitaji. Kwa kuzingatia kuwa umeme una umuhimu wa kipekee katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali itachukua hatua kadhaa za kukabiliana na upungufuhuu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza; kuiwezesha TANESCO kupata mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa kwa ajili yakununulia mitambo ya uzalishaji na kuangalia upya namna ya kugawanya shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji; kwa lengo la kuiachia TANESCO kujikita kwenye eneo ambalo ina uwezo nalo kiushindani na hivyo kuleta ufanisi katika sekta nzima ya umeme.

(Mimi nahisi hapo penye red TANESCO anatengenezewa Jeneza)

Aidha, kutokana na kukamilishwa kwa sera, sheria na kanuni za ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP),Serikali itaandaa utaratibu wa kuhusisha sekta binafsi katika sekta ya umeme na inatarajiwa kwamba baadhi ya miradi ya uzalishaji umeme itatekelezwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.

(Sijui kama kweli zitakuwa sekta binafsi)

Serikali imeshaanza majadiliano na wawekezaji katika uzalishaji wa umeme kwa ubia katika miradi ifuatayo; Mtwara MW 300, Mpanga MW 144, na miradi ya usafirishaji umeme wa kV 400 ya Morogoro-Tanga-Kilimanjaro-Arusha km 682 na upanuzi wa Gridi ya Kaskazini Magharibi kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa - km 1000.
………………………………………………………………………………………………………………………………………..........................................................................................

Serikali inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na biogesi pamoja na kutumia kwa uangalifu nishati ya umeme iliyopo.

(Asante Mkullo kwa kutufumbua macho wadanganyika)

……………………………………………………………………………………………………………..................................................................................................................
baina ya viwanda vya nguo na sekta ya kilimo. Juhudi zinazoendelea za kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa maji na mafuta ambavyo ni upepo, jua na biogesi, zitasaidia kufanikisha mpango wa uzalishaji wa bidhaa viwandani. Kadhalika, Serikali itaboresha mazingira ya sekta ya viwanda (vikubwa, vidogo na vya kati), ili
kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

(Ngeleja baada ya wiki tatu uje utupatie bajeti uliyotenga ya Umeme wa upepo, Jua, na Biogesi)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
MheshimiwaSpika,

vii) Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 200 kama sehemu ya gharama kwa ajili ya ununuzi wa genereta zenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 60 kwa mkoa wa Mwanza na megawati 100 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

(Tumeona lakini isije kuwa Dowans nyingine)



e) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi za kutengeneza vifaa vinavyotumia mionzi ya jua (inputs for manufacture of solar panels) kwa lengo la kuhamasisha uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini.

(Mhhh,....Kweli hako sio kamradi ka mtu?...tutajua tu kwani sasa hivi kila mtanzania ni Thomaso)


 
Ee Mungu tunaomba utusamehe kwa kumchagua huyu bwana kuiongoza nchi yetu hii. Tulidanganywa kwa ahadi kemkem, pia tulielezwa kuwa hili ni chaguo lako. Lakini sasa tunashindwa kuelewa kuwa hili ni chaguo la nani hasa. Tunaomba utusamehe kwa hili na mengine tuliyokukosea.
Amen
 
Tunasaikitika Rais wa nyakati hizi anaongelea na kusingizia ukame kwenye umeme. Kungekuwa na usaili kuhusu umeme wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana angeshindwa. Haingii kichwani mtu ambaye yuko angani kama popo kwenye umeme wa uhakika aongelee mambo ya Mtera kukosa maji! Enzi za sayansi na tekinoloji bado una ukungu wa kujua kuna vianzo mbadala vya umeme? Si bure atakuwa kwenye mtandao wa Jairo kwenye sakata la kulazimisha bajeeti kupita! Nadhani hata Mwl Nyerere angeibuka leo angeitisha uchaguzi mkuu. Lakini alitamka wazi mwaka 1995. Sasa tumeyaona/. Taifa liko hoi na viwanda vimefungwa yuko na mashada ya maua SA kwenye makaburi ya wapiganaji wa zamani. Nchi tulizozisaidia sasa ziko juu kiuchumi. Inatia aibu kuangalia wa tz hawana basics: chakula, malazi, matibabu. Wahalkifu red handed wanaundiwa kamati na kupelekwa likizo ya malipo.
 
Hivi huu ukame unaiathiri nchi yetu tu!? Mbona majirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zambia, Malawi n.k. nao wana hali ya hewa kama ya kwetu lakini nchi hizo hazina mgao wa kutisha wa umeme kama nchi yetu!?
 
Kila mtu anafahamu kwamba seikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe. Kuna nchi nyingi tu ambazo hazina tatizo la umeme kama linalotupiga hivi sasa, lakini kama TZ nchi hizo pia hazina uwezo wa kufanya mvua inyeshe. Kama hii ndiyo thinking ya kiongozi wetu mkuu basi inabidi kukata tamaa kabisa na tatizo la umeme litaendelea kutupiga siku zote hadi watu wenye creative thinking watakaposhika hatamu za uiongozi
 
Hakuna kitu hapo siasa hizo toka 2006 mpaka leo! Kifupi serikali haina mpangilio mzuri wa maendeleleo kwani kila kukicha watumiaji wa umeme wanaongezeka aache kusema awamu zilizopita walizalisha M 600 sasa hivi watanzania tupo zaidi 45milion miji inakua kila siku kimsingi hakuna alichokifanya, yeye alitakiwa kuongeza angalau M800 tusingekua na tatizo la umeme.
 
Usanii ni mwingi zaidi.Ukame kuwa tatizo ndo tatizo lenyewe halisi aliloulizwa kuwa wamelifanyia kazi gani.Katumia loophole hapo na kudai matatizo ni mvua coz anajuwa wananchi wanaongozwa kiimani imani,kwamba mambo ya mvua ni mambo ya Mungu!Wananchi wengi wasioelewa wataona Rais anaonewa...Kwasababu wanaamini ni kweli Mh Rais hana "nguvu za Mungu" za kuleata mvua.Na hata wengine watasema ukosekananaji wa mvua ni tatizo linalohitaji maombi,kwamba yawezekana ni laana za Mungu..Hawajui kuwa kutotafuta ufumbuzi wa kupata umeme ambao hautegemei mvua ndo kosa kubwa la Mh Rais.

Pia kasema tatizo ni ukame at the same time kudai kuna njia nyingine wanazishughulikia ambazo ni mbadala wa maji.keshakiri kuwa tatizo siyo ukame peke yake,maana kama ni ukame peke yake asingegusia hizo issue za umeme wa jua huko singida na makaa ya mawe elsewhere.Amesema wamezalisha umeme wa megawatts 300 toka 2009 hadi leo kulingansiha na megawatts 600 zilizozalishwa tokea tupate uhuru hadi 2009.Kwa maana hiyo bado anachukua credit na at the same time anadai tatizo ni mvua.Kama si cheusi chekundu kwa watanzania ni kitu gani?Kwasababu kama umeweza kuongeza umeme wa megawatts 300 bila kujali kuwa kulikuwa na ukame ama ukosefu wa mvua,then si inammanisha kuwa mmeweza kuli overcome hilo tatizo?Maana kama sivyo,then quit taking credits since mvua ni mambo ya Mungu na huwezi kuileta.

Tatizo siyo maji,tatizo ni viongozi waloshindwa kutupatia alternatives zenye kukidhi matarajio ya matumzi yetu.Alitakiwa akiri kwamba wanalishughilkia tatizo la umeme kwa kujaribu kupata other alternatives to the water ones,i.e the ones that depends on rain.Kudai kuwa umeme wa mabwawa pekee ndo unaotegemewa na huku akijipa crediti kwa serikali yake kupata umeme wa nishati nyinginezo ni usanii toka kwa Mh rais.

Hakutakiwa kudai kuwa tatizo ni ukame na wakati akijua kwamba tatizo ni kutokuwa na alternative other than umeme unaotegemea mvua.Very incompetent from the president.Angesema tu tunatafuta other alternatives ila tatizo ni muda.Lakini hawezi kusema hayo kwasababu njia ya mwongo ni fupi.
 
Watanzania wote wangekua kama mimi uyo sharobaro hastahili kumalizia muda uliobaki apo ikulu coz jamaa ni useless eti anasema serikali haiwez kuleta mvua kweli ana akili uyu vp kuhusu mabilion ya richmond na dowans wahucka wangeadhibiwa na pesa zikaingia kwenye issue ya umeme tatizo lisingekua kubwa kias hiki ila jamaa ye kucheka any time interview yote linacheka tu eti ukame hovyoo.
 
Hakuna kitu hapo siasa hizo toka 2006 mpaka leo! Kifupi serikali haina mpangilio mzuri wa maendeleleo kwani kila kukicha watumiaji wa umeme wanaongezeka aache kusema awamu zilizopita walizalisha M 600 sasa hivi watanzania tupo zaidi 45milion miji inakua kila siku kimsingi hakuna alichokifanya, yeye alitakiwa kuongeza angalau M800 tusingekua na tatizo la umeme.
Nakubaliana na hilo la miji kukuwa,populations kuongezeka nk. Pia anapodai kuongezeka huko kwa uzalishaji bila kusema ukweli huo kuwa watumiaji wa umeme nao wameongezeka na bado wanaendelea kuongezeka ndiyo utajuwa kuwa viongozi wetu hawajali kuhusu future ya Taifa letu na wala hawana habari kabisa ya nini wanatakiwa kukifanya for the nation.They cant even project/Forecast anything.Ni wazi walichozalisha hakiendani na mahitaji yaliyopo kwakuwa hawaku consider future projections/forecast of the consumptions wakati wa maamuzi ya uzalishaji huo.Ni bora liende tu.Kama vile mwana JF alipodai kuwa they cant think beyond the next meal!

Kama pia wanategemea kukuza uzalishaji ndani ya nchi na pia kuwavutia wawekezaji,then ni wazi kuwa wangelishughulikia swala la uememe kwani hilo ni miongoni mwa top priorities za wawekezaji,na pia kwa Taifa ambalo tunatakiwa kuvikuza viwanda vya uzalishaji,hilo ni pigo kubwa sana na watalijutia i can almost guarantee you.

Kama hamna umeme nchi imekufa,hilo liko wazi.Hkauna mwekezaji atayekwenda kwenye nchi yenye umeme wa kubahatisha na wakati umeme ndo unategemewa kwenye uzalishaji!Nchi ikifa kiuchumi ndo kwishe.Hakuna serikali itayaoweza ku withsatand hilo,na ndiyo maana nashangazwa sana na kutokujali kwake ama kutokuwa kwake na knowledge ya nini kinachoendelea na kipi kifanyike ili tuweze ku overcome.Kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na hilo tatizo hilo kutamcost yeye na serikali yake maana hiii si issue ya kuichezea.Lets wait n c.
 
HTML:
" Sababu ya kukosekana kwa umeme nchini ni uhaba wa mvua, na serikali haiwezi kutengeneza mvua! " - Dr Jakaya Kikwete
 
To hell,i realy hate Mr P+ wasaidizi wake!very little IQ in analysing matters
 
Back
Top Bottom