SoC04 Mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi na kuhuisha taarifa za shinikizo la damu za Watanzania ili kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza

Tanzania Tuitakayo competition threads

derajdegreat

New Member
Apr 23, 2024
4
2
UTANGULIZI

Magonjwa yasiyoambukizwa ni magonjwa ambayo hayatokani na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani, magonjwa yasiyoambikizwa yanaongoza kwa kusababisha vifo duniani kote ikiwemo Tanzania. Vifo 32 kati ya 100 duniani kote husababishwa na magonjwa yasiyo ambukizwa na kwa Tanzania vifo 13 kati ya 100 husababishwa na magonjwa hayo, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani ya mwaka 2023.

Magonjwa yasiyoambukizwa yapo mengi lakini magonjwa manne kati ya hayo yanachangia kwa asilimia 80 ya vifo vyote vinavyosababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa. Magonjwa hayo ni saratani, magonjwa ya mfumo wa upumuaji,magonjwa ya moyo na kisukari( ikiwemo magonjwa ya figo yanayotokana na kisukari). Magonjwa haya yamekua mzigo kiuchumi kwa serikali katika sekta za afya na kwa familia zenye waathirika wa magonjwa haya.


KWANINI TUANGALIE ZAIDI SHINIKIZO LA DAMU?

Tafiti zinasadiki kua ongezeko la shinikizo la damu linaongoza kwa kusababisha magonjwa ya moyo na pia linaongeza uwezekano wa mtu kupata kisukari na magonjwa ya figo. Lakini pia tafiti iliyofanyika mkoa wa mwanza mwaka 2020 ilibaini watu 65 kati ya watu 100 waliopimwa na kukutwa na shinikizo kubwa la damu hawakuwa wanajua kua wana tatizo hilo. Hii naonyesha asilimia kubwa ya watanzania wanaishi na matatizo ya ongezeko la shinikizo la damu pasina wao wenyewe kufahamu. Hali hii inasababisha watu wengi kujikuta tayari wakiwa katika magonjwa haya ya kuambukizwa yanayosababishwa na ongezeko la shinikizo la damu.

Kitu cha kufurahisha ni kwamba, “SHINIKIZO LA DAMU HALISABABISHI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA KWA SIKU MOJA”, yaani inahitaji mda kwa tatizo la shinikizo la damu kusababisha magonjwa ya moyo, kisukari na magonjwa ya figo. Lakini pia “ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU HALITOKEI GHAFRA”. ongezeko la shinikizo la damu hutokea kwa hatua, na hatua za mwanzo zinaweza kudhibitiwa kirahisi kwa kubadilisha mitindo ya maisha au kwa kutumia madawa kidogo tu.

Kwa kusema hayo ni wazi kua TUKIWEZA KUWAGUNDUA WENYE ONGEZEKO LA DAMU MAPEMA, TUTAWEZA KUZUIA ONGEZEKO ZAIDI, NA PIA TUTAWEZAKUZUIA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA AMBAYO YANGESABABISHWA NA ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU.

MFUMO UTASAIDIA VIPI NA UTAFANYAJE KAZI?

Kwa bahati nzuri serikali imeanzisha utaratibu ambao huduma za afya zitamfikia kila mtu alipo kupitia wahudumu wa afyangazi za jamii. PENDEKEZO NI KUA uchaguliwe mkoa mmoja(wa majalibio kwa mfumo huu kabla ya kutumika nchi nzima) kati ya kumi iliopangwa kupata wahudumu wa afya ngazi ya jamii, kisha Pamoja na majukumu watakayopewa waelekezwe namna ya kupima shinikizo la damu kwa kutumia mashine za kidijitali (digital sphygmomanometer) wakisimamiwa na wauguzi wachache katika zoezi hili. Baada ya kuelekezwa, kwa kila kitongoji kama watakavyokua wamepangiwa wapime watu wazima wote(umri juu ya miaka 18) wa kitongoji na zoezi hili lifanyike kwa mkoa huo mzima.

Baada ya zoezi hilo watakao kutwa na shinikizo kubwa la damu waanzishiwe matibabu, na watakaokutwa katika hatua za kuongezeka kwa shinikizo wapewe elimu ya kubadilisha mtindo wa maisha. Watu hawa taarifa zao ZIHIFADHIWE KATIKA MFUMO WAKIELEKTRONIKI na wapimwe tena baada ya wiki moja (kwa watakao kutwa na shinikizo kubwa la damu) na baada ya mwezi mmoja (kwa watakao kutwa katika hatua za ongezeko). Na kwa watakaokutwa na shinikizo la damu likiwa salama warudie kupimwa baada ya miezi sita nao taarifa zao zihifadhiwe kwaajili ya kuzirejea kujua uelekeo wa shinikizo lao la damu. Taarifa katika mfumo wa kielektroniki ziambatanishwe na anuani ya makazi na namba ya simu ya mkononi ya kila aliepimwa.

Mfumo huo wa kielektroniki utengenezwe kwa namna ambayo utapangilia muonekano wa taarifa kuanzia watu mwenye ongezeko kubwa la damu na wawekewe alama nyekundu, wakifuatiwa na watu wenye hatua za awali za ongezeko na wawekewe alama ya njano, na mwisho watu wenye shinikizo la damu salama wawekewe alama ya kijani.

Katika mfumo huo kuwe na timu ya wasimamizi wa taarifa hizo(data managers) kuanzia ngazi ya kata ambapo wanaweza kua baadhi ya wauguzi na madaktari wa kata hio. Hawa kazi yao itakua kuingia katika mfumo na kuona ni nani na yupo wapi ambaye shinikizo lake la damu lipo katika hatua za kuongezeka au tayari limeongezeka. Kwa kuona hivo wata wasiliana na watu hao kuwaita siku maalumu na kuwapa elimu ya jinsi yakudhibiti ongezeko au kuwaanzishia dawa kutegemeana na matokeo ya vipimo. Pia kuwe na wasimamizi wa taraifa ngazi ya wilaya na mkoa ili kusimamia ufanisi wa zoezi hili. Mfumo utawaruhusu wasimamizi ngazi ya wilaya na mkoa kupata ripoti ya wilaya nzima na mkoa mzima(kutokea kila kata). Ripoti ya kielektroniki itaonyesha ufanisi wa kila kata katika kupunguza idadi ya watu wenye alama nyekundu na njano kwenda kijani.Na pia timu ya wilaya na mkoa itaongeza juhudi katika maeneo ambayo yanaonyesha maendeleo hafifu ya kupambana na shinikizo la damu.

FAIDA ZA MFUMO HUU

1 Itaongeza unafuu kwa kudhibiti magonjwa yasiyoambukizwa yasitokee kuliko kujikita kuyatibu.
2. Mfumo utahitaji wahudumu wa afya wachache katika kudhibiti kuliko wengi ambao wangehitajika ikiwa watu wataugua magonjwa yasiyoambukizwa.
 
Kwa kuona hivo wata wasiliana na watu hao kuwaita siku maalumu na kuwapa elimu ya jinsi yakudhibiti ongezeko au kuwaanzishia dawa kutegemeana na matokeo ya vipimo. Pia kuwe na wasimamizi wa taraifa ngazi ya wilaya na mkoa ili kusimamia ufanisi wa zoezi hili. Mfumo utawaruhusu wasimamizi ngazi ya wilaya na mkoa kupata ripoti ya wilaya nzima na mkoa mzima(kutokea kila kata).
Msisitizo utolewe hasa kwenye elimu, tiba ya madawa ni pale ambapo imebidi.

Tusifanye kosa la kupima sana (screening) halafu hatujajiandaa na mzigo wa wagonjwa wapya watakaopatikana.

Hata hivyo kikanuni tu haitakiwi kufanya 'screening' bila mpango wa tiba.

Uzuri ni kwamba magonjwa yasiyoambikizwa huwa yanahitaji zaidi elimu kuliko dawa. Na ni rahisi kusambaza elimu mfano: Kuwaelekeza watu wawasikilize akina Profesa Janabi ama Dokta Fredrick Mashili (JamiiAfya) kwa ajili ya afya na mazoezi. Elimu inawafikia watu weeeeeeeeeengi kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom