Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,010
- 2,604
Si kweli kwamba upinzani umeishiwa pumzi ila umehujumiwa kwa mtazamo wangu.Kiukweli kwa sasa upinzani ni kama umeishiwa pumzi na kuendelea kuulea ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kisingizio cha ruzuku.
Je, hakuna haja ya kuitishwa upya kwa kura ya maoni kuona kama watanzania bado tunauhitaji mfumo wa vyama vingi vya siasa?
Jumamosi njema
Maendeleo hayana vyama!
Wazo lako si baya ila kabla ya hiyo kura tuvipe usawa vyama vipige kameni sawa kujieleza kwa nini visifutwe.
tufanye mabadiliko ya hiyo tume itakayosimamia uchaguzi huo iwe huru na haki isiyo na maslahi pande zote.
Uundwaji wa hii tume;
1. Kila chama kiwe na wawakilishi sawa (observer) wenye maslahi na vyama vyao katika kila hatua muhimu ya zoezi la hiyo kula.
2. Vyama vishirikishwe katika kumteua na kumchagua mwenyekiti wa tume hiyo na asiwe na maslahi na chama chochote (neutral) Mwenyekiti wa tume hiyo apatikane kutokana na njia vyama vitakavyoona inafaa.
Nadhani kwa nafasi hiyo wakishindwa wataridhia ombi lako.
Sent using Jamii Forums mobile app